Mchezaji yeyote duniani hutafuta vitu viwili tu, Kucheza na kushinda Makombe

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Jamani moja ya kitu ambacho wazungu wametupiga K.O nacho ni hili.

Wachambuzi wengi walimwingiza mkenge Fei kwa kigezo cha kusema eti Mpira ni ajira na kuna siku utafikia kikomo. Yes, tunakubali hatukai ila ukweli Mpira wowote duniani lazima Uucheze na lazima utwae makombe.

Kama hupati nafasi ya kucheza hapo ndio unaweza sema nataka niondoke hapa hata kama unatwaa makombe maana mpira wowote alzima uucheze usipoucheza hutopata watu wakukuona na kukusajili ambapo pengine wale ndio watakupa hela Nyingi uzitakazo.

Fei angekaa Yanga leo hii angekua anasakwa na team Nyingi za Nje sana ambazo naamini kabisa zingekua zinampa hela nyingi kuliko anayopata saivi pale Azam believe Me or not.

Saivi hafatiliwi maana Azam haina chochote na kwa mfumo wa soka la Afrika team hazifanyi scout zinafata mtu anaesemwa sana na team inayoongolewa sana ambayo now ni Yanga.

Fei washauri walimponza hata Ronaldo alikua maskini sana ila aliamini aucheze kwanza mpira sehemu atakayoonekana na atwae vikombe.

HARRY KANE NOW ANAHAHA ANAZIDIWA VIKOMBE HADI NA JOHN EVANS.

20240603_093932.jpg

Pia soma: Feisal alikimbia kupokea medali ya FA kwenye mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho la CRDB
Feitoto wakati unatunyamazisha Wana Dar Young Africans Kiukweli Ulifanikiwa, Ila Kiko Wapi?
 
Harry Kane ana gundu hata akienda City anaweza asitwae kombe
Msimu huu unaokuja Kane lazima anyanyue kwapa.

Kuna wachezaji kibao vijana kama Oscar wa Brazil akiwa Chelsea alikataa sifa akachagua fedha, pia wapo wachezaji vijana kama Ruben Neves, Malcom, Mitrovic et al walikataa kuendelea kucheza ulaya wakaamua kutimkia Uarabuni kula fedha za mafuta.

Makombe bila fedha hayana tija, kuna wachezaji kama Mbappe baada ya kupata fedha amezikataa fedha na kuamua kutafuta balo N'dor kwingine, ila tofauti na hapo nitajie wachezaji huko ulaya wengine waliokataa fedha na kuamua kufuata makombe?
 
Jaman moja ya kitu ambacho wazungu wametupoga K.O nacho ni hili.

Wachambuzi wengi walimwingiza mkenge Fei kwa kigezo cha kusema eti Mpira ni Ajira na kuna siku utafikia kikomo.
Yes tunakubali hatukai ila ukweli Mpira wowote dunian lazima Uucheze na lazima utwae makombe...

Kama hupati nafasi ya kucheza hapo ndio unaweza sema nataka niondoke hapa hata kama unatwaa makpmbe maana mpira wowote alzima uucheze usipoucheza hutopata watu wakukuona na kukusajili ambapo pengine wale ndio watakupa hela Nyingi uzitakazo..

Fei angekaa Yanga Leo hii angekua anasakwa na Team Nyingi za Nje sana ambazo naamini kabisa zingekua zinampa hela nyingi kuliko anayopata saiv pale Azam Believe Me or Not.

Saiv hafatiliwi maana Azam haina chochote na kwa mfumo wa soka la Afrika Team hazifanyi scout zinafata mtu anaesemwa sana na Team inayoongolewa sana ambayo gor now ni Yanga.

Fei washauri walimponza hata Ronaldo alikua maskini sana ila aliamini aucheze kwanza mpira sehemu atakayoonekana na atwae vikombe.

HARRY KANE NOW ANAHAHA ANAZIDIWA VIKOMBE HADI NA JOHN EVANS.View attachment 3007238
Unajua Kane akiwa spurs alikuwa analipwa kidogo kuliko anacholipwa kwa sasa pale Bayern Munich?, vipi alikataa hela zipi hapo?
 
