Mchengerwa amwagiza daktari Temeke kufunga Duka la Dawa pembezoni mwa Hospitali

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema hatavumilia tabia ya baadhi ya madaktari wa hospitali za Serikali kuwaelekeza wagonjwa kununua dawa kwenye maduka binafsi.

1769496159030.png
Amesema akimtaja daktari mmoja wa Hospitali ya Temeke anayemiliki duka la dawa jirani na hospitali hiyo na kumuagiza alifunge mara moja kabla hajachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Ninazo taarifa za daktari mmoja katika Hospitali ya Temeke mwenye duka la dawa jirani na hospitali namwagiza alitoe mara moja kabla sijamtoa yeye,” amesema Mchengerwa.

1769496309438.png
Mchengerwa amesema Bohari ya Dawa (MSD) ina uwezo wa kutosha wa kusambaza dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zote za Serikali, akisisitiza kuwa Serikali imewekeza vya kutosha kuhakikisha dawa zinapatikana bila kikwazo.

Akizungumza Jumatatu, Januari 26, 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha Afya Kaloleni jijini Arusha, Waziri huyo ameagiza Halmashauri ya Jiji la Arusha kuanza mchakato wa maombi ya kukipandisha hadhi kituo hicho kuwa Hospitali ya Wilaya baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la ghorofa tano.

Amesema msongamano mkubwa wa wagonjwa alioukuta katika kituo hicho ni kikwazo kwa utoaji wa huduma kwa wakati, na kusisitiza kuwa Serikali haina nia ya kuona wananchi wakikaa muda mrefu kwenye foleni badala ya kushiriki shughuli za uzalishaji.

Chanzo: Mwananchi Digital
 
Serikali ya ajabu.....
Hakuna Hospitali Tanzania yenye dawa zote....
Hapo ni kuwaambia wagonjwa waende kununua dawa mbali zaidi

Pia sio kosa mtumishi kuwa na biashara....

Labda uchunguzi ufanyike..kujua kama anawalazimisha wagonjwa Kwenda nje..hapo itakuwa kosa
Na najua Pharmacy Council wataandika barua ya kusimamisha Hilo duka...maana hawana namna
 
Ndo shida ya kuiba chaguzi na kulazimisha kuwatawala watu kwa mabavu.

Akili hamna alafu mnalazimisha kuwa Viongozi. Hospitali zenu hazina dawa, kila siku mnahamasisha watu wajiajiri na kufanya uwekezaji. Alafu nyie nyie ndo mnalazimisha kufunga biashara za watu.

Pumbavu kabisa.
 
Mean while wao wanafungua sheli karibu na Huduma Za kijamii na makazi ya watu na hakuna wa kuwafungia
 
Ndo shida ya kuiba chaguzi na kulazimisha kuwatawala watu kwa mabavu.

Akili hamna alafu mnalazimisha kuwa Viongozi. Hospitali zenu hazina dawa, kila siku mnahamasisha watu wajiajiri na kufanya uwekezaji. Alafu nyie nyie ndo mnalazimisha kufunga biashara za watu.

Pumbavu kabisa.

Hapo anataka kuhalalisha kua kukosekana kwa dawa hosp. kunachangiwa na hilo Duka

Kumbe ni yeye hajanunua dawa za kutosha
 
Drama tu hzo toka awamu ya tano hayo maduka yalipigwa marufuku lakini sasa karbu hospitali zote nchini maeneo ya karibu kuna maduka ya dawa..tena ajabu zaidi wahudumu wa hospital hzo wanajua dawa zote zinazopatikna kwenye maduka hyo..Utasikia muhudumu anakwambia nenda kanunua pale X pharmacy hz dawa zinapatikana pale..sasa unajiuliza muda wote yupo kazini anajuaje X pharmacy kuna hzi dawa?
 
Ni either ni maduka yao au ni businesa partner wao, Hata mm ningekua Dr. Lazima nifanye hicho kitu.

Kwasababu hata usiponunua dawa duka la nje hapo, Utaenda kununua tu sehemu nyingine maana hosp. hakuna dawa.
 
Kwamba kuna dawa hospitali ila wagonjwa wanaenda kununua pharmacy za nje? Hayo maduka ya dawa yalifunguliwa bila vibalu? Unalifunga kwa misingi ipi?
 
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema hatavumilia tabia ya baadhi ya madaktari wa hospitali za Serikali kuwaelekeza wagonjwa kununua dawa kwenye maduka binafsi.

Amesema akimtaja daktari mmoja wa Hospitali ya Temeke anayemiliki duka la dawa jirani na hospitali hiyo na kumuagiza alifunge mara moja kabla hajachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Ninazo taarifa za daktari mmoja katika Hospitali ya Temeke mwenye duka la dawa jirani na hospitali namwagiza alitoe mara moja kabla sijamtoa yeye,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema Bohari ya Dawa (MSD) ina uwezo wa kutosha wa kusambaza dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zote za Serikali, akisisitiza kuwa Serikali imewekeza vya kutosha kuhakikisha dawa zinapatikana bila kikwazo.

Akizungumza Jumatatu, Januari 26, 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha Afya Kaloleni jijini Arusha, Waziri huyo ameagiza Halmashauri ya Jiji la Arusha kuanza mchakato wa maombi ya kukipandisha hadhi kituo hicho kuwa Hospitali ya Wilaya baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la ghorofa tano.

Amesema msongamano mkubwa wa wagonjwa alioukuta katika kituo hicho ni kikwazo kwa utoaji wa huduma kwa wakati, na kusisitiza kuwa Serikali haina nia ya kuona wananchi wakikaa muda mrefu kwenye foleni badala ya kushiriki shughuli za uzalishaji.

Chanzo: Mwananchi Digital
Amekosea sana Waziri na inabidi kuifunga hiyo pharmacy. Naamini amejazwa majungu na washindani wa mwenye hiyo pharmacy.
 
Kama nyumban kwako unatoa huduma ZOTE kwa 100% hakun mwanafamilia ataend kwa jirani
kabsa yani, wenyewe wazingatie tu huduma zote na dawa zote vipatikane mda wote vituo vya afya.
Waone kama hayo maduka yatakuwepo karibu na vituo vya afya.
 
Back
Top Bottom