Mchezaji wa JKT aliyemfanyia Faulo mbaya Pacome afika hospital na kumfanyia dua

Mchezaji wa JKT aliyemfanyia Faulo mbaya Pacome afika hospital na kumfanyia dua

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ukisikia wema na uungwana kwenye mpira ni huu. Hongera kwa kuonyesha upendo kwake
=====
Mchezaji wa JKT Tanzania FC, Hassan Wahabi (Mwenye kanzu nyeusi), akiongoza dua, kumuombea Mchezaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, katika wodi ya Hospitali ya Agakhan, Dar Es salaam alipolazwa, kutokana na maumivu aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara,

HMJQeiNW8AALdP7.jpg
 
Dua haitasaidia. Amecheza hovyo sana. Pacome arastaafu mapema kwa lazima. Hata akipatiwa matibabu nje ya nchi bado naona hakuna timu kubwa kwa hapa bongo zitamzingatia sana mama kwanza ataingia woga wa kupamabana kwa nguvu ktk mechi. Aombee mkataba wake uwe wa muda mrefu hapo Yanga
 
Imenikumbusha mwaka 1982 au 1983 Ahmad Amasha wa Yanga alimvuja mguu Yusuph Ambwene wa CDA ya Dodoma na kusitisha career yake ya kucheza soka

Jioni ileile alienda kumjulia hali Muhimbili.

Ila wachezaji waangalie usalama wa wenzao wanapokua wanatimiza majuku yao uwanjani. Huu ni mchezo tu
 
Dua haitasaidia. Amecheza hovyo sana. Pacome arastaafu mapema kwa lazima. Hata akipatiwa matibabu nje ya nchi bado naona hakuna timu kubwa kwa hapa bongo zitamzingatia sana mama kwanza ataingia woga wa kupamabana kwa nguvu ktk mechi. Aombee mkataba wake uwe wa muda mrefu hapo Yanga
Pacome ndiyo mchezaji wa kwanza kuvunjika mguu?
 
Hapo ni viwango vya matibabu tu ndo Suluhisho. Kama wataona huduma bado wamtoe wampeleke kwenye matibabu ya juu, Bosi wao si yupo...Sema Jamaa hayuko sawa, kisaikolojia lazima ikuathiri, umeshapiga mahesabu yako kuwa Hapa misimu ijayo naondoka zangu naenda hatua za mbele zaidi then majanga
 
Huo uso wa Mayele unatosha kueleza kila kitu kabla ya kutupanga
 
Back
Top Bottom