Mchezaji Sankara Karamoko aamua kuachana na Yanga na kwenda kucheza Ulaya

Wewe hujakutana na ubaguzi bado. Ni bora huyo Kingstone anabaguliwa na mashabiki. Sasa yeye Farid ndani ya timu kumejaa ubaguzi hapo unatokaje? Though kiukweli siwezi nikakupinga waliowengi hawana moyo wa kupambana
Tutabishana yote ila ukweli ndio huo we unafikiri msuva kucheza huko kwa warabu habaguliwi? Unakuta anabaguliwa sana tu ila anakaza roho sababu yupo kwenye utafutaji.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
wa west wale ni watu wengine kabisa.
Kule maisha ni magumu halafu hamna cha mjomba wala shangazi ndyo maana wakipata nafasi huwa hawaleti mchezo


Wakati bongo mambo yanaweza kuwa magumu ukienda kwa mjomba anakupokea na unakula fresh na pocket money unapewa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa naongea na mshua mmoja alifanya kazi Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zamani. Yeye Mtanzania.

Alisema kuwa, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wakenya na Waganda walikuwa wanapenda sana kutafuta fursa za kwenda ughaibuni, kusoma, kufanya kazi. Walikuwa wanapeana michongo sana.

Lakini, kwa upande wa Watanzania, ilionekana kama ukifanya mipango ya kwenda nje wewe ni msaliti.

Tumetoka huko miaka mingi, tumefungua nchi, ila bado kama walivyosema Waingereza "old habits die hard".

Zamani nilikuwa nafikiri ni tatizo la lugha, Watanzania wanaogopa kwenda nje kwa sababu hawajui lugha. Sasa huyo Ivorian anaenda Austria huko wanaongea Kijerumani. Hata yeye hakijui.
 
Hamna cha ubaguzi wala nini. Ni kweli mchezaji kutoka ukanda huu anatakiwa kufanya extra effort ili kupata namba kwa sababu hatuna profile. Ingekuwa ubaguzi basi wachezaji weusi wote wasingekuwa wanapata namba.
 
Uthubutu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…