Mchezaji Gerald Mdamu inadaiwa kutelekezwa na Polisi Tanzania baada ya kupata ajali; Ni aibu Tafadhali IGP ingilia kati

Mchezaji Gerald Mdamu inadaiwa kutelekezwa na Polisi Tanzania baada ya kupata ajali; Ni aibu Tafadhali IGP ingilia kati

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Yule mchezaji alievunjika miguu na jeshi la Polisi kumtelekeza

Akiongea na Hili Game ya Clouds FM Dada wa Mgonjwa aitwaye Rabeka Mdamu amesema kuwa Jeshi la Polisi halijasaidia chochote kwenye matibabu ya mchezaji huyo wa timu ya polis Tanzania aliyeumia akiwa kazini. Aliongeza kuwa familia imekosa hela ya kugharamikia vipimo zaidi.

Alivyotafutwa mwenyekiti wa timu hiyo ndungu Robert Munisi amedai kuwa Rabeka hana haki ya kuulizia hilo kwa kuwa Gerald and mke na Baba yake na kwamba Polisi walimsafirisha toka KCMC hadi MOI na kwamba huyo Rabeka hana hela yeyote ya kushughulikia chochote.

Ameongeza kuwa Polisi hawawezi kumkimbia mtendaji wao aliepigania nembo yao.

Nafikiri tu:

Hivi hili jeshi ndio lililo msafirisha mbowe kwa gharama kubwa?
 
Na kusimamia mbio za Mwenge
heee bibie upoo???? mbona kimya hivyo mara ya mwisho ulisema uko central unasaini makaratasi ya kumtoa mwamba vipi hukufanikiwa? yaani ukiwa chadema na akili huwaga zinawaruka kabisa pole lakini msalimie kamanda ukienda kumuona
 
Hapo kuanzia TFF, Timu pamoja na wadhamini ingekua wanajitambua tungesikia kitu kwa umoja wao maana jamaa alichokua anakitegemea ndio kimekua hivyo sema kwa kuwa wote ni wabinafsi hawawezi kufanya lolote kwa huyo mchezaji labda kelele zipigwe nyingi mno...matibabu tuu hivyo je malipo mengine si mtamsumbua sana au kutomlipa kabisa...
 
Mke kasema wameambiwa watarudishiwa gharama watakazotumia...hivyo hajatelekezwa.

Sema tu huo mlolongo wa pesa za Serikali mpaka kutoka Mgonjwa anaweza kukosa mambo muhimu ni bora wadau wa michezo wakajichangisha mdogomdogo.

Nilibahatika kusikia Maelezo ya Msemaji Wa Polisi na ya Mke.

Msemaji amesema kuwa hawamtambui Dada mtu kwenye mchakato wowote Wa matibabu ya Gerald na kwamba wanamtambua Mkewe ambaye walipewa maelekezo na Mgonjwa kuwa ndiye Wa kuwasiliana naye Kwa mambo yoyote yale. Msemaji anasema wao PT ndiyo waliomsafirisha Mgonjwa kutoka KCMC kuja MOI na wao ndiyo wanalipia gharama zote mpaka sasa.

Mke akakiri kumtambua Dada na mchango wake kwenye harakati za matibabu ya Mgonjwa. Kisha akaenda mbali zaidi kuwa Gharama zote za kumsafirisha Mgonjwa kutoka KCMC kwenda MOI, pamoja na matibabu zimelipiwa na Kaka Wa Mgonjwa. Mwajiri ambaye ni PT hajatoa mchango wowote zaidi ya kumpigia tu simu na kuulizia hali ya Mgonjwa. Ahadi iliyopo ni wapewe risiti zote za matibabu kisha watarejesha pesa iliyotumika.

Kwa maelezo ya huyu Msemaji wa PT na ya Mke Wa Mgonjwa nimepata picha kuwa PT ni maongo makubwa, ila ndiyo tabia yao kubambikia na kusema uongo tu, Manyang'au wakubwa..

Bora wadau wa michezo tumsaidie Gerald ila siyo kuwategemea hawa Mumiani..
 
