PreGE2025 Mchengerwa: Anayedhani anaweza kutingisha kiberiti, ajaribu na atakiona

PreGE2025 Mchengerwa: Anayedhani anaweza kutingisha kiberiti, ajaribu na atakiona

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kuchukua hatua kali dhidi ya watu ambao wamekuwa wakihusika na uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.

Mchengerwa ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Lwanjilo, akiwa kwemye ziara yake ya siku moja mkoani Mbeya, ambapo amesema serikali haiwezi kumvumilia mtu yeyote anayeleta chokochoko kwa kutikisa kiberiti kwa mambo ya uvunjifu wa amani tuliyo nayo iliyoasisiwa na viongozi wetu Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na Amani Abeid Karume.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Awali akiwasikisha taarifa ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Lwanjilo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ericah Yegela amesema ujenzi wa shule hiyo unaoghalimu zaidi ya billioni moja unakwenda kusaidia wanafunzi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata elimu.

 
Waziri mshamba kuliko mawaziri wote

Awaulize wakina mpina, bashiru, polepole na ndungai walivyokuwa na kiburi sasahivi wanacho?

Ushamba wa madaraka
Kuoa mtoto wa Rais ndo kunamfanya awe na kiburi hivyo. Anajiona nchi yote ipo mikononi mwake. Anaona wananchi wote na vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko mkononi mwake kwa sababu tu ameoa mtoto wa Rais.

Wakati utamfundisha.
 
Mchengerwa ametoa maagizo hayo

TOKA MAKTABA :

11 March 2025
Villamor Airbase, PH

IMETHIBITISHWA SASA NDEGE INAYOMCHUKUA MSHUKIWA DUTERTE IMESHAONDOKA KUELEKEA THE HAGUE UHOLANZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=OgIVlTtNRXk

Rais Marcos Junior wa Philippines amethibitisha kuwa rais wa zamani Duterte baada ya kushikiliwa kwa muda na mamlaka ya serikali ya The Philippines ili ijiridhishe kuipitia kwa umakini hati ya Interpol ya kumkamata Duterte kama imekidhi vigezo vyote vya kisheria vya taifa la the Philippines pia vigezo vya kimataifa.

Baada ya kutimiza zoezi hilo la kuipitia hati ya kumkamata ya Interpol kama ziko vizuri, na kuridhika ipo sawa, baadaye mamlaka za The Philippines ikahakikisha inampa haki zote za kiraia rais mstaafu Duterte ya nafasi ya kuonana na mkewe mpendwa pia kuagana na familia kabla ya kupandishwa ndege kwenda ICC Hague ..

Rais Marcos Junior alipohojiwa baada ya kuthibitisha kuwa Duterte ameondoka katika anga la ndege la the Philippines kuwa kupelekwa kwa Duterte hadi Mahakama ya Kimataifa ya The ICC kama ni mbinu ya kisiasa kumuondosha Duterte nchini The Philippines.

Rais Marcos Junior amesema hilo siyo kweli kwamba wamemtosa mpinzani wao Duterte, bali ni sehemu ya kuhakikisha haki inapatikana kupitia mfumo wa haki jinai ya kimataifa kwa pande zote mbili yaani upande wa rais mstaafu Duterte anayeshutumiwa, na upande mwingine wale walalamikaji raia wa the Philippines waliowasilisha malalamiko yao Mahakama ya Kimataifa Dhidi ya Uhalifu ya ICC The Hague Uholanzi.
 
TOKA MAKTABA :

11 March 2025
Villamor Airbase, PH

IMETHIBITISHWA SASA NDEGE INAYOMCHUKUA MSHUKIWA DUTERTE IMESHAONDOKA KUELEKEA THE HAGUE UHOLANZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=OgIVlTtNRXk

Rais Marco Junior wa Philippines amethibitisha kuwa rais wa zamani Duterte baada ya kushikiliwa kwa muda na mamlaka ya serikali ya The Philippines ili ijiridhishe kuipitia kwa umakini hati ya Interpol ya kumkamata Duterte kama imekidhi vigezo vyote vya kisheria vya taifa la the Philippines pia vigezo vya kimataifa.

