Mchepuko wa mdogo wangu amenielewa

Mchepuko wa mdogo wangu amenielewa

Shekhee mzito sana katika kufanya maamuzi..yani ungekua mngoni tunazungumza mengine sahizi.
 
Hapo swali ni nyie kama ndugu mta deal vip na huyo mwanamke mjinga.

Maana mwanamke mjinga achelewi kufarakanisha ndugu

Na nachoona hapo sijuiiii
 
Wewe mpare...nyie wapare huwa hamlazi damu goma likijipinda.
Skia huyo Dada mimba yake ime kupenda, vyovyote atakavyo fanya ni hiyo mimba inampelekesha.
Usiombe game hapo utazingua ambiere
 
Anataka usaidie kurutibisha mtoto aliyeko tumboni,, maana damu ni moja ya kwako na mdogo wako
 
Mimi sijui dogo anafaidikaje na huyo mchepu na dogo NI MTU MZIMA kaomba nimsaidie kusolve Jambo nakataaje ikiwa Mimi nimemkuta na mke wake na mchepu wake sjui walianza VIPI naanzaje kumuambia waachane hivi wewe unaijua nguvu ya mapenzi wewe swala la kupigiwa Hoti sjui kutengewa ugari na shemeji kwangu halipo sina muda Huo Aisee. Swala la kuachana na mchepu si jukumu langu halinihusu Hata kidogo Ila kama Kuna mgogoro NI kusuluhisha na kulala mbele Kila MTU ana maisha Yake Pengine dogo anawamudu wote au ana mpango wa kuongeza mke sa mi naanzaje kumpangia kwa MFANO.
Huyu dogo ni ndugu kweli au dogo msio na uhusiano wowote. Kama ni dogo kwa maana mdogo wako, wewe hufai kabisa. Utawezaje kwenda kwa mdogo wako, unatengewa chakula na shemeji kwa heshima, huku unakuwa kuwadi wa kutumwa kwa mchepuko. Ungesema hutaki kuhusika kwa namna yoyote, ningekuelewa, lakini kutumika kuharibu ndoa ya mdogo wako ni dhambi kubwa. Wewe unajidai uliwahi kusuhulisha, je ikitokea shemeji yako akajuwa wewe ni kuwadi itakuwaje..angalia usijemwagiwa maji ya moto na reception yote kuharibiwa.
 
Wakuu hamjambo aisee.

Mmefanikiwa na kubarikiwa Sana na Mungu WA Mbinguni.

Moja Kwa moja naanza, nilihamia kikazi mkoa Fulani kanda ya ziwa huku bahati nzuri huku yupo bwana MDOGO amekuwepo huku miaka MINGI na familia yake SA siku moja tupo kwenye matembezi tukakutana na kadada Fulani hivi kana tako zito sana aisee dogo kanitambulisha huyu NI shemeji yako Ila mpango WA kando.

Basi tukasalimiana pale kisha tukasepa hata nikiwa nakutana Naye huyo MCHEPUKO WA DOGO ni salamu Tu na utani kidogo mi mbele ukizingatia mi si muongeaji sana ni WALA introvert.

SASA hivi karibuni huyo mchepu WA dogo amekuwa na tabia ya kutaka mi niwe naenda kumuona anapofanyia kazi hasa jioni yaani mpaka anamzingua dogo mbona bro wako simuoni mi nikajua dogo anatania si akanionyesha SMS huyo mchepu anamlaumu dogo mbona humwambii bro wako aje au Ndo hutaki nimuone [emoji848] nikastuka Sana kuona HIYO SMS Basi nikamwambia dogo taenda kumcheck.

LAKINI zamani haikuwa hivyo cha ajabu dogo ananiambia Yule mchepu anasema mi nikionana Naye tunaongea vema Sana tofauti na dogo yaani mchepu wa dogo unanielewa Sana tukiwa tunaongea.

Jana dogo ananiambia Yule ana mimba changa uwenda HIYO mimba imekuelewa sana [emoji848]

SASA WAKUU Kwa Hali Hii huyu mchepu ANATAKA Nini kwangu huyu [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Kwa kuwa wewe ni kaka, hakikisha unalinda heshima yako mbele ya dogo.

Huyo mwanamke ataondoka mwisho wa siku endapo mdogo wako ataamua kumuacha ila undugu wenu ni wa damu.

Busara ni kupiga chini hilo wazo na kumuweka mbali na wewe. Pili, huyo siyo mwanamke mzuri kwa maendeleo na umoja wa familia.

Ugomvi wa kimapenzi ukianza huwezi kujua kitakachotokea, mmoja wenu huenda akafa na mwingine kuozea jela. Hapo familia yenu ndiyo itapata hasara.

Dogo alifanya vizuri kukutambulisha huku akijua mchepuko wake atakuwa salama mikononi kwako.

Acha tamaa za kijinga, linda heshima yako na ya familia yenu.
 
Back
Top Bottom