TANZIA Mchekeshaji Pembe afariki dunia

TANZIA Mchekeshaji Pembe afariki dunia

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
images.jpg
Mzee Yusufu Kaimu mchekeshaji mkongwe maarufu kama Pembe afariki dunia alasiri ya leo jijini Dar es Salaam. Taarifa zimethibitishwa na Msanii wa Filamu, Vincent Kigosi “Ray” na taratibu za mazishi zinafuata.

=====

Mwigizaji na Mchekeshaji Mkongwe Nchini Tanzania, Mzee Yusuph Kaimu maarufu Pembe amefariki dunia jioni ya leo October 20,2024 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Baadhi ya Waigizaji akiwemo Vicent Kigosi (Ray) na Mau Fundi wametoa taarifa za msiba huo na kusema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye, @AyoTV_ imeongea pia na Katibu wa Chama cha Waigizaji Kinondoni, Jafari Makatu ambaye amethibitisha na kusema “Alikuwa anaumwa alilazwa Temeke Hospital, amefariki kama saa moja iliyopita, alilazwa kama siku tatu nne, na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona Kesho baada ya kuambiwa anaumwa”
 
Je unamaanisha ni huyu ikiwa ndio

R. I. P View attachment 3130856
Asee. Apumzike kwa amani. Kwa wakati wao kama KAOLE SANAA GROUP ! walitupa burudani kwa hakika , siyo maigizo au sinema za wakati huu ni mambo ya mapenzi tu.

Kwa sasa hivi huwezi kuwaachia watoto Tv wachague program wenyewe bila Parental Guide unless umeamua kuwaachia wenyewe wajifunze ujinga.
 
Back
Top Bottom