Mchengerwa: Rais ameridhia kuipandisha hadhi Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji. Soko kubwa na Stendi kuanza kujengwa

Lakini vgawaji

Lakini si yote hiyo itahitaji watumishi wapya, vitendea kazi nk????.... Kilichokwepwa Chato ni gharama na Eneo jipya la utawala.... Vipi kwa Kibiti?
Ishu ni kwamba kupanda hadhi hakukwepeki muda ukifika. Suala la Rufiji au Kibiti kupanda hadhi ya ki-halmashauri ni sahihi kama vigezo wanavyoweka vimetimia. Ila ile ya Chato kuwa Mkoa ilikuwa na ukakasi kwa sababu ni kama ilikuwa ya kulazimisha sana.
 
Kwa
Yale Yale ya chato kujengwa hospitali ya rufaa ya Kanda yanajirudia rufiji
sababu Dhahabu yetu imevunwa nyingi matani kwa matani kila siku iendayo kwa Mungu nadhani sio mbaya watu wa maeneo yale wakapata hata kaHospitali ka rufaa ka kufutia machozi !

Au nasema uongo ndugu zanguni ????!! πŸ™„πŸ˜³
 
Mkuu ... Yote hii ni double standard... Mchengerwa anataka tu kulazimisha Sababu ni waziri anayehusika na mambo hayo na mkaazi wa Eneo hilo....

Na wenyewe hukohuko Rufiji wanavutana kwa iwe Ikwiriri au Utete.....

Bora hata Chalinze iwe Wilaya kuliko hiyo Rufiji kupambaniwa....
 
Juzi nilikuwa kisarawe aisee pale panasikitisha.

Ingawa ni moja wapo ya wilaya kongwe kabisa ila maendeleo ni duni mno.
Kisarawe ushirikina unawaponza ni karibu kabisa na Dar lakini hapaendelei .Kibaha imewapiga bao hata Chanika kieneo kimechipuka juzi tu kinawapiga bao .
 
Lakini vgawaji

Lakini si yote hiyo itahitaji watumishi wapya, vitendea kazi nk????.... Kilichokwepwa Chato ni gharama na Eneo jipya la utawala.... Vipi kwa Kibiti?
Halmashauri tayari ina watumishi, labda bajeti ya kuboresha miundombinu ndiyo itakayoongezeka, Pia lazima bajeti iongezeke. Kupandisha hadhi mji ni cheap kuliko kuanzisha eneo jipya kama mkoa
 
Ambao tokea uhuru hamjawahi pata maji ya bomba muendelee kusubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…