Mchezaji yeyote Duniani hua anatafta vitu viwili tu 1.Kucheza na 2.Makombe.
Acha uongo, umewahoji wachezaji wote?
Hebu twende kwa mifano michache. Sadio Mane amehama Bayern Munich iliyokuwa na ubingwa wa Bundesliga kwa misimu 11 mfululizo, akaenda Al Nassr isiyokuwa na taji kwa misimu 5 iliyopita. Analipwa ths 2B kwa wiki. Halafu eti ukomae na makombe wakati huna hela
 
Msimu huu unaokuja Kane lazima anyanyue kwapa.

Kuna wachezaji kibao vijana kama Oscar wa Brazil akiwa Chelsea alikataa sifa akachagua fedha, pia wapo wachezaji vijana kama Ruben Neves, Malcom, Mitrovic et al walikataa kuendelea kucheza ulaya wakaamua kutimkia Uarabuni kula fedha za mafuta.

Makombe bila fedha hayana tija, kuna wachezaji kama Mbappe baada ya kupata fedha amezikataa fedha na kuamua kutafuta balo N'dor kwingine, ila tofauti na hapo nitajie wachezaji huko ulaya wengine waliokataa fedha na kuamua kufuata makombe?
Pesa muhimu
 
  • Thanks
Reactions: K11
Acha uongo, umewahoji wachezaji wote?
Hebu twende kwa mifano michache. Sadio Mane amehama Bayern Munich iliyokuwa na ubingwa wa Bundesliga kwa misimu 11 mfululizo, akaenda Al Nassr isiyokuwa na taji kwa misimu 5 iliyopita. Analipwa ths 2B kwa wiki. Halafu eti ukomae na makombe wakati huna hela
Ametwaa makombe hadi hapo na ana umri gani?

Kuna kombe hajawahi twaa??
Labda worl cup tu

Hoja yako imekufa vibaya sana mchezaji huanza kutafta hela baada ya kukuza CV yake akiwa amejitwalia makombe na amejitangaza vya kutosha.
 
Unajua Kane akiwa spurs alikuwa analipwa kidogo kuliko anacholipwa kwa sasa pale Bayern Munich?, vipi alikataa hela zipi hapo?
Umeingia mlemle kumbe mpira sio pesa ndio maana alikua nacheza pale Spurs...ila na pia uelewe Kane hajafata pesa Munich anataka kombe...kajitangaza sana pale spurs so now unaona ameenda sehemu anataka kombe hio hela kapewa tu kwa sbabau ya ile CV yake ila yeye interest yake ni kombe.

Ni kile nilikua nasmea Fei angekaa Yanga angejitangaza sana na leo angepata Team ambayo ingempa makombe na pesa ingempa maana angekua anajulikana sana na angekua na profile kubwa.
 
Hoja yako imekufa vibaya sana mchezaji huanza kutafta hela baada ya kukuza CV yake akiwa amejitwalia makombe na amejitangaza vya kutosha.
So, unamshauri Mzize asiende Ulaya kwanza hadi akuze CV yake kwa kutwaa makombe mengi na kujitangaza, hata kama ofa imekuja?
 
Pesa kwanza . Makombe ni mali ya klabu. Mlitaka kumfanya kama Ngasa? Acheni chuki kwa wachezaji hayo ni maisha.

Kwahiyo mlitaka aendelee kuwa Yanga huku akilipwa ml3 ilimradi tu awafurahishe mashaki wa Yanga?
 
Msimu huu unaokuja Kane lazima anyanyue kwapa.

Kuna wachezaji kibao vijana kama Oscar wa Brazil akiwa Chelsea alikataa sifa akachagua fedha, pia wapo wachezaji vijana kama Ruben Neves, Malcom, Mitrovic et al walikataa kuendelea kucheza ulaya wakaamua kutimkia Uarabuni kula fedha za mafuta.

Makombe bila fedha hayana tija, kuna wachezaji kama Mbappe baada ya kupata fedha amezikataa fedha na kuamua kutafuta balo N'dor kwingine, ila tofauti na hapo nitajie wachezaji huko ulaya wengine waliokataa fedha na kuamua kufuata makombe?
Ila daily saiv unawasikia wanatak kurudi ulaya sio kweli.

