Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Na ndio ushawishi wake ni mkubwa sana kwenye kufanya maovu.Pesa ni kama kisu inategemea na matumizi yako.kisu kinaua,kinakata mboga jikoni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na ndio ushawishi wake ni mkubwa sana kwenye kufanya maovu.Pesa ni kama kisu inategemea na matumizi yako.kisu kinaua,kinakata mboga jikoni
Nilifuga Hawa kuku Kuna mpemba akamnunua, kamuweka kaenda nae pembaike, nikaogopa Sana.. special yenye nguvu Sana. Anatofaut Sana strength na wakawaida, kroila ambae miez kadhaa ni mgumu kupta kienyeji yytFollowing
Nilikuwa nafuga kuku huko kusini sasa nikaweka mbegu za kuku kishingo; walifanya vizuri sana lakini jamaa moja akaniambia usifuge hawa kuku hawana soko huku watu hawanunui. Kumuuliza kwanini hakuwa na jibu
Pole sana ndio mambo ya ulimwengu hayo.
Mafanikio yapo kwenda sana kwa mganga na kutofanya kazi kwa bidiiKwahiyo mafanikio yapo kwenye kufanya kazi kwa bidii?
Iringa sehemu gani mkuu,nipe ramani,nina mtu hapa mafinga anakwepa kufanya Kazi miaka miwili na pesa kashakula nusu milioniSikupi connection Ila nakupa Siri ....
Dar es salaam Hakuna mganga kuna Wafanyabiashara..
Dar es salaam Hakuna miti...
Utajiri nenda iringa
mapeNzi nenda mbeya/Tabora
Kinga ya mwili kigoma/ sumbawanga...
Iyo ndio connection yangu kwako.
Kumbe?Mafanikio yapo kwenda sana kwa mganga na kutofanya kazi kwa bidii
HaswaaSijawahi kuelewa logic ya watu waliofanikiwa kuwa wamebarikiwa sana.Na watu ambao hawajafanikiwa kuwa na mikosi au kwa lugha ya makanisa ya kisasa wanasema wamefungwa. Ila Wayahudi hiyo logic kwao inatumika mpaka leo. Kuna vitu vipo ila uhalisia wake jamii inaaminishwa. Mafanikio ni yale yasiyoonekana kwenye macho !
Acha uogaLeo sijui nalalaje😭😭😭 nani alinituma nipite kwa hio thredii😭😭
Uyasemayo ni kweli kabisa kwani wengi waliofanikiwa huku Uswahilini walijikita kwenye ushirikinaSipo hapa kumshawishi mtu aingie kwenye ushirikina, sipo hapa kudharau Imani ya dini ya mtu yoyote. Ila Nipo hapa kusema ukweli.
Watu wanatupa moyo kuhusu mafanikio, wengi wao husema kufanya kazi kwa bidii ndio njia ya mafanikio! Wao huita hiyo ndio Siri!
Lakini Ndugu zangu nipo hapa kuwapa Siri ingine ya mafanikio! Sio kuua mzazi wa kutoa kafara Ila Ni kukulinda. Katika mafanikio au katika biashara yoyote.
Mtu asikuambie mtaji wa laki Tano ndio ulionifanya niwe na nyumba na magari! Tena wanasema nilifanya kazi Sana kwa bidii, na siri ya mafanikio yangu ni kufanya kazi kwa bidiii! Huo ni uongo mtupu.
Siri za mafanikio zipo kwenye Siri ya ushirikina moja, ni wewe kujikinga kupitia ushirikina! Au kukinga biashara yako kwa ushirikina, usipozingatia Ayo maisha yako yatakuwa chini miaka nenda miaka rudi huku ukiona wengine wanashaini
Mchawi kazi yake sio kuroga tu kazi yake ingine ni kurudisha nyuma maisha yako.
Karibuni 2022.
