Kwanza kabisa naomba ufahamu kuwa mimi nimeandika hivi sio kwa lengo la kupinga makatazo yako kuhusu magari mengine (mbali na mabasi ya mwendo kasi) kutumia barabara za BRT. Sifurahii barabara hizo tulizojengwa kwa jasho la kodi zetu zije ziharibiwa kwa muda mfupi tu kabla ya lengo la ujenzi wake kukamilika, hivyo kukataza ni sahihi kabisa.
Lakini mimi nimeandika kuhusu zile lawama ulizozielekeza kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, mhe Chalamila.
Ni wazi kwamba wewe sio mfuatiliaji wa mambo, na maamuzi yanayotolewa kila siku na viongozi wengine nchini. Ndio maana umekurupuka kumshambulia na kwa namna fulan "kumdhalilisha hivi" mkuu wa mkoa huu wa Dar es salaam.
Nasema hivyo kwa sababu wote tuliona na wengine kusikia kauli ya aliekuwa waziri wa ujenzi kipindi kile mhe. Innocent Bashungwa akiagiza magari mbali mbali yaruhusiwe kupita katika barabara za BRT (haswa kilwa road) ili kupunguza msongamano wa foleni usiokuwa wa lazima hadi pale mabasi ya mwendokasi yatakapoletwa na kuanza kufanya kazi katika barabara hizo. Mkuu wa mkoa kama msimamizi wa serikali alichofanya na kuipokea amri hiyo kutoka kwa waziri husika na kuifanyia kazi. Sasa hapo kosa lake liko wapi mpaka kuanza kumpiga mkwara usiokuwa na maana.
Inamaana wakati Bashungwa anatoa amri hiyo wewe haukuwepo nchini?
Kama ulikuwepo kwanini umbebeshe Chalamila zigo la lawama huku muhusika ukiwa unamjua na kumuacha?
Au ulitaka Chalamila apingane hadharani na kauli ya Bashungwa ili ionekane anapingana na boss wake?
Tukija katika swala la malori kuharibu barabara hapo ndo unaonesha uzembe mkubwa mlio nao viongozi wa serikali. Hivi inawezekana vipi barabara iharibike mpaka ifikie hatua uliyosema, huku viongozi husika mkiwa nchini mnashuhudia uharibifu huo bila kuchukua hatua stahiki mapema?
Yani kiongozi unasubiri kitu kishaharibika ndo uje uchukue hatua ya kukataza kisitumiwe?
Sasa huko Rwanda mnaposema mnaendaga kujifunza, hua mnakwenda kujifunza nini? Maana ninachofahamu kule hakuna kiongozi anaeweza kufumbia macho uzembe unaofanyika au kufanywa katika wizara yake, na ndomaana unakuta kila kitu katika nchi ile kinafanyika kwa ufanisi mkubwa na utaalam wa hali ya juu. Tofauti na huku kwetu viongozi ni kula hela za miradi, kazi hazifanyiki kwa ubora unaotakiwa, uzembe umekithiri na bado kiongozi unajitokeza hadharani kumlaumu kiongozi fulani kupitia uzembe wa kiongozi mungine.
Week kama 3 zilizopita tumemuona mhe Abdallah Ulega akipiga mkwara wakandarasi wa mradi wa BRT kwamba wanachelewa kumaliza miradi kana kwamba yeye alikuwa nje ya nchi kwa kipindi chote cha ujenzi kiasi kwamba hakuwa anaona jinsi ujenzi huo unavyoendeshwa kwa mwendo wa kono kono.
Mtu unajiuliza kama uzembe huo unafanyika katikati ya mji mkubwa kama huu bila wahusika (wizara ya ujenzi) kuufuatilia mapema, je huko mikoani hali ikoje?
Nilichotaka kukwambia ni kwamba cheo ni dhamana ndugu yangu. Usione leo mkweo kakuweka katika nafasi uliyopo so unaweza kumfokea kila mtu, kuna siku unaweza kujikuta hao unaowafokea ndo wanakuwa mabosi wako, so watapoanza kukuhenyesha na wewe usianze kulalakamika. Ungekuwa mzalendo wa kweli ungeanza ku deal na hizo kampuni za ujenzi mlizoingia nazo mikataba ya kujenga barabara mapema sana.
Hizo barabara zote zinazojengwa zinajengwa chini ya kiwango, baada ya miaka 2 tu zitakuwa mashimo matupu. Viongozi mpo mnaona na hamfanyi kitu.
Kampuni hizo zilianza kujikongoja toka mwanzo wa ujenzi. Mimi nilikuwa mtu wa kwanza kuripoti na toa angalizo juu ya kile kinachofanyika hapa JF, lakini si wewe wala Bashingwa aliechukua hatua kuwasimamia wakandarasi. Sasa umefika muda wa uchaguzi ndo mnaanza kujifanya mnauchungu wa kuwasimamia wakandarasi na wengine kuwabebesha wakuu wa mikoa makosa yasiokuwa ya kwao.
Sisi wananchi sio wajinga. Tunajua na kufahamu kila kinachofanyika katika nchi hii. Kuanzia matendo yenu hadi maneno yenu. So piga kazi kaka acha siasa katika kila jambo.
Huo pichani ni uzi niliowahi kuuandika kitambo kidogo kuhusu kampuni hizo za ujenzi. Kama mngefuata ushauri wangu mapema, leo hii Ulega asingeongea yale aliyoongea siku ile.