Mchezaji wa zamani wa Zambia auliwa na mbwa wake

Mchezaji wa zamani wa Zambia auliwa na mbwa wake

Mweusi mwezie, vipi rangi hapo ni tatizo?,siku ya kifo haina means ya kujiokoa, why why why marehemu hakupiga yowee la kuomba msaada?,kuna maswali mengi kuliko majibu
Haya huwa ni mashauri magumu sana: Kwa dar es salaam nimeshuhudia visa viwili vya namna hii, ila, si jambo la kiushangaza hasa pale ambapo mwenye mbwa hana knowledge ya kutosha ya tabia za mbwa
 

“Baada ya umeme kurudi, niliingia ndani kumtafuta mume wangu lakini sikumpata. Niliendelea na upekuzi kisha nikamuona akiwa amelala nje kwenye bustani. Nilipotoka nje kupeleleza kulikoni, nikagundua mume wangu alikuwa hatikisiki baada ya kuumwa na mbwa wetu watatu."

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo, Philemon Mulala ameuawa na mbwa wake nchini Afrika Kusini.

Msemaji wa polisi, Sam Tselanyane, alisema kuwa mke wake aliwaambia kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha na kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kibaya kwani mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea watembea kwa miguu na magari yaliyokuwa yakipita.

''Nilipiga ripoti kwa polisi na kuomba msaada wa kumpeleka hospitalini ,lakini walipofika walisema ameshafariki."

Mamlaka zimewaondoa mbwa hao wawili ambao ni 'Cross breed" ya Pitbul na mbwa wa tatu hajulikani asili yake ila anasemekana kuwa mkali.

Mulala alihamia Afrika Kusini kuichezea klabu ya Kaizer Chiefs mwaka wa 1988. Pia alichezea Cape Town Spurs na Lenasia Dynamos kabla ya kustaafu.

=====

Mamlaka zimesema Philemon Mulala alishambuliwa na Mbwa wake 3 wenye asili tofauti akiwa nyumbani kwake Lichtenburg, North West usiku baada ya Umeme kukatika.

Mke wa Mulala amesema alikuwa upande mwingine wa nyumba wakati wa tukio na alisikia Mbwa wakibweka lakini hakutilia shaka kwa kuwa mtaa huo una Mbwa wengi wanaobweka, baada ya muda alimtafuta Mume wake ndani na kumkosa hadi alimkuta nje ya nyumba akiwa amejeruhiwa vibaya na Mbwa hao.

Baada ya Polisi wa Uokoaji wa Dharura (EMRS) kufika, Mulala alithibitishwa kuwa amefariki katika eneo la tukio. Mulala amewahi kucheza katika klabu za Cape Town Spurs na Dynamos na timu ya taifa ya Zambia mwishoni mwa miaka ya 1980.

SOCCER 24
Hivi mbwa ana uwaje mtu labda hivyo ulivyo sema watatu ila mimi nikikutana na mbwa namuona kama mbuzi tu....majuzi kuna mbwa kajipendekeza kunishambulia alicho kutana nacho ...hadi mwenye mbwa akashangaa na kunishutumu eti kwanini sikimbii mm nikamjibu ulishawai kuona wapi mbwa anakimbiwa
 
alive. Ukute ana life insurance ya maana
Dawa ni kuachana na life insurance! Nakumbuka Kuna dada huko South alikuwa anawakatia life insurance baadhi ya ndugu zake kisha anawaua na Yeye kupata hayo mafao! Kule kuna shida.
 
Mbwa wa kisasa ni shida kweli!!yaani umeme ukikatika anashindwa kumtambua mfugaji?!!
nakumbuka miaka hiyo nipo village, ilikuwa naweza kumfungia mbwa wangu nikaenda hadi kijiji kingine, napita chochoro zote, nikiwa kule wakimfungulia tu, ananusa miguu nilipopita hadi ananikuta kijiji kingine. tukienda kuwinda unachofanya ni kumnusisha kwato moja tu aliyokanyaga nguruwe pori au digidigi/swala, atafuata alipokanyaga hadi anamkuta. sio hizi takataka za pitbull nini sijui.
 
Back
Top Bottom