Mane anataka kurudi Girona
Henderson katoka yupo Ajax saiv.
Kuna Carrasco alienda China akarud at the end sio?
 
So, unamshauri Mzize asiende Ulaya kwanza hadi akuze CV yake kwa kutwaa makombe mengi na kujitangaza, hata kama ofa imekuja?
Ulaya sio Chamazi..ndio kitu naaamanisha ...samahan ulisomea Shule gani primary?
 
Pesa kwanza . Makombe ni mali ya klabu. Mlitaka kumfanya kama Ngasa? Acheni chuki kwa wachezaji hayo ni maisha.

Kwahiyo mlitaka aendelee kuwa Yanga huku akilipwa ml3 ilimradi tu awafurahishe mashaki wa Yanga?
Kibongobongo..kama Makombe kwanza kwanini anaumia akikosa kombe?

Halaf kingine azam watakuja kumuuza maana hawawez kua na mchezaji yeye anapata anachota ila wao hawapati wanachotaka toka kwake unadhan Azam wao wanataka mchezaji wakuongelewa tu hawataki mataji?
 
Jamani moja ya kitu ambacho wazungu wametupiga K.O nacho ni hili.

Wachambuzi wengi walimwingiza mkenge Fei kwa kigezo cha kusema eti Mpira ni ajira na kuna siku utafikia kikomo. Yes, tunakubali hatukai ila ukweli Mpira wowote duniani lazima Uucheze na lazima utwae makombe.

Kama hupati nafasi ya kucheza hapo ndio unaweza sema nataka niondoke hapa hata kama unatwaa makombe maana mpira wowote alzima uucheze usipoucheza hutopata watu wakukuona na kukusajili ambapo pengine wale ndio watakupa hela Nyingi uzitakazo.

Fei angekaa Yanga leo hii angekua anasakwa na team Nyingi za Nje sana ambazo naamini kabisa zingekua zinampa hela nyingi kuliko anayopata saivi pale Azam believe Me or not.

Saivi hafatiliwi maana Azam haina chochote na kwa mfumo wa soka la Afrika team hazifanyi scout zinafata mtu anaesemwa sana na team inayoongolewa sana ambayo now ni Yanga.

Fei washauri walimponza hata Ronaldo alikua maskini sana ila aliamini aucheze kwanza mpira sehemu atakayoonekana na atwae vikombe.

HARRY KANE NOW ANAHAHA ANAZIDIWA VIKOMBE HADI NA JOHN EVANS.

View attachment 3007238
Inasikitisha sana mtu kuleta mada bila kufanya utafiti Kwa wahusika, ilipaswa tuambiwe wachezaji wangapi wamehojiwa na kusema wanahitaji kucheza,kupata makombe na hawafuati pesa. Wachezaji kutoka Amerika ya kusini na Afrika kwenye umasikini hawawezi Kutafuta kombe kabla ya pesa, wachezaji wanapenda timu kubwa Kwa kuwa wanapata pesa nyingi zikifuatiwa na makombe.
 
Mtoa mada kafanye kazi Jiji ya kusafisha mazingira utapata medali nyingi na sifa kibao,mshahara laki moja elfu arobaini mia tatu na tisa una mke na watoto wawili,
Kama zilivyo familia nyingi za kiafrika baba,mama,shangazi,dada wanakuangalia wewe!
Hebu acha kuikosea adabu pesa!
 
Inasikitisha sana mtu kuleta mada bila kufanya utafiti Kwa wahusika, ilipaswa tuambiwe wachezaji wangapi wamehojiwa na kusema wanahitaji kucheza,kupata makombe na hawafuati pesa. Wachezaji kutoka Amerika ya kusini na Afrika kwenye umasikini hawawezi Kutafuta kombe kabla ya pesa, wachezaji wanapenda timu kubwa Kwa kuwa wanapata pesa nyingi zikifuatiwa na makombe.
Umewahoji wangapi?
Au ndie fei toto?
 
Back
Top Bottom