Mchezo gani ulikuwa unaupenda utotoni

Mchezo gani ulikuwa unaupenda utotoni

Me nilikua napenda kutengeneza n'gombe wa udongo kutega kware kwenye mashamba ya ulezi na kuogelea. Kupiga kinguo nguo mara chache sana.
 
Mimi nilikuwa napenda sana kuchez soka yani hata kuanzia aaubuhi mpaka usiku nacheza tu kula sikumbuki na najua jioni nikirudi home maza lazima anasubiri na kiboko getini.

Ilikuwa kila mwezi week lazima malapa ninunuliwe mapya kutokana na kukatika mpirani. Viatu vya shule havimalizi mwezi.

Asee baada ya kuanza sekondari maisha yakachukua taswira mpya na ndoto zangu za kuja kuwa Tanzanian Gaucho zikafia viwanja vya shule na chuo tu.

Nilipata mademu wakali lakini kwa vyenga vyangu na tobo darizi.
 
Mnatengeneza duara halafu mnaimba: -

"Kidea, kidea, kide kide kide kide kide kide, i love nakupenda...."

kisha unaenda kumchagua unayempenda...

Mitaa ya ubungo maziwa miaka ya 90..[emoji3]
 
Mnatengeneza duara halafu mnaimba: -

"Kidea, kidea, kide kide kide kide kide kide, i love nakupenda...."

kisha unaenda kumchagua unayempenda...

Mitaa ya ubungo maziwa miaka ya 90..[emoji3]
Hahahaha!!!
 
Umenifanya nikumbuke miaka 26iliyopita.kigogo darajani,tulikua tunaenda kuogera.sito sahau nilipo pata gonjwa LA KICHOCHO.
 
Umenifanya nikumbuke miaka 26iliyopita.kigogo darajani,tulikua tunaenda kuogera.sito sahau nilipo pata gonjwa LA KICHOCHO.
Hahahaha!!! Chumanile: ulikikanyaga tu we hukukiona hicho kichocho?
 
Back
Top Bottom