DOKEZO Mchengerwa! Usiishie kutoa maelekezo tu kagua barabara zinazojengwa na TARURA hapo Dar ujionee vituko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waziri Mchengerwa nimesikia maagizo yako kwa TARURA kuhusu ubora na viwango vya barabara wanazozijenga.

Ombi langu usiishie kutoa maagizo ingia site ujionee vituko mwenyewe.

Anzia na barabara za hapo Dar. Barabara zinajengwa kwa design za karne ya 18 kwenye karne ya 21. Kuna barabara mpya kabisa hapo Dar zimejengwa bila njia za watembea kwa miguu, bila njia za waendesha baiskeli mfano njia ya mbezi msakuzi.

Barabara zinajengwa bila kufungwa taa kuwezesha watu kutembea na kufanya shughuli mbalimbali hata usiku.

Kuna uhuni mkubwa sana unafanywa kwenye ujenzi wa barabara nchi hii. Tena sio kwa TARURA tu hadi TANROADS.

Kama Dodoma Mtumba waliweza kudesign barabara wakaweka njia za watembea kwa miguu, njia za kupita baiskeli na wakafunga taa swali ni je kwa nini hawafanyi sehemu zingine?

Mulikeni hili eneo na wananchi waone umuhimu wa kulipa kodi kwa ubora wa miradi inayojengwa.
Mkumbushe na kulipa madeni ya wakandarasi ya miradi ya barabara ya mwaka wa fedha uliopita 2023/24.
 
Ufuatiliaji ndio unao kosekana kwa sasa kwa baadhi ya watendaji.
Kama wizara ya ardhi kwa sasa imelala sio kama ilivyo kuwa chini ya Slaa,
Ningekuwa Waziri kuna Wizara na Taasisi ningeweza kuzifuta, kufukuza watumishi wote na kuziunda upya.

Wizara hizo ni
1. Wizara ya Ardhi- Kutokana na kufeli kupanga na kupima maeneo ya nchi hadi nchi yetu kuwa kituko cha ujenzi holela.

2. Wizara ya Ujenzi- Kutokana na ujenzi wa barabara nyingi chini ya kiwango na kwa design za kishamba.

3. TARURA

4. TANROADS
 
Mbona hayati magufuli alikuwa.mkali.kwenye ujenzi ulio.chini ya.kiwango. where.is.value.for money. Wachina.wanazidi kumeza uchumi wetu kwa.hela zetu za ujenzi.

Sasa hivi kuna rstaurant na. Hotel kwa.ajili.ya.wachina.tuu.jinsi.walivyo na.jeuri ya pesa walioipata kwa.sababu ya uzembe.wa.wasimamizi.wa tenda
 
Dar njia zinafata jinsi maendelezo yalivyofanywa, ukiamua kubomoa nyumba, hata hiyo fidia itakuwa ngumu, walau tuna pa kuanzia, tutaangalia hayo baadae
 
Hilo si mnaruhusu wenyewe😁
 
CHURA ndio anapenda mawaziri wa kuagiza kama YY. Na sio kwenda SITE.
Ww jiulize hii nchi kama iko na waziri wa ardhi? Na hili nendeni mkaliangalie na sio YY au waziri. Anamanisha sisi wananchi.kituko kiko magogoni pale NAMBA 1.
All the best!!
 
Waziri Mchengerwa nimesikia maagizo yako kwa TARURA kuhusu ubora na viwango vya barabara wanazozijenga.

Ombi langu usiishie kutoa maagizo ingia site ujionee vituko mwenyewe.

Anzia na barabara za hapo Dar. Barabara zinajengwa kwa design za karne ya 18 kwenye karne ya 21. Kuna barabara mpya kabisa hapo Dar zimejengwa bila njia za watembea kwa miguu, bila njia za waendesha baiskeli mfano njia ya mbezi msakuzi.

Barabara zinajengwa bila kufungwa taa kuwezesha watu kutembea na kufanya shughuli mbalimbali hata usiku.

Kuna uhuni mkubwa sana unafanywa kwenye ujenzi wa barabara nchi hii. Tena sio kwa TARURA tu hadi TANROADS.

Kama Dodoma Mtumba waliweza kudesign barabara wakaweka njia za watembea kwa miguu, njia za kupita baiskeli na wakafunga taa swali ni je kwa nini hawafanyi sehemu zingine?

Mulikeni hili eneo na wananchi waone umuhimu wa kulipa kodi kwa ubora wa miradi inayojengwa.
Kwa sasa taasis inayoongoza kwa ubabaishaji wa miradi yake nahisi ni TARURA. Walivyowajinga, wanababaisha wakati matokeo yake yanaonekana kwa macho tofauti na taasis nyingine.

Naamini hawa jamaa wamesoma vizuri tu lakini wizi wa kupunguza bajeti na kuwabana wakandarasi ndiyo unafanya matokeo yao yawe mabovu.
 
Dar njia zinafata jinsi maendelezo yalivyofanywa, ukiamua kubomoa nyumba, hata hiyo fidia itakuwa ngumu, walau tuna pa kuanzia, tutaangalia hayo baadae
Hizi ndo akili za hovyo kuwahi kutokea.

Nani kasema hawawezi kujenga kwa hivyo viwango? Kuna ufinyu gani wa maeneo katika barabara ya Mbagala- Posta? Gongo la Mboto- Posta hadi kufanya barabara za kawaida kuwekwa njia mbili?

Kuna ufinyu gani wa barabara Goba? Mbezi Msakuzi hadi kufanya wasiweke njia za watembea kwa miguu na baiskeli?

Huku kuendekeza ujinga kwenu ndo kunafanya hawa ma engineer kila siku kuwabunia miradi ya hovyo na kuwapiga kwa ufisadi
 
Umesema barabara za Tarura, uliza kwanza kama hizo wanajenga Tarura
 
Acha kuhamisha magoli. Kwani Barabara za mitaani zinasimamiwa na nani?

Miradi ya DMDP inasimamiwa na nani?

Kwenye uzi pia wamewekwa hadi TANROADS. Kwa hiyo hadi Waziri wa Ujenzi nae akaangalie Barabara zake zinavyojengwa kwa viwango duni huku pesa nyingi zikipigwa.

Nchi hii kuna wizi mkubwa sana unafanywa kupitia hii miradi ya ujenzi hasa barabara.

Na sio kwamba watu hawawezi ku design vizuri na kujenga vizuri. Mfano umewekwa barabara za Mtumba, Dodoma au hata Coco Beach pale Dar. Design ya kuweka njia za watembea kwa miguu na waendesha baiskeli zilizingatiwa vizuri. Sasa kwa nini wanashindwa kufanya hivyo kwenye maeneo mengine kama sio upigaji tu?
 
Wanufaika wa.miradi ya.kifisadi. ya.barabara. naona wamevamia thread. Hakuna excuse ni utapeli tuu
 
Back
Top Bottom