Mzee wa old school
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 873
- 1,405
Dahhh! Afrika!! Kuna watu wajinga sana!!Mchezaji wa soka kutoka team ya Al Merreickh ya Sudan aitwae Ahmed Abdelsalam, hapo pichani chini, ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa mapumzikoni nyumbani kwake.
Mchezaji huyo amekutwa na umauti huo kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini humo, ambapo pia league imesimama na wachezaji kurejea makwao kwa mapumziko kupisha vita hiyo, huyu mchezaji nilimuona uwanjani pale kwa Mkapa wakicheza na Simba, wakati wa mashindano ya simba Super Cup
Ila jamani vita sio jambo zuri kabisa, na huwa wanaoumia, kuteseka, na hata kufa ni wale wasio na hatia, kijana mdogo aliyekua anapambania career yake, amezimika ghafla km mshumaa.
RIP handsome boy!!! [emoji24][emoji24][emoji24]View attachment 2660332
Wanao wapiganisha wamekaa wanawacheka tu... Ni ujinga sana