Hata ushuani mkuu watu washirikina sana tuUyasemayo ni kweli kabisa kwani wengi waliofanikiwa huku Uswahilini walijikita kwenye ushirikina
pole sana, ndio kupona hivyo mpendwa.Leo sijui nalalaje😭😭😭 nani alinituma nipite kwa hio thredii😭😭
Ni kweli mkuu, tunaona hata mawaziri na viongozi wengine serikalini na ndiyo maana sitokuja muamini mbunge yeyote maishani mwangu au mwana siasa wa aina yeyote.Hata ushuani mkuu watu washirikina sana tu
Hao ndo balaaNi kweli mkuu, tunaona hata mawaziri na viongozi wengine serikalini na ndiyo maana sitokuja muamini mbunge yeyote maishani mwangu au mwana siasa wa aina yeyote.
AmenUchawi uchawi uchawi aaagh ptuu inachosha sasa..kila sehemu watu wanalia na madhara yatokayo na uchawi.
Mm nashindwa hata kuandika,nimeamua kumuachia Mungu tu kama ataamua kuniacha niendelee kuteswa,kunyanyaswa na kuonja joto ya jiwe na wachawi sawa tu si ameamua iwe hivyo bhana Ila mm nimechoka na sina msaada wowote kutoka popote zaidi yake.
Nimechoka kuona wenzangu wakisonga mbele mm nikiwa nyuma na wamwisho kila siku, nimechoka kudharaulika sababu sina maendeleo kama wenzangu,nimechoka pesa zangu kuishia kwenye matibabu,nimechoka na kuugua maradhi yasiyoisha mwilini mwangu.
Nimechoka kutibia wazazi,nimechoka kutibia wadogo zangu,nimechoka kutibia familia,nimechoka kuishi kwa huzuni na mateso.
Nimechoka kujaza namba za simu za madaktari na manesi,nimechoka kitembelea maduka yamadawa,nimechoka kunywa dawa,nimechoka kugeuza dawa mbadala wa Chakula.
Nimechoka dharau,kebehi,masengenyo na vijembe juu ya uduni wangu unaosababishwa na wao wenyewe,nimechoka nimechoka nimechoka.
Eeh Mungu Mwenyezi,Mfalme wa falme,Mmiliki wa mbingu na dunia na ukazisimamisha pasipo nguzo,Mfalme wa siku ya Malipo,Mwingi wa Rehma mwnye kurehemu.
Ulieniumba mm ukamuumba baba na mama yangu,ukawaumba bibi na babu zangu, ukaumba wanangu,ukaumba ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake,Nakuomba eeh Rabbi uninusuru mm pamoja na kizazi changu chote dhidi ya udhalimu wa shetani na hila Zake zote.
Ewe Mola wangu mtukufu,usieshindwa na chochote mana vyote ni Mali yako,hakuna kilichopo nje matakwa yako,hakuna linalowezekana ila kwa idhini yako..nakuomba uniponywe mm,waponye wazazi wangu, iponyewe familia yangu,iponye jamii yangu liponye taifa langu dhidi ya uchawi, ulozi,ushirikina,na hila zote ovu za shetani.
Ninakuomba utufungulie milango ya rizki zetu ziwe za halali,za wepesi na uzikinge dhidi ya mabaya yoyote.sisi bila ww hatuwezi kitu Mungu wangu.
Tupe afya tuondolee maradhi,tupe Neema tuondolee ufakiri na umaskini,tupe mioyo safi tuondolee chuki na husda,tupe upendo tuondolee huzuni fitna na majungu.
Eeh mola wetu mlezi,mwenye huruma,mwenye upendo na msikivu, tunaomba usikie Dua yetu,tunakuomba usikie kilio chetu.sisi ni wakosefu tu si wakamilifu,ukamilifu unao ww Mungu wetu mtukufu.
Ninaomba yote haya kwa imani yangu kwangu,na kwa imani za wenzangu ila naamini sisi sote tunakutukuza ww kwa njia tofauti.
Amiiin
Amiiin
Amiiin