Mchepuko wa mdogo wangu amenielewa

Shekhee mzito sana katika kufanya maamuzi..yani ungekua mngoni tunazungumza mengine sahizi.
 
Anataka familia imtambue
 
Hapo swali ni nyie kama ndugu mta deal vip na huyo mwanamke mjinga.

Maana mwanamke mjinga achelewi kufarakanisha ndugu

Na nachoona hapo sijuiiii
 
Wewe mpare...nyie wapare huwa hamlazi damu goma likijipinda.
Skia huyo Dada mimba yake ime kupenda, vyovyote atakavyo fanya ni hiyo mimba inampelekesha.
Usiombe game hapo utazingua ambiere
 
Anataka usaidie kurutibisha mtoto aliyeko tumboni,, maana damu ni moja ya kwako na mdogo wako
 
Huyu dogo ni ndugu kweli au dogo msio na uhusiano wowote. Kama ni dogo kwa maana mdogo wako, wewe hufai kabisa. Utawezaje kwenda kwa mdogo wako, unatengewa chakula na shemeji kwa heshima, huku unakuwa kuwadi wa kutumwa kwa mchepuko. Ungesema hutaki kuhusika kwa namna yoyote, ningekuelewa, lakini kutumika kuharibu ndoa ya mdogo wako ni dhambi kubwa. Wewe unajidai uliwahi kusuhulisha, je ikitokea shemeji yako akajuwa wewe ni kuwadi itakuwaje..angalia usijemwagiwa maji ya moto na reception yote kuharibiwa.
 

Kwa kuwa wewe ni kaka, hakikisha unalinda heshima yako mbele ya dogo.

Huyo mwanamke ataondoka mwisho wa siku endapo mdogo wako ataamua kumuacha ila undugu wenu ni wa damu.

Busara ni kupiga chini hilo wazo na kumuweka mbali na wewe. Pili, huyo siyo mwanamke mzuri kwa maendeleo na umoja wa familia.

Ugomvi wa kimapenzi ukianza huwezi kujua kitakachotokea, mmoja wenu huenda akafa na mwingine kuozea jela. Hapo familia yenu ndiyo itapata hasara.

Dogo alifanya vizuri kukutambulisha huku akijua mchepuko wake atakuwa salama mikononi kwako.

Acha tamaa za kijinga, linda heshima yako na ya familia yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…