Mke kasema wameambiwa watarudishiwa gharama watakazotumia...hivyo hajatelekezwa.

Sema tu huo mlolongo wa pesa za Serikali mpaka kutoka Mgonjwa anaweza kukosa mambo muhimu ni bora wadau wa michezo wakajichangisha mdogomdogo.
Unalikopesha jrshi la polisi?🤣😅😂
 
Ndiyo maana akina Kaheza wamekataa mishahara yao ya kuungaunga wakati ni Taasisi kubwa ya Serikali, wanawakamua tu wachezaji bila hata kuwakatia BIMA...
 
Yule mchezaji alievunjika miguu na jeshi la Polisi kumtelekeza

Akiongea na Hili Game ya Clouds FM Dada wa Mgonjwa aitwaye Rabeka Mdamu amesema kuwa Jeshi la Polisi halijasaidia chochote kwenye matibabu ya mchezaji huyo wa timu ya polis Tanzania aliyeumia akiwa kazini. Aliongeza kuwa familia imekosa hela ya kugharamikia vipimo zaid...
JESHI hili hili la kumvisha Mo kanga? ha ha ha ha haaa.
 
Nilibahatika kusikia Maelezo ya Msemaji Wa Polisi na ya Mke.

Msemaji amesema kuwa hawamtambui Dada mtu kwenye mchakato wowote Wa matibabu ya Gerald na kwamba wanamtambua Mkewe ambaye walipewa maelekezo na Mgonjwa kuwa ndiye Wa kuwasiliana naye Kwa mambo yoyote yale. Msemaji anasema wao PT ndiyo waliomsafirisha Mgonjwa kutoka KCMC kuja MOI na wao ndiyo wanalipia gharama zote mpaka sasa....
Duh, we jamaa kama kweli umesikiliza sasa kwa nini unapotosha?.

Gharama za Ambulance zimetolewa na PT, na ni sh milioni moja na nusu...ila kuna gharama zinazoendelea pale MOI ambazo analazimika kuzilipa Kaka wa Gerald...na pesa waliyopokea kama ya chakula ni 45000.

Ni kweli nilivyomsikia Msemaji wa Polisi ni kama alipaniki baada ya kusikia Dada Mtu akiwalaumu. Kwa matazamo wangu huyo Bwana hakupaswa naye kuingia kwenye malumbano yasiyo na tija wakati kilichopo mezani ni Mgonjwa asaidike....Yeye angejikita kwenye nini kinaendelea Gerald asaidike.

Ila kwa hizi taasisi huenda wapo wenye nia njema ya kuona Gerald anasaidika sema ndio hivyo pesa mpaka kuidhinishwa huko huwa ni mtihani.
 
Nilibahatika kusikia Maelezo ya Msemaji Wa Polisi na ya Mke.

Msemaji amesema kuwa hawamtambui Dada mtu kwenye mchakato wowote Wa matibabu ya Gerald na kwamba wanamtambua Mkewe ambaye walipewa maelekezo na Mgonjwa kuwa ndiye Wa kuwasiliana naye Kwa mambo yoyote yale....
Katu usiwasikilize wala kuwaamini PT!
Hakuna taasisi iliyooza na inanuka uvundo kama PT linapokuja suala la PESA!

Naamini kabisa hao wahanga maneno wanayosema kuwa wameambiwa 'wawasilishe risit' kisha watafidiwa gharama! Kama PT wanashindwa kusafirisha maofisa wao kwenda mahali popote panapohusu majukumu yao ya kazi wanawaambia wakifika wapeleke risiti watashindwa vipi kutoa maelekezo hayo kwa raia?

