Mchezaji gani aliyefariki ulikuwa unamkubali sana?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Leo tuwakumbuke mafundi wa mpira ambao walikuwa wana uwezo mkubwa sana wakiwa dimbani enzi za uhai wao kabla ya kutangulia mbele ya haki.

Mimi naanza na huyu Said Nassoro Mwamba Kizota. Huyu jamaa mpira aliujua sana ila pia ubabe pia aliumudu mno. Toka anacheza mshambuliaji kisha baadae kurudi kucheza beki.

Enzi anacheza straika mabeki wengi walikuwa wanamuogopa, pia aliporudi kucheza beki, washambuliaji wengi wakawa wanamuogopa. Aliweza kucheza kwa kiwango cha juu sana kwa muda mrefu. Kama hujawahi kumuona enzi za uhai wake, anacheza kama anavyocheza Sergio Ramos.

Alijitengenezea sifa na umaarufu jinsi alivyomudu kumzuia mshambuliaji matata wa miaka hiyo, marehemu Majid Musisi wa Sports Club Villa kwenye klabu bingwa Afrika mashariki pale Kampla mwaka 1993 bila shaka.

Kwako wewe, ni mchezaji gani ulimkubali enzi ya uhai wake?
 
kwa wachezaji wa kitanzania hajawahi kutokea central forward kama Said Nassoro Mwamba 'Kizota' huyu alikuwa mnyamwezi wa tabora aliye jifunza mpira ukubwani!
baada ya kuwasambaratisha vilivyo wa ghaba pale 'shamba la bibi' kocha wa taifa wa Ghana alitoa machozi alipo ambiwa 'kizota' anacheza ligi ya Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…