Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kuoa mtoto wa Rais ndo kunamfanya awe na kiburi hivyo. Anajiona nchi yote ipo mikononi mwake. Anaona wananchi wote na vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko mkononi mwake kwa sababu tu ameoa mtoto wa Rais.Waziri mshamba kuliko mawaziri wote
Awaulize wakina mpina, bashiru, polepole na ndungai walivyokuwa na kiburi sasahivi wanacho?
Ushamba wa madaraka
Mchengerwa ametoa maagizo hayo
ChalamilaTOKA MAKTABA :
11 March 2025
Villamor Airbase, PH
IMETHIBITISHWA SASA NDEGE INAYOMCHUKUA MSHUKIWA DUTERTE IMESHAONDOKA KUELEKEA THE HAGUE UHOLANZI
View: https://m.youtube.com/watch?v=OgIVlTtNRXk
Rais Marco Junior wa Philippines amethibitisha kuwa rais wa zamani Duterte baada ya kushikiliwa kwa muda na mamlaka ya serikali ya The Philippines ili ijiridhishe kuipitia kwa umakini hati ya Interpol ya kumkamata Duterte kama imekidhi vigezo vyote vya kisheria vya taifa la the Philippines pia vigezo vya kimataifa.
Baada ya kutimiza zoezi hilo la kuipitia hati ya kumkamata ya Interpol kama ziko vizuri, na kuridhika ipo sawa, baadaye mamlaka za The Philippines ikahakikisha inampa haki zote za kiraia rais mstaafu Duterte ya nafasi ya kuonana na mkewe mpendwa pia kuagana na familia kabla ya kupandishwa ndege kwenda ICC Hague ..
Rais Marcos Junior alipohojiwa baada ya kuthibitisha kuwa Duterte ameondoka katika anga la ndege la the Philippines kuwa kupelekwa kwa Duterte hadi Mahakama ya Kimataifa ya The ICC kama ni mbinu ya kisiasa kumuondosha Duterte nchini The Philippines.
Rais Marcos Junior amesema hilo siyo kweli kwamba wamemtosa mpinzani wao Duterte, bali ni sehemu ya kuhakikisha haki inapatikana kupitia mfumo wa haki jinai ya kimataifa kwa pande zote mbili yaani upande wa rais mstaafu Duterte anayeshutumiwa, na upande mwingine wale walalamikaji raia wa the Philippines waliowasilisha malalamiko yao Mahakama ya Kimataifa Dhidi ya Uhalifu ya ICC The Hague Uholanzi.
Hawa wa hapa bado wanajifikiria kuwa miungu isiyo guswa; kwa kuwa tu wakati huu wameshikilia madaraka.IMETHIBITISHWA SASA NDEGE INAYOMCHUKUA MSHUKIWA DUTERTE IMESHAONDOKA KUELEKEA THE HAGUE UHOLANZI
Tumekusikia mkwe wa Rais, hakikisha mama anashinda kwa kishindo(sauti ya msisitizo ya Rais mkapa)Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kuchukua hatua kali dhidi ya watu ambao wamekuwa wakihusika na uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.
Mchengerwa ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Lwanjilo, akiwa kwemye ziara yake ya siku moja mkoani Mbeya, ambapo amesema serikali haiwezi kumvumilia mtu yeyote anayeleta chokochoko kwa kutikisa kiberiti kwa mambo ya uvunjifu wa amani tuliyo nayo iliyoasisiwa na viongozi wetu Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na Amani Abeid Karume.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Awali akiwasikisha taarifa ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Lwanjilo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ericah Yegela amesema ujenzi wa shule hiyo unaoghalimu zaidi ya billioni moja unakwenda kusaidia wanafunzi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata elimu.
Madame upo? Long time no see mpaka nikajua umetuachia rinchi letu hili la kishamba.Mpaka lini?