Mchezaji Gerald Mdamu inadaiwa kutelekezwa na Polisi Tanzania baada ya kupata ajali; Ni aibu Tafadhali IGP ingilia kati

Police wanaleta siasa kwenye afya za waajiri wake waache hizo wawe na huruma huyu binadamu.....
 
Kwamba mchezaji wa ligi kuu hana bima ya afya?
Kwamba hamjui akili ZA polisi ni hamnazo
 
Kutokana na maelezo ya Ndugu yake anayemuuguza Moi, inasikitisha - yawezekana kijana si kucheza mpira tu bali anaweza hata asitembee tena.

Watanzania tumsaidie kijana huyu hata ikibidi akatibiwe nje ya nchi haraka, tusiache ndoto yake ikapotea hivi hivi.
 
Kama polisi Tanzania inawatekelezaga askari wake linapokuja suala la pesa litaacha kumtelekeza huyo raia? Majitu yaliyokaa kwenye nafasi za juu za hilo jeshi ni mabinafsi, roho mbaya, tamaa kama vile hayapokei mishahara, ukiyaona yalivyonenepeana utafikiri kitimoto
 
Kwanza nampa pole nyingi sana Mchezaji Gerald Mathias Mdamu kwa Kilichotokea na anachokipitia sasa. Naamini Mwenyezi Mungu atampigania, atamtia Nguvu na Kumfuta Machozi na Machungu yake.

Pili nadhani pamoja Jambo Kuu na la Msingi analolihitaji Mchezaji Gerald Mathias Mdamu kuwa hiyo Tiba ya haraka lakini anahitaji upesi sana Psychological Counseling kwani nilichogundua Kinachomtesa huyu Mchezaji ni Kuambiwa kuwa anatakiwa akatwe Miguu yote Mawili kutokana na jinsi alivyoumia vibaya mno.

Tatu natambua Juhudi za Nduguze na hasa Mkewe ( pamoja na Dada yake mkubwa Rebecca ) za Kumpambania Mpendwa wao Mchezaji Gerald Mathias Mdamu ila kuna Kitu si Kizuri nimekigundua baina ya hawa Ndugu zake na Ugonjwa wa Mchezaji husika.

Taarifa nilizonazo GENTAMYCINE ni kwamba Mchezaji husika Gerald Mathias Mdamu huenda kwa Kuwajua Ndugu zake walivyo aliomba Mawasiliano yake yoyote ( hasa yahusuyo Pesa ) yapitie kwa Mkewe tu na wala si hawa Ndugu zake wengine wanaohangaika Redioni, Runingani na katika Mitandao ya Kijamii.

Nne kwa mtazamo wangu ninachokiona sasa ni kama vile Ndugu wa Mchezaji Gerald Mathias Mdamu ni kama vile wanataka Kuutumia huu Ugonjwa wa Ndugu yao sehemu Kuu ya Kujipatia Kipato na hata Mtaji wa Biashara na sasa wameshamuingiza Mke wa Mchezaji katika Mtego wao na sasa wanampelekesha watakavyo na Kuwasikiliza wao.

Tano leo hii tukisema kuwa Jeshi la Polisi limemtelekeza Mchezaji wa Polisi Tanzania Gerald Mathias Mdamu na kwamba halijatoa ( halitoi ) Ushirikuano wowote ule Kwake tutakuwa tunajitafutia Laana mbaya kwa Mwenyezi Mungu na kuwa Wazushi na Waongo.

Taarifa za uhakika nilizonazo zinasema kwamba ni Jeshi la Polisi ndiyo limetoa AMBULANCE ya Kumsafirisha Mchezaji Gerald Mathias Mdamu kutoka Hospitali ya KCMC Kilimanjaro kuja Muhimbili ( MOI ) Dar es Salaam kwa Gharama za Tsh 1,400,00/= Kamili.

Mchezaji Gerald Mathias Mdamu bado ana Mkataba na Jeshi la Polisi na hata Mshahara wake anaupokea kama Kawaida. Baada ya Kufikishwa hapo Muhimbili ( MOI ) bado Gharama za Vipimo na Chakula kwa wanaomuangalia Jeshi la Polisi linawapa ja pia kuna Daktari wa Jeshi la Polisi yupo hapo MOI ( Muhimbili ) ili kusaidia Matibabu yake.

Je, kwa huu Uungwana wa Jeshi la Polisi uliomfanyia Mchezaji Gerald Mathias Mdamu nao ( Jeshi la Polisi ) hawastahili pongezi nyingi kutoka Kwetu na badala yake tunaonyesha Chuki zetu Kwao labda kwa sababu zetu tu za Itikadi ya Vyama na Matukio ya nyuma?

Je, hawa Ndugu kuanzia Mke wa Mchezaji Gerald Mathias Mdamu ( aishiye Dar es Salaam ) huyo Kaka na Dada yake wamemsaidia lipi la Gharama Ndugu yao huyo zaidi ya Kulia na Kulaumu tu?

Na GENTAMYCINE siko hapa labda Kuwatetea Jeshi la Polisi ila nataka kama Binadamu na Waungwana tuwe 'Fair' katika hili na sasa Kipaumbele chetu kiwe ni Kushikamana na Kuhamasishana huku na kule ili Mchezaji Gerald Mathias Mdamu apatiwe Tiba na ikiwezekana apone kabisa na siyo Kulumbana kwani haisaidii ( haitosaidia ) na tukumbuke Sisi tunalumbana tu ila Mchezaji Yeye anazidi Kuumia na Kuteseka hasa Kisaikolojia.

Na bahati nzuri Baba Mzazi wa Mchezaji Gerald Mathias Mdamu ni Askari Polisi Mstaafu hivyo taratibu zote za Kipolisi na Kiserikali hasa katika Suala la Tiba na Kuuguza anazijua na nasikia ndiyo anamhangaikia zaidi Mwanae akishirikiana na Waandamizi wa Polisi pamoja na Timu yake ya Polisi Tanzania.

Namwombea Mchezaji Gerald Mathias Mdamu kwa Mwenyezi Mungu apate Msaada na Ushirikuano mkubwa kisha apone na arejee katika Majukumu yake ( kama ikiwezekana ) ila tafadhali akipewa Ushauri wa Kitabibu wa Kukatwa Miguu yote miwili ( Kitu ambacho Yeye hataki na hapendi Kukusikia ) namwomba akubali tu kwani Ulemavu siyo Kufa.
 
Sijui government,sijui polisi,sijui jeshi,sijui CCM,sijui serikali,etc

Fvck you all,kafieni huko,jitegemeeni wenyewe....

Nimevunja keyboard kabisa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu angalia usiumie na wewe bado tunakuhitaji humu[emoji1787][emoji1787]
 
Hii taasisi imejaa utapeli sana,si kwa watumishi wake askari wala raia.

Ulikuwa uchaguzi mbaya sana kwa huyu jamaa kuamua kuitumikia.
 
Kuna watangazaji fulani viherehere wa vipindi vya michezo,naona kama washaanza pitisha mabakuli

Ova
 
Hayo majibu ya jeshi letu kwa raia ndg wa dada yanatosha kabisa kujua who's..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…