Mchele 3200kg, maharage 3000kg na mahindi 100 yamefika 140k

Mchele 3200kg, maharage 3000kg na mahindi 100 yamefika 140k

Mchele ukifika kg 5000 na maharage 4000 na unga 2500, tutagundua chakula mbadala...
 
Kla mtu atakula kwa urefu wa kamba yake wakulima kla sku wanalia bei za mbegu na pembejeo zmepanda bei na hakuna ata mwananchi anaewasaidia wala kuwaongelea
Sasa saiv wanauma mazao yao kwa bei nzuri wananchi mnataka kuruma na kulia lia.
Nunueni tu mkishindwa ingieni na nyie shamban mlime
Nahis hata hiyo bei ya mchele kilo 3500 haimgusi mkulima directly. Mfano mchele wa mbagara unagharama za usafirishaji,ukoboaji,pakia na pakua ya mazao kwenye mifuko,mbolea na mbegu na madawa mengine.
 
Jpm alikua na mbaraka tangu aingie madarakani nchi haikuwahi kuwa na ukame..pia alijitahidi kuzuia uuzwaji holela wa mazao nje ya nchi.

Ukidhibiti chakula maisha hayawezi kuwa magumu.

Sasa wahuni walichokifanya..mvua chache bado wakafungua mipaka yote..unategemea nn hapo zaidi ya maumivu.

#MaendeleoHayanaChama

Ulikuwa nje ya nchi nini, unajua ukame uliokuwepo 2016? Au kwakuwa ulikuwa kwenye ulaji wakati akiwa madarakani, unadhani kila mtu alikuwa kama wewe? Unadhibiti wakulima kuuza nje chakula kwani umewasaidia kulima? Kwanini hampangii watu namna ya kutumia mishahara yao, bali mnataka kuwapangia wakulima wapi pa kuuza mazao yao?
 
Mfumuko wa bei hasa mazao ya chakula unatisha!

Mfano kilo ya mchele sasa imefika shilingi 3200kg na maharage 3000kg. Kuhusu mahindi ndiyo usiseme kabisa maana gunia la kilo 100 linauzwa laki na arobaini.

R.I.P JPM.

Nimetoka huko sokoni mwenyeweeeee
Maharage 3000
Mchele 3000

Suzy Elias leo umemkumbuka dad😆😆😆

Ila usisahau Yapo mambo mengi yanachangia haya mambo
 
Viongozi wa sasa ukimtaja tu JPM ndo wanaongeza pamba masikioni afu wanakunja ndita[emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]

Sijui aliwakosea nn, hata MAZURI yake hawataki yasikia!!!!!!
Honestly tunakoelekea sikoo!ifike mahali wakubali tu JPM aliwazidi pakuubwa mno!shida ya Yule mzee ni watumishi na matajiri tu ndo aliwafungia Busta ,huku chini At least waliinjoi!mchele kutoka 1300 mpk 3000 na kuendelea.
Kiukweli Serikali inafeli Sanaa kudhibiti mfumuko wa Bei kisingizio kisiwe Vita wala Nini inshort maza Hana mda na nchi na hua Hawazi tu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Asilimia kubwa mapito tunayopitia sasa hivi kama nchi, madhara yameanzia kwenye utawala wa Magu. Alivuruga sana upande wa zao la korosho. Pia kwenye mahindi akazuia wakulima kuuza nje, hii iliyumbisha sana mitaji ya wakulima wengi.

Unajua tatizo tulilonalo watanzania wengi ni wabinafsi sana,tena sana. Imagine mtu analima msimu mzima kwa tabu, anatumia gharama zake, alaf inapofika muda wa kuuza mazao walau arudishe gharama zake na faida, analazimishwa kuuza kwa Bei ya chini ili kunufaisha walaji. Walaji wanaweza kuona serikali imefanya jambo jema kwavile wao wanapata chakula, ila haiangalii upande wa mkulima.

