Mchepuko unakaribia kuvunja ndoa yangu

Mchepuko unakaribia kuvunja ndoa yangu

Uzuri ni kwamba wanandoa mmoja wapo akianza kuchepuka Basi ujue na mwingine huanza hapo wote wachepukaji unavyomdanganya mkeo na kwenda kwa mchepuko naye hukudanganya hivyo hivyo na kwenda kwa mchepuko wake hapo mko sawa wote ondoa hofu endelea na huo mchepuko wako
 
Sisi wana JF hatuwezi kukutoa huko maana wakati unaenda hujatuhusisha. Kama huwezi toka mwenyewe basi jinyonge wote wakose.

NB. Ingetuhusisha kabla labda Mshana na team yake wangefanya majambozi wakutowe kwa garama yeyote.

Rip in advance.
 
Mimi nakushauri umuache mke wako nenda kwa mchepuko halafu muandikie mchepuko kuwa ndo mmiliki wa mali zako zote .
Follow me for more relationship tips [emoji41][QUOTE="BILGERT, post: 37342556, member: 276248"
 
Mchepuko anakucontrol na unashindwa kumuacha, Kuna kitu hapo, Kama mkeo anakila kitu na anakuheshimu usitake akuchukie...fanya kila linalowezekana achana na hako kamchepuko.
 
Duh,hivi inawezekana kulogwa bila hata kunywa ama kula cha kwake mkuu?
Mkuuu, Sidhani Kama Kuna njia Moja ya kufanya hayo Mambo.

Ila pia inawezekana hajakuloga ila wewe umekolea kwakeumempenda zaidi ya mkeo.
 
Mwanaume ukishajijua huna akili basi usioe maana unakwenda tu kutesa binti wa watu na watoto wasio na hatia.

Ifikie hatua wanaume wenye akili tu ndio waoe.
 
Kama mjuavyo kwetu sisi wanaume hatuachi kuchepuka ikiwa ndo asili na hulka yetu.

Nadhani hata ukiachana na mchepuko huyo utatafuta mwingine. Maana ni asili yako..
Achana na huyo mchepuko tafuta mwingine Labda itasaidia kumpenda Tena mkeo na kuheshimu
 
Kosa umefanya wewe unamlaumu mchepuko. Yaaani wewe Sio unaevunja ndoa yako bali ni mchepuko[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sijasoma yote, nimeona huu ni utoto kabisa. Hivi unaanzaje kuruhusu mchepuko akutawale na hata hivyo kama unatafuta mchepuko wa malengo naye ujue utapoteza mke uliye naye. Mchepuko ni kugonga na kuamsha..! Sasa wewe unamruhusu mpaka anakupigia simu usiku na unamuaga kabisa na yeye Mkeo anakuruhusu ? Duuh! kama ni mke ulibahatika au na yeye anakamjaa kanamkaza na usihisi hajui anajua ila kakukatia tamaa.
 
WhatsApp Image 2020-11-19 at 9.16.59 PM.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Mh! naomba namba ya mkeo nimshauri Jambo.

Kama huwezi kujitoa Basi muache mkeo kabla hajachoka akakuacha yeye.

Huwa mnaoa ili iwaje?
 
Pole sana omba Mungu akutoe katika hilo gereza ndugu yangu
 
Siku ya mwisho ikifika shetani ataturuka sana yani ata ruka

meter 100 akae mbali atukane,maana kuna mambo watu tunafanya

tukidanganyana ni shetani ila tunamsingizia bure kaka wa watu,kaka shetani.
Huyu hajamsingizia shetani, kasema ni hulka ya wanaume kuwa na mchepuko na ni asili. Hiyo ni Imani Yake, Sasa sijui kaitoa wapi labda ndo huyo shetani
 
Wewe tatizo lako kubwa,ni kuwa umeshindwa kutofautisha uati ya uzuri na Utamu! Mke wako ni mzuri lakini siyo mtamu Kama mchepuko wako,ambao nao siyo mzuri Kama Mkeo lakini ni mtamu! Na ndiyo maana nyumbani huna hamu ya kupiga game Kama unavyopiga kwa Mchepuko! Tafakari kabla ya hatari.
 
Michepuko mna nini lakin? Wakuu ninaandika kwa masikitiko na majonzi makubwa saana. Nimeoa takribani miezi Tisa sasa. Kama mjuavyo kwetu sisi wanaume hatuachi kuchepuka ikiwa ndo asili na hulka yetu.

Namshukuru Mungu,nimebahatika kupata mwanamke mzuri,mwenye upendo na pia Ni mcha Mungu. Tatizo ni huyu mchepuko niliye naye,anani control mnooo.Yaan ananifanyia visa sijapata kuona.

Inafikia nyakati Mke wangu simjali Wala kumheshimu tena,najikuta nguvu zote nazielekeza kwa mchepuko. Na mbaya Zaid mchepuko ananipeleka vile anavyo jisikia,namfanyia Mambo mengi kuliko hata ninayo yafanya kwenye familia yangu,

Lakini naambulia matokeo hasi kutoka kwa huyo mchepuko. Mchepuko anaweza kunihitaj hata saa tano usiku,ntajikuta nmedanganya kwa wife ili tu niweze kutoka.

Kuna nyakati mchepuko atanifanyia vitimbi na vibweka kiasi kwamba napoteza kabisa mood ya kazi. Nkirudi nyumbani,mke wangu namdanganya then atanifariji na kunitia nguvu na maisha yanaendelea.

Imefikia hatua nataka niachane kabisa na mchepuko,nashindwa kabisa yaan.ntampotezea Leo lakini kesho ntamtafuta Tena Bila kujali madhila anayo nifanyia.

Nimechoshwa na hii Hali wakuu,natamani kujinasua katika hii Hali ninayo pitia. Nahitaji kujikita kwenye familia yangu. Kinacho niumiza zaidi naweza kukaa hata wiki sijapiga game nyumbani,ila nataka kupiga tu game na mchepuko.

Mke wangu anakuwa mnyonge mnoo. Najutia saana kuwa na mchepuko,najitahid kutafuta njia nzuri ya kutoka na hatimaye kuacha kabisa.

Ushauri wangu kwa vijana wenzangu ambao mmeoa. Kama unaweza please tulia na mke wako ili usipitie Hali ambayo naipitia.

Nb:Mke wangu Ni mzuri na ametimia kila idara kuliko hata mchepuko.

Cc Extrovert
Mkuu, mie nina mke zaidi ya miaka 20 lakini sina mchepuko. Hiyo fikra yako ya kutufanya wanaume tuna tabia ya kutafuta michepuko ONDOA.
 
Back
Top Bottom