Mchezaji Sankara Karamoko aamua kuachana na Yanga na kwenda kucheza Ulaya

Mchezaji Sankara Karamoko aamua kuachana na Yanga na kwenda kucheza Ulaya

Wewe hujakutana na ubaguzi bado. Ni bora huyo Kingstone anabaguliwa na mashabiki. Sasa yeye Farid ndani ya timu kumejaa ubaguzi hapo unatokaje? Though kiukweli siwezi nikakupinga waliowengi hawana moyo wa kupambana
Tutabishana yote ila ukweli ndio huo we unafikiri msuva kucheza huko kwa warabu habaguliwi? Unakuta anabaguliwa sana tu ila anakaza roho sababu yupo kwenye utafutaji.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
wa west wale ni watu wengine kabisa.
Kule maisha ni magumu halafu hamna cha mjomba wala shangazi ndyo maana wakipata nafasi huwa hawaleti mchezo

Wakati bongo mambo yanaweza kuwa magumu ukienda kwa mjomba anakupokea na unakula fresh na pocket money unapewa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Japo nipo nje ya mada Mimi naamini kabisa viwango vya wachezaji wa africa magharibi vinafanana tu na sisi huku ila wenzetu wametuzidi connection tu ndio maana akicheza kidogo tu africa huyo unasikia tu yupo ulaya...fikiria mchezaji kama feisali,ibrahim baka,aishi manula,kibu denis,Dickson job,kapombe,mzamiru,kuna dogo mmoja akiitwa rashidi juma nk hawa ni wachezaji ambao wamekosa connection tu tangu wapo vijana ila laiti wangekuwa wamezaliwa africa magharibi japo sio wote niliowataja ila nadhani nusu yao wangekuwa ulaya
Nilikuwa naongea na mshua mmoja alifanya kazi Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zamani. Yeye Mtanzania.

Alisema kuwa, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wakenya na Waganda walikuwa wanapenda sana kutafuta fursa za kwenda ughaibuni, kusoma, kufanya kazi. Walikuwa wanapeana michongo sana.

Lakini, kwa upande wa Watanzania, ilionekana kama ukifanya mipango ya kwenda nje wewe ni msaliti.

Tumetoka huko miaka mingi, tumefungua nchi, ila bado kama walivyosema Waingereza "old habits die hard".

Zamani nilikuwa nafikiri ni tatizo la lugha, Watanzania wanaogopa kwenda nje kwa sababu hawajui lugha. Sasa huyo Ivorian anaenda Austria huko wanaongea Kijerumani. Hata yeye hakijui.
 
Ushawahi kukutana na issue ya ubaguzi? Katika wote hao atleast Farid Musa alikazakaza ila naye alikua anabaguliwa sana. Anakwambia mazoezi anafanya vizuri tu na anasifiwa ila kwenye mechi hapangwi.

Ofcourse hatuwei kataa hata wa mataifa mengine pua wanakutana na ubaguzi ila imagine katika group la watu 50+ wewe peke yako unazungumza kiswahili na Kiingereza hujui. Wachezaji wa west nao lugha inawabeba hasa English & French
Hamna cha ubaguzi wala nini. Ni kweli mchezaji kutoka ukanda huu anatakiwa kufanya extra effort ili kupata namba kwa sababu hatuna profile. Ingekuwa ubaguzi basi wachezaji weusi wote wasingekuwa wanapata namba.
 
Nilikuwa naongea na mshua mmoja alifanya kazi Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zamani. Yeye Mtanzania.

Alisema kuwa, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wakenya na Waganda walikuwa wanapenda sana kutafuta fursa za kwenda ughaibuni, kusoma, kufanya kazi. Walikuwa wanapeana michongo sana.

Lakini, kwa upande wa Watanzania, ilionekana kama ukifanya mipango ya kwenda nje wewe ni msaliti.

Tumetoka huko miaka mingi, tumefungua nchi, ila bado kama walivyosema Waingereza "old habits die hard".

Zamani nilikuwa nafikiri ni tatizo la lugha, Watanzania wanaogopa kwenda nje kwa sababu hawajui lugha. Sasa huyo Ivorian anaenda Austria huko wanaongea Kijerumani. Hata yeye hakijui.
Uthubutu
 
Back
Top Bottom