Mchezaji gani aliyefariki ulikuwa unamkubali sana?

Leo tuwakumbuke mafundi wa mpira ambao walikuwa wana uwezo mkubwa sana wakiwa dimbani enzi za uhai wao kabla ya kutangulia mbele ya haki.

Mimi naanza na huyu Said Nassoro Mwamba Kizota. Huyu jamaa mpira aliujua sana ila pia ubabe pia aliumudu mno. Toka anacheza mshambuliaji kisha baadae kurudi kucheza beki.

Enzi anacheza straika mabeki wengi walikuwa wanamuogopa, pia aliporudi kucheza beki, washambuliaji wengi wakawa wanamuogopa. Aliweza kucheza kwa kiwango cha juu sana kwa muda mrefu. Kama hujawahi kumuona enzi za uhai wake, anacheza kama anavyocheza Sergio Ramos.

Alijitengenezea sifa na umaarufu jinsi alivyomudu kumzuia mshambuliaji matata wa miaka hiyo, marehemu Majid Musisi wa Sports Club Villa kwenye klabu bingwa Afrika mashariki pale Kampla mwaka 1993 bila shaka.

Kwako wewe, ni mchezaji gani ulimkubali enzi ya uhai wake?
Weka kumbukumbu sawa mwaka wa 1993 almarhumu said mwamba alikuwa bado ni mshambuliaji akisaidiwa na Eddy pamoja na mmachinga so asingeweza kumkaba musisi. Mwaka ambao mwamba alibadilika na kuwa kitasa ni mwaka wa 1998.Baada ya mechi nadhani ilikuwa na wanyarwanda au waganda mpaka half time tumekula thalatha (3)ndo akaona ujinga na kurudi mkoba mpaka tunanyanyua kwapa.
 
Leo tuwakumbuke mafundi wa mpira ambao walikuwa wana uwezo mkubwa sana wakiwa dimbani enzi za uhai wao kabla ya kutangulia mbele ya haki.

Mimi naanza na huyu Said Nassoro Mwamba Kizota. Huyu jamaa mpira aliujua sana ila pia ubabe pia aliumudu mno. Toka anacheza mshambuliaji kisha baadae kurudi kucheza beki.

Enzi anacheza straika mabeki wengi walikuwa wanamuogopa, pia aliporudi kucheza beki, washambuliaji wengi wakawa wanamuogopa. Aliweza kucheza kwa kiwango cha juu sana kwa muda mrefu. Kama hujawahi kumuona enzi za uhai wake, anacheza kama anavyocheza Sergio Ramos.

Alijitengenezea sifa na umaarufu jinsi alivyomudu kumzuia mshambuliaji matata wa miaka hiyo, marehemu Majid Musisi wa Sports Club Villa kwenye klabu bingwa Afrika mashariki pale Kampla mwaka 1993 bila shaka.

Kwako wewe, ni mchezaji gani ulimkubali enzi ya uhai wake?
Morrison...
 
Nani anamkumbuka Machepe?mtangazaji wa radio Tz alisema haya pale alipofunga Simba against Yanga"Machepe anaichepea Yanga" ... alikuwa na umri mdogo , kipaji kikubwa lakini ndio hivyo mchezaji huyo aliyekuwa kipenzi Simba akapotea na kufariki mapema.
 
Back
Top Bottom