Mchezaji wa Chelsea aponda show ya Diamond

Mchezaji wa Chelsea aponda show ya Diamond

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,095
adam-na-diamond.jpg

Mtanzania ambaye kwa sasa ni raia wa Uingereza na anayechezea klabu ya Chelsea, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu.“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s embarrassing,” ametweet.

“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”

“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”



Kwa sasa Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.
 
Wasanii wa bongo kwenye international media na interview pamoja na show huwa wanaboronga sana na hawajui kuiteka mass.but there are few who are very competent.mfano AY
 
Huyu mtoto yupo academy ya Chelsea .. Ni mzanzibar
m zanzibar si mtanzania?yupo mwengine m znz anaitwa ismail feruzi na yeye anachezea chelsea.ni mchezaji mzuri ambae analipwa vizuri.
 
Namwelewa dogo,show za bongo fleva magumash tu.unaingia unapigiwa mziki kwenye cd kisha msanii anazuga na mic.ndo mana napenda band live.vyombo vyote vinapigwa wanamuziki unawaona na sebene likichanganya unazama kati mwenyeeewe
 
Kuna huyu jamaa heaven on desert tuko naye hapa JF kila kukicha haachi kumsifia Diamond naona atakuja na taarifa zaidi kuhusiana na hiyo shoo!
 
wapo wengine,wanachezea timu ndogo ndogo ni wachezaji wazuri tu,ila utaifa sio.wakifanikiwa watajulikana utaifa ambao sio wao
 
Hii show a Diamond UK mbona ipo kimya kimya mno this time?

Kuna picha moja tu iliyoonyesha "nyomi" kwenye show yake ya kwanza ndio inayozunguka mitandaoni. Hakuna picha nyingine zaidi ya zinazomuonyesha akila bata maeneo mbalimbali huko kwa malkia Elizabeth.
 
wapo wengine,wanachezea timu ndogo ndogo ni wachezaji wazuri tu,ila utaifa sio.wakifanikiwa watajulikana utaifa ambao sio wao

Kuna watanzania wengi wanacheza timu za watoto za epl, kuna mmoja namsikia anaitwa Clinton (alizaliwa 1998 ubalozi ulikpolipuliwa) naye anachezea timu ya watoto ya moja ya klabu ya epl
 
Back
Top Bottom