Ila sisi kama wanajamii tunahitaji kujiongeza sana eneo la wasanii kwa jinsi tunavyowatreat.
Huyu gwiji wa uchekeshaji nimeanza kumuona nikiwa bwana mdogo sana tena vidudu. Alikuwa akituchekesha kila ijumaa channel ya CTN.
Yeye Mzee Pembe,Mzee Small,TupaTupa,na Bi Chau. Hawa watu wametufanya siku zetu kuwa za furaha sana kwa vitu na vibweka vyao ambavyo walifanya bila ushawishi wowote ila tu kwa kuchagua kuwa sehemu ya watoa burudani katika jamii.
Cha ajabu watu hawa hufariki katika maisha ya ufukara na kujipapasa bila msaada wowote ule huku wakiwa hawana vyanzo vya mapato kutokana na kazi zao hizi ambazo wamezifanya kwa utashi na kujitolea kwa hali ya juu.
Nadhani ingekuwa ni busara sana kama taasisi au vijana tungekuja na ubunifu wa kimfumo ili hawa watu waweze kupata matunda ya kazi zao in the future ili iwe kama shukurani kwa zawadi yao ya furaha wanayotupatia bila kujua.
R.I.P Legendary Pembe.