Baada ya kutimiza zoezi hilo la kuipitia hati ya kumkamata ya Interpol kama ziko vizuri, na kuridhika ipo sawa, baadaye mamlaka za The Philippines ikahakikisha inampa haki zote za kiraia rais mstaafu Duterte ya nafasi ya kuonana na mkewe mpendwa pia kuagana na familia kabla ya kupandishwa ndege kwenda ICC Hague ..

Rais Marcos Junior alipohojiwa baada ya kuthibitisha kuwa Duterte ameondoka katika anga la ndege la the Philippines kuwa kupelekwa kwa Duterte hadi Mahakama ya Kimataifa ya The ICC kama ni mbinu ya kisiasa kumuondosha Duterte nchini The Philippines.

Rais Marcos Junior amesema hilo siyo kweli kwamba wamemtosa mpinzani wao Duterte, bali ni sehemu ya kuhakikisha haki inapatikana kupitia mfumo wa haki jinai ya kimataifa kwa pande zote mbili yaani upande wa rais mstaafu Duterte anayeshutumiwa, na upande mwingine wale walalamikaji raia wa the Philippines waliowasilisha malalamiko yao Mahakama ya Kimataifa Dhidi ya Uhalifu ya ICC The Hague Uholanzi.

Chalamila
 
Huyu na wenzake kwenye kundi la kumpigania Samia asiposema hayo itashangaza sana.

Lakini kujipambanua huko kwa nafasi yake hiyo ndiko kunakozidi kuwafumbua macho waTanzania kuhusu kundi hili linalotaka kuleta mvugano nchini mwetu.
Hawa ndio wavunja sheria wenyewe, hallafu wanageuka na kujitangaza kuwa walinda AMANI (ya matumbo yao)>

Alipovuruga uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa anafikiri watu wataendelea kuwaruhusu hawa mashetani kunyang'anya HAKI za wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka wao?

Kundi hili ni lazima lianze kutazamwa kwa makini na litakapo hatarisha maisha ya waTanzania liweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwanza ni lazima tuwatambue waliomo kwenye hili kundi.
 
Ameshakuwa waziri wa mambo ya ndani.

Ndio wakuu wa mikoa wako chini ya TAMISEMI

Lakini wana majukumu tofauti ya wizara (being strategic implementors wa tasks tofauti za serikali) na ndio maana pia wapo kwenye kamati ya ulinzi (hayo ni majukumu ya mambo ya ndani na ulinzi).

Maana yake ni kwamba uwepo wa wakuu wa mikoa kwenye kamati za ulinzi wa mkoa; maelekezo yao kwenye maswala hayo yanatoka mambo ya ndani au ulinzi.

Isitoshe kamati ya ulinzi ya mkoa inajumuisha RPC na mwakilishi wa jeshi kutokana na issues zake. Watajadili mambo kutokana na tishio la usalama.

Mchengerwa hana mamlaka ya kuwaagiza wakuu wa mikoa kuhusu mambo ya ulinzi na usalama.

Hata siasa zenyewe wanajua basi au majukumu yao zaidi ya kupewa nafasi tu kwa utaratibu wa nepotism.

Sasa sisemi CDM mkawadanganye watu wakaumizwe, watanzania hawako tayari kwa hiyo njia yenu. Muwe na huruma na watoto wa watu.

Alikadhalika kauli ya Mchengerwa ni ya mtu alielewa madaraka.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kuchukua hatua kali dhidi ya watu ambao wamekuwa wakihusika na uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.

Mchengerwa ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Lwanjilo, akiwa kwemye ziara yake ya siku moja mkoani Mbeya, ambapo amesema serikali haiwezi kumvumilia mtu yeyote anayeleta chokochoko kwa kutikisa kiberiti kwa mambo ya uvunjifu wa amani tuliyo nayo iliyoasisiwa na viongozi wetu Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na Amani Abeid Karume.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Awali akiwasikisha taarifa ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Lwanjilo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ericah Yegela amesema ujenzi wa shule hiyo unaoghalimu zaidi ya billioni moja unakwenda kusaidia wanafunzi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata elimu.

Tumekusikia mkwe wa Rais, hakikisha mama anashinda kwa kishindo(sauti ya msisitizo ya Rais mkapa)
Vunja watu miguu,Rais aingie ikulu kwa kishindo
 
Back
Top Bottom