Wape risit utakaa miaka mpaka hiyo hela utaisahau! Mtu ana matatizo, anahitaji hela sasa hivi, mnamwambia alete risit mtamfidia, come on mbw@ nyie, anajitibia kwa hela gani? Kazi kusingizia watu kesi za ugaidi na kupambana na upinzani! Alaaniwe yeyote anayezaidia na kushiriki ushetani wa ccm! (Mungu awabariki na kuwasimamia wale waliomo humo wenye hofu ya Mungu)
 

Mdamu anatia huruma, aomba msaada wa Watanzania​


mdamu pic


STRAIKA wa Polisi Tanzania, Mathias Mdamu aliyevunjika miguu yote katika ajali iliyotokea hivi karibuni timu yake ikitokea mazoezini mjini Moshi anatia huruma. Amewaambia Watanzania kwa uchungu mkubwa huku akilia; “Naombeni mnisaidie, hali yangu mbaya.” Mdamu alihamishiwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam akitokea KCMC -Moshi.

Akizungumza na Mwanaspoti kupitia simu ya kaka yake, Benedicto Mdamu(pichani kabla ya ajali) alitamka maneno mazito yaliyoambatana na kilio kisha alishindwa kuendelea kuzungumza. “Nawaomba Watanzania kwa upendo wao, huruma zao, wanione na mimi kama wanavyowaona wengine ili nisaidiwe nitibiwe, lakini kama kilio changu kitamfikia na mama yangu Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anikumbuke mtoto wake ili nitibiwe kwa uharaka,” alisema huku akilia kwa uchungu na kaka yake akimtuliza na kumwambia amtumaini Mungu.

Awali Polisi wenyewe kupitia kwa Robert Munisi alidai kushangazwa na malalamiko yanayoibuka kila kukicha huku akisisitiza kwamba walihusika kumhamisha mchezaji huyo kutoka Moshi kwenda Dar na wanawasiliana na Mkewe kila mara kutoa msaada kwavile aliumia akiwa kazini. Mdamu ambaye ana watoto wawili Bryson (6) na Julian ambaye ni mchanga hajui hatima yao endapo kama atakosa matibabu ya haraka.

Straika huyo yupo na ndugu zake wa karibu ambao wanaweka wazi kuhitaji msaada wa hali na mali kutoka kwa familia ya soka nchini, ili atibiwe haraka kabla mambo hayajaenda kombo.

Benedicto anayemuuguza Mhimbili, ameeleza wanavyopitia wakati mgumu, huku mdogo wake akionekana kukata tamaa na kutoelewa hatima yake.

Aliliambia Mwanaspoti kwamba gharama zinazotakiwa kila siku anajikuta wakati mwingine anashindwa kuzimudu na kufanya mdogo wake awe mtu wa kulia kila wakati, huku akijiona hana thamani tena mbele ya uso wa dunia.

“Nitoe wito kwa wachezaji, makocha na wadau wa soka mbalimbali atakayeguswa na chochote amsaidie mdogo wangu ili aweze kutibiwa kwa haraka kabla ya mambo kuendelea kuwa mabaya, maana muda unavyokwenda ndivyo anavyojisikia vibaya,” alisema.

“Bora niwe muwazi ili asaidiwe, najua kuna wachezaji ambao wataguswa na kama wanataka kuamini wanaweza wakaja kujionea wenyewe, sijui hata niseme nini hata kama kuna kiongozi atasikia kilio changu naomba atusaidie na Mungu atambariki.”

MKE ATOA NENO

Mkewe Mdamu aliyejitambulisha kwa jina la Julian Marekela licha ya kuongea kwa hofu na huzuni kubwa alizungumza machache na kuwaomba Watanzania wamsaidie mumewe apone.“Naomba msaada ili mume wangu atibiwe kwa haraka maana ana hali mbaya, sijui hata nifanye nini,” kisha akakata simu na kuendelea kulia kwa uchungu.

BARAZA AMSIKITIKIA

Kocha Francis Baraz ambaye aliwahi kumfundisha Mdamu timu ya Biashara United kabla hajahamia Polisi Tanzania, alisikitishwa na hali yake.

“Nimemfundisha nikiwa Biashara United, zilinishtusha sana taarifa zake, Mdamu alikuwa na ndoto kubwa sana katika soka, naamini ipo siku zitatimia,” alisema.

Kwa yeyote ambaye atapenda kumsaidia Mdamu awasiliane kwa simu ya kaka yake namba 0714 - 716843.
 
Back
Top Bottom