Mchengerwa cheo ni dhamana kaka, jifunze kuheshimu kazi na maamuzi ya wengine

Waziri alikemea kuruhusu malori kutumia barabara ya mwendokasi na si magari yote.
 
Ktk hili waziri nadhani bashungwa na mkuu wa mkoa walikua sahihi kuruhusu barabara hizo zitumike kupunguza kero kubwa sana ya foleni iliyokuwepo hususani kilwa road.
Kweli kabisa mkuu.
 
Tatizo viongozi hupenda kuingiza siasa katika mambo ambayo hayahusiani kabisa na siasa kama haya mkuu.
 
Kwa hiyo MALORI yapite katika barabara za MWENDOKASI ?!!!

Sababu ya hayati JPM kuleta SGR ni kupunguza uharibu wa miundombinu ya barabara...

Leo hii turuhusu malori mazito yapite katika BRT ?!!

Hebu kuwa "serious".....
Tatizo sio kupita au kutokupita. Tatizo ni je alieruhusu magari kupita katika barabara za BRT yeye hamjui? Na kama anamjua kwanini asimwambie huyo mhusika badala ya kumbebesha lawama mungine?

Na kingine kwanini hakukemea swala hilo toka mwanzo na badala yake anasubiri barabara imeshaharibika ndo anatoa katazo? Siku zote alikuwa wapi? Au kwa vile uchaguzi mkuu unakaribia?
 
Ndio maana nikasema kwamba viongozi wetu wengi sio wazalendo halafu eti wanajifanya kwenda Rwanda kujifunza. Barabara nyingi nchini zimejengwa chini ya ubora tena kwa kutumia muda mrefu kinyume na ule muda wa makubaliano kitu ambacho kwa serikali makini na yenye maono ya Rwanda hakiwezi kutokea.

Upuuzi wote wa kujenga barabara chini ya ubora wachina wanaufanya katika nchi yetu tu, ila kamwe upuuzi huo hauwezi kuusikia au kuuona ukifanyika Rwanda au hata hapo Kenya.

Na ndiomaana ukiangalia barabara za Rwanda, Kenya na Tanzania utaona tu kwa macho kuwa ni wapi ambapo wachina wamebambika bambika lami juu juu ili wakusanye chao wasepe.
 

Ah wapi unatetea ujinga unafki
Ukiona hivyo basi tambua wazi kuna mkanganyiko na muingiliano wa majukumu. Shida iko serikali kuu
 
Kweli kabisa
 
Wakumdharau huyo jamaa! Katumwa na Chalamila
Hebu futa ujinga wako. Mimi nimeandika kuwa nakubaliana na maamuzi ya kukaza malori yasipite katika barabara ya mwendokasi. Ila sasa kwani malori hayo yalianza kupita leo au jana? Kwanini hakuonya hilo swala la malori kupita katika barabara za mwendokasi mapema mpaka anasubiri uchaguzi ufike na barabara ziharibike ndo ajitokeze?

Kumekuwa na uzembe wa viongozi kuacha mambo yajiendee yenyewe, yakishaharibika ndo anakuja mtu na mikwara kujaribu kuwatishia wengine na wakati kama yeye mwenyewe angewahi kuchukua hatua mapema kuzuia madhara hilo jambo lisingeharibika. Angalia mfano barabara ya BRT phase 4. Ipo kati kati ya jiji na Bagamoyo road ambapo viongozi wa serikali wakiwemo wa wizara husika wanapita kila siku wakielekea majumbani kwao au ofisini.

Wanaona barabara hiyo inavyochelewa kujengwa haraka ikamalizika kwa wakati. Leo hii bado mwezi mmoja muda wa mkataba uishe ndo waziri anajifanya kuja kukagua na kudai eti ujenzi wenyewe ndio kwanza upo asilimia 23. Hivyo kawataka waongeze juhudi ili huo mwezi mmoja uliobaki wawe wameshamaliza.

Sasa kwa akili ya haraka haraka unaona huo muda uliobaki unaweza kumaliza barabara ambayo imebakisha asilimia 77 kuisha? Kama miaka takriban miwili imejengwa asilimia 23% huku serikali ikishindwa kuwasimamia wamalize kwa wakati je huo mwezi mmoja uliobaki utasaidia nini? Kwanini hawakuwasimamia tangu mwanzo ili kuwatia jamba jamba wamalize barabara zetu kwa wakati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…