TANZIA Mchekeshaji wa muda mrefu Sobogani Zabron maarufu Erick Kisauti amefariki Dunia

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731

Mchekeshaji wa muda mrefu Sobogani Zabron maarufu Erick Kisauti amefariki Alfajiri ya leo akiwa nyumbani Kwa Ndugu zake Kibaha Mkoani Pwani.

Mchekeshaji mwenzie, Masai Nyota aliyewahi kufanya nae kazi mbalimbali za sanaa ambaye amesema ni taarifa za ukweli na amezipokea asubuhi ya leo na kwamba kwa sasa anajiandaa kuelekea Kibaha mahali ulipo.

“Msiba upo Kibaha hapa ndio tunajiandaa kuchomoka kwenda mimi natokea nyumbani kwangu Chanika, nilipata taarifa za karibu kutoka kwa Camera Man Yoso tuliyekuwa nae Kwenye kambi ya vituko show, aliniambia anaumwa TB kuna kipindi akaanza kukaa sawa lakini baadae kansa ya ngozi ikaibuka, leo Alfajiri napigiwa simu naambiwa amefariki Alfajiri, nyumbani”
 
Daah, Apumzike pema, mwendo ameumaliza.
 
Apumzike kwa Amani. Wote ss njia ni hiyo.
 
Buriani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…