MCHENGERWA NA TAMISEMI YAKO FUATILIENI CHATO KUNA UPIGAJI AJABU, HASA KWENYE CHAGUZI NA KAZI NYINGINE MAALUM

MCHENGERWA NA TAMISEMI YAKO FUATILIENI CHATO KUNA UPIGAJI AJABU, HASA KWENYE CHAGUZI NA KAZI NYINGINE MAALUM

Kasongo yeeyee

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2024
Posts
308
Reaction score
654
Mhe. Waziri Mchengerwa na wizara yako imulikeni Chato na chukueni hatua mapema. Mambo si mambo kule, hali si hali.

Nimepenyezewa taarifa kuwa watumishi wa zoezi la uchaguzi wanadhulumiwa malipo yao kuanzia siku ya kwanza ya uchaguzi hadi leo hii, na hadi sasa zoezi la ugawaji fomu kwa wagombea linasuasua, watumishi wanadai fedha zao.

=>Msimamizi wa uchaguzi na timu yake tangu mwanzo wanawaeleza watumishi kuwa watalipwa kuendana na mwongozo wa malipo wa uchaguzi lakini mwongozo huo unafichwa kama bangi, wanasikia stori tu. Wakifuatilia wanaambiwa mwongozo utatolewa kisha chenga zinaendelea.

=>Watendaji hawakupewa barua za uteuzi hadi jana baada ya presha za juzi za DAS na Mwenyekiti wa Halmashauri. Barua za tarehe 25/09 zilikuwa zimebanwa huko hadi jana tarehe 26/10!

=>Mkataba wa kazi haujatolewa, nadhani wanasikilizia tena upepo mpaka kinuke zaidi ndipo wawapatie.

=>Wakati katika halmashauri zingine watu wameshalipwa fedha zaidi ya shilingi milioni moja, Chato wamelipwa shilingi 590k pekee!

=>Wakati katika zoezi la uandikishaji halmashauri zingine zikilipa shilingi 500k kwa siku 10 (@50k), Chato walilipa 300k. Baada ya kutiwa presha na DAS na Mwenyekiti wa Halmashauri juzi ndipo jana wakawatafuta wale waandikishaji na kuwaongezea 110k, hivyo jumla ikawa 410k.

=>Semina hata iwe ya siku mbili/tatu inakuwa diluted na kufanyika kwa siku moja, na malipo yanafanyika ya siku moja.

=>Semina ya kwanza kabisa afisa uchaguzi alitangaza kuwa malipo ni 30k na ilifanyika kwa siku moja, lakini baada ya watumishi kusikia kutoka halmashauri zingine na kulalamika wakaongezewa 10k ikawa 40k, hata hivyo ilitakiwa kuwa 120k (siku 3).

=>Kuna malipo ya ufuatiliaji na uhamasishaji wa zoezi ambayo ni 1000k kwa watendaji wa vijiji na 1100k kwa watendaji wa kata halmashauri zingine zimeshalipa. Kwa Chato watendaji wa kata wamelipwa fedha zao hizo, lakini wale wa vijiji wakapigwa kimya hadi juzi DAS na mwenyekiti wa Halmashauri walipoingilia na kuwaahidi watendaji kuwa watalipwa fedha hizo. Hata hivyo bado timu ya uchaguzi ya wilaya imewakazia na kuwaambia kuwa hakuna fungu hilo waende wawadai hao waliowaahidi.

Kwa Chato dhuluma za namna hii ni za muda mrefu, na ni katika kila jambo linalohusu fedha. Pale watumishi hawalipwi fedha za kujikimu wanapoajiriwa, fedha za likizo na uhamisho hazilipwi, promotion zinafanyika kwa connection, maelekezo ya kikazi yanatolewa kwenye groups za Whatsapp hawataki kuwaita watumishi kwenye vikao kwa kihofia madudu yao, na uozo mwingine mwingi ajabu.

Halafu watumishi wakifuatilia na kuhoji haki zao huwa wanatishiwa kufukuzwa kazi au kutokupata promotion. Yote haya ni katika idara mama ya utawala na rasilimali watu. Idara nyingine zinakuwa vizuri kutegemea na msimamo wa mkuu wa idara husika.

Katika uchaguzi wa 2020, baada ya kumaliza zoezi na kukabidhi matokeo na vifaa wahusika karibia/zaidi ya 1000 walidhulumiwa 50k kila mmoja, na walipokwenda kulalamika kwa DC aliyekuwepo kipindi hicho aliwatimua na kuwatishia kuwasomba kwa malori na kuwasweka mahabusu.

Yaani kwa ufupi Chato ni kama vile hakuna serikali au ni kisiwa/nchi inayojitegemea, ipo tofauti sana na halmashauri zingine ndani ya mkoa na nchi kwa ujumla.

Hatua zichukuliwe, la sivyo mambo hayatokuwa sawa.
 
Huyo waziri ni mkaza mwana wa saa100.
Hakuna ufuatiliaji hapo, nawe ukizikuta chukua hakuna wa kukuuliza
 
unachosema ni kweli kabisaa. hata sehemu nyingine watu wamepiga hela kwa kuwahulumu waandikishaji. Hasa hilo la semina kuifanya kuwa siku moja badala ya siku mbili ni karbia halmashaur zote nchini ili wapige pesa. Hii nchi uozo ni mwingi mnoo. Mama yetu samia unahujumiwa na unaowaamini. Tuma kikosi kazi kichunguze kimya kimya juu ya upigaji. Halmashauri zimeoza
 
unachosema ni kweli kabisaa. hata sehemu nyingine watu wamepiga hela kwa kuwahulumu waandikishaji. Hasa hilo la semina kuifanya kuwa siku moja badala ya siku mbili ni karbia halmashaur zote nchini ili wapige pesa. Hii nchi uozo ni mwingi mnoo. Mama yetu samia unahujumiwa na unaowaamini. Tuma kikosi kazi kichunguze kimya kimya juu ya upigaji. Halmashauri zimeoza
Yaani halmashauri za nchi hii zina mambo ya ajabu, ila Chato imekuwa too much aisee! Halmashauri za mkoa wa Geita kama Nyang'wale na Geita mjini wanalipa vizuri, lakini chato ni maajabu. Yaani mwajiri mwenye kipato kikubwa anamnyonya kila mtumishi wake zaidi ya 70% ya malipo yake kwenye zoezi halafu anataka matokeo chanya kwenye kazi!

Huwa najiuliza Magufuli na umwamba wake wote ilikuwaje wizi wa ajabu unaendelea hapo sebuleni kwake kabisa na hajui, maana pale ni pabovu tangu zamani, ila panazidi kadri siku zinavyoenda.

Yaani stahiki ya mtumishi hata iwe milioni moja wanataka wapige yote 100%, au wakikuhurumia wapige 90%!

Nadhani kuna laana pale
 
Back
Top Bottom