Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
“Baada ya umeme kurudi, niliingia ndani kumtafuta mume wangu lakini sikumpata. Niliendelea na upekuzi kisha nikamuona akiwa amelala nje kwenye bustani. Nilipotoka nje kupeleleza kulikoni, nikagundua mume wangu alikuwa hatikisiki baada ya kuumwa na mbwa wetu watatu."
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo, Philemon Mulala ameuawa na mbwa wake nchini Afrika Kusini.
Msemaji wa polisi, Sam Tselanyane, alisema kuwa mke wake aliwaambia kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha na kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kibaya kwani mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea watembea kwa miguu na magari yaliyokuwa yakipita.
''Nilipiga ripoti kwa polisi na kuomba msaada wa kumpeleka hospitalini ,lakini walipofika walisema ameshafariki."
Mamlaka zimewaondoa mbwa hao wawili ambao ni 'Cross breed" ya Pitbul na mbwa wa tatu hajulikani asili yake ila anasemekana kuwa mkali.
Mulala alihamia Afrika Kusini kuichezea klabu ya Kaizer Chiefs mwaka wa 1988. Pia alichezea Cape Town Spurs na Lenasia Dynamos kabla ya kustaafu.
=====
Mamlaka zimesema Philemon Mulala alishambuliwa na Mbwa wake 3 wenye asili tofauti akiwa nyumbani kwake Lichtenburg, North West usiku baada ya Umeme kukatika.
Mke wa Mulala amesema alikuwa upande mwingine wa nyumba wakati wa tukio na alisikia Mbwa wakibweka lakini hakutilia shaka kwa kuwa mtaa huo una Mbwa wengi wanaobweka, baada ya muda alimtafuta Mume wake ndani na kumkosa hadi alimkuta nje ya nyumba akiwa amejeruhiwa vibaya na Mbwa hao.
Baada ya Polisi wa Uokoaji wa Dharura (EMRS) kufika, Mulala alithibitishwa kuwa amefariki katika eneo la tukio. Mulala amewahi kucheza katika klabu za Cape Town Spurs na Dynamos na timu ya taifa ya Zambia mwishoni mwa miaka ya 1980.
SOCCER 24