sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Mchawi kiukweli hana akili, mtu umelala zako usiku ukidhani wengi mmelala kumbe ndi kwanza kuna watu hutumia huo mwanya kujiandaa kuja kukusumbua usiku.
Nakumbuka nikiwa kijana mdogo (miaka 22) nlichoka kukaa hostel za chuoni nikaenda kupanga ghetto mtaani ili niwe na uhuru zaidi kumiliki chumba changu, kujipikia, yani kiudupi kuwa na mamlaka zaidi hasa pale nilipokuwa nimepata mchumba kama yalivyo matamanio ya vijana wengi katika huo umri.
Sasa hiki chumba nilichopanga nilikaa kama mwezi bila kero yoyote, kulikuwa pia kuna wapangaji wenzangu wanne ambao pia tulielewana vizuri tu na wala hapakuwa na shida au historia yyote ya ushirikina.
Kabla ya kulala nilikuwa naomba kama kawaida wakuu.
Sasa kuna siku nikiwa naanza kulala naskia kwenye dali kuna vishindo, dakika za mwanzo nilidhani huenda ni panya buku ila nikaona huyu ni mwanadamu kabisa anakimbia, kwa hofu nikatoka nje haraka sana, nilivyotoka tu haikuchukua mda wapangaji wengine wote nao kutoka huku wakilalamika ishu hio hio, kiukweli tulikaa nje mda mrefu kidogo ila tukarudi vyumbani huku tukiwa na hofu, nakumbuka hio siku nililala saa 10.
Hali ilipoa ila baada ya wiki tena hali ikatokea kituko kile kile, nakumbuka ile siku luku ilikata usiku mida ya saa tano kasoro hivi nikiwa natumia laptop, nikasali na nikaingia kulala, usingizi ulivyoaza kutaka kunipitia nlistushwa na vishindo darini na kwa mbali kukiwa na kama sauti za watu wanaoongea lugha nisiyoijua zikiambana na ngoma nyepesi, kiukweli nilihisi moyo wangu unataka kunitoka mdomoni maana ulikuwa unadunda sana, nikasikia milango ya wapangaji wengine inafunguka wanatoka nje nikaona hapa kishanuka ngoja nitoke tu, Mpangaji mwenzetu alinunua luku na hio siku taa hazikuzimwa.
Tukio la 3 na la mwisho katika nyumba hii lililonifanya nihame kesho yake ni baada ya siku kadhaa mbeleni usiku kuna kitu kilipiga juu ya bati mithiri ya kimondo, yani ilisikika PAAAAAH!! sauti kubwa sana, nilichomoka nduki chumbani, wapangaji wengine nao kama kawaida wakatoka nje, ile siku nakumbuka ilikuwaa ndio funga kazi, ile sauti ingeweza kumuamsha hata mlevi alielala fofofo kiukweli, ilikuwa ni kubwa sana,
Nakumbuka nilvyoingia tu chumbani nilianza kukunja nguo zangu usiku huo mida ya saa tisa, nikawa nacheki muvi kwenye laptop maana usingizi uliisha kabisa, siku hio sikwenda hata chuoni nilishinda na madalali kutafta chumba sehem nyingine, Nlipopata chumba nilirudi kule ghetto kwangu na gari flani kubwa kidogo kuzidi kirikuu, nilifungua kitanda, nilitoa mapazia, n.k. Basi ndio nikahama hio sehemu na kwenda sehem nyingine huku nikiwa nimeacha kodi ya miezi mitatu.
Nachoshukuru huyo dalali alientaftia chumba kipya alikuwa ni rafiki yangu na alinifunidisha ujanja kwamba niwe naulizia ulizia kwa boda boda, wauza duka, au watu wa karibu na nyumba nayotaka kuhamia hali yake ipoje hata kama ni kwa kutoa ka rushwa,