Serikali ilichotakiwa ni either kununua Yale mazao kwa Bei nzuri ili isimlalie mkulima, au waweke mazingira mazuri kwa wakulima kwa kuwapunguzia gharama za pembejeo za kilimo, ili kipindi cha mavuno basi wasiwe kwenye ulazima wa kuuza mazao Yao kwa gharama kubwa.

Mvua na hali ya hewa sio kitu pekee kilicho sababisha vyakula kupanda, baada ya seke seke zilizopita, wakulima wengi wamelima kwa kiwango kidogo kwa kuhofia kutumia gharama kubwa alaf return iwe ndogo. Lakini pia kupanda kwa Bei ya mbolea, imelimit wakulima na kiwango cha ulimaji.
Wewe acha uongo, kipindi cha Magufuli watu walilima sana maana alipita mikoani na kuwaambia mtu asiye fanya kazi atakufa kwa njaa Maana Serikali aina shamba la chakula,na akawambia wakuu wote wa Mkoa wataokao tangaza njaa kwenye Mkoa wake huyo atakuwa amejifukuzisha kazi,hivi viongozi wote mikoani waliakikisha kila mtu anashamba la mazao hasa maindi, hivyo chakula kikawa kingi kwenye masoko mpaka mazao mengine yakakosa soko,ameingia Samia akapandisha mbolea mfuko yaliokuwa unauza elfu 60,000/ukapanda adi 120,000/watu wengi wakashindwa kulima ndio Maana unaonashoterge ya chakula kwenye masoko, Sasahivi vijana wameacha kulima wamewachia wazee Maana fedha za bure zimerudi mtaani
 
Mfumuko wa bei hasa mazao ya chakula unatisha!

Mfano kilo ya mchele sasa imefika shilingi 3200kg na maharage 3000kg. Kuhusu mahindi ndiyo usiseme kabisa maana gunia la kilo 100 linauzwa laki na arobaini.

R.I.P JPM.
Hivi huku ndiko kuisoma namba au?
Wanaoisoma namba ni wapizani na wasio na chama au hata watu wa chama dola wale wadogo wadogo nao wanaoisoma namba???
 
Attachments

  • CCM MBELE KWA MBELE CAPTAIN JOHN KOMBA(720P_HD).mp4
    17.7 MB
Tatizo kilimo kinapuuzwa sana na vijana walio wengi ukiwambia swala la kulima wanakuona Kama niwazamani sana, kwahiyo wakulima wamekuwa wachache ambao nao kwa % kubwa wanalima Kwa kujikimu wenyewe huku vjjn through out the year Hakuna mtu anayenunua maharage wala mahindi vitu vyote kila familia inavyo, na mtu anayelima anauza ili apate kianzio Cha msimu mwingine wa kilimo. Elimu itolewe zaidi tujiajiri kupitia kilimo
 
Mwakani mambo yawezakuwa mabaya zaidi maana shambani mambo simazuri na nchi jirani wananunua mazao kwafujo
 
Honestly tunakoelekea sikoo!ifike mahali wakubali tu JPM aliwazidi pakuubwa mno!shida ya Yule mzee ni watumishi na matajiri tu ndo aliwafungia Busta ,huku chini At least waliinjoi!mchele kutoka 1300 mpk 3000 na kuendelea.
Kiukweli Serikali inafeli Sanaa kudhibiti mfumuko wa Bei kisingizio kisiwe Vita wala Nini inshort maza Hana mda na nchi na hua Hawazi tu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Gunia la mpunga lilinunuliwa 40,000 ,saiz 100,000.

Na hakuna anaezuia food kuuzwa nje wakat Kuna uhaba soko la ndani!!!
 
Sawa, na je vp kuhusu kilo moja ya mchele kwa sasa Nairobi?
Mfumuko wa bei hasa mazao ya chakula unatisha!

Mfano kilo ya mchele sasa imefika shilingi 3200kg na maharage 3000kg. Kuhusu mahindi ndiyo usiseme kabisa maana gunia la kilo 100 linauzwa laki na arobaini.

R.I.P JPM
 
Putini anawaza kumaliza vita
 
Back
Top Bottom