Mchezo gani wa utoto ulikuwa unaupenda sana?

Me nilikuwa nikipenda Sana kuogelea yani nilikuwa nitoka Asubuhi hata lunch nasahau narudi jioni


Sasa hapo jioni naporudi ndo napokutana na matokeo ya nilichofanya


Mpaka nikawa nafungiwa geti hamna kutoka
 
Me nilikuwa nikipenda Sana kuogelea yani nilikuwa nitoka Asubuhi hata lunch nasahau narudi jioni


Sasa hapo jioni naporudi ndo napokutana na matokeo ya nilichofanya


Mpaka nikawa nafungiwa geti hamna kutoka
Daaah. umenikumbusha kuogolea mixer boys and girls kuanzia asubuhi hadi jioni, ukitoka humo macho mekundu unaona ukungu tu, jumlisha na kidali poo cha kwenye maji na ule mchezo wa kitoto toto kwa wale wakubwa kidogo.
God bless Pwani.
 
😂😂😂mkuu paka na mbwa ulikuwa unawapeleka wapi 🤷
 
Mchezo ambao niliouopenda zaidi ni mpira wa visoda tulikuwa tunatumia magazeti kubandika vichwa vya wachezaji kwnye visoda au kutumia karatasi tuandika majina ya wachezaji basi kila mtu na timu yake tunakipiga ligi ya kitaa kumpata bingwa.
 
siku izi wapo bize wanachezea remote wanachek movie
[/QUOTE ]Kabisa mkuu,Siku hizi michezo mingi tuliyocheza zamani inapotea taratibu hata kombolela nayo imeanza kupotea enzi zile mid a ya jioni mtaani kelele za watoto Sikh hizi kimya.
 
Nilikuwa napenda sana mchezo wa kupanda kwenye miti. Ilifika kipindi nahama mti mmoja kwenda mti mwingine

Kunasiku wakati namalizia tawi nidake la mti mwingine niliporonyoka nikatulia shingo

Shingo ilipinda ikawa kama Spring marafiki zangu wote wakakimbia nikabaki nalia naeleka home huku shingo ipo kama namba 7

Wakati nakaribia nyumbani nikagundua kiwa nimejinyea, nikaanza kugopa kwenda, nikaingia kwenye kichaka nijifute kwanza, wakati nipo huko kichakani nikajifutia upupu matakoni


Mkund.u ulitoa Bawasili ya emegency nikawa nashindwa hata kutembea kilichonisaidia ni kupiga kelele na yowe kali kwa wakati mmoja nikaokolewa na wananchi

Nikapelekwa hosp. Wakati nimezirai kwa maumivu makali. Nilipofika huko wakakataa kunitibu wakataka PF.3

Kila mtu hakujua nini kimenikuta, wengine walisema nilitaka kunyongwa, mara nimelawitiwa na thougts kibao.

Polisi walikuja kunihoji nikasema ukweli, nikawataja na baadhi niliokuwa nao ndio wakasema kweli nimeanguka juu ya mti.

Hosp. Nilifungwa kiroba cha mchanga shingoni nikaning'inizwa kwenye wodi mpya inajengwa nikafungwa kama popo kichwa chini miguu juu

Wakamuita mtu wa tiba asili. Yeye akashauri akoke moto chini aweke dawa. Daaaah nusu nife kwa ule moshi wa yule mganga mseng.e

Shingo ikavimba balaa nikapigwa Xray nikaambiqa nimeteguka vibaya sana nikapewa rufaa hafi hosp. Ya mkoa morogoro nao wakaona hali tete wakaniambie niende muhimbili ndo nikaponea huko hadi leo shingo yangu inagoma kuzunguka nipo kama roboti

Daaah nashkuru nilipona nipo okey

Ndo mambo yakaisha ivyoo
 
kumbe ulikuwa mtalaamu wa kupiga chenga kweye futiboli au ukicheza golini?
Hiyo tunazungumzia enzi hizo..yap nilikuwa karibu na golini.nilikuwa nikicheza mpira wa miguu nafurahi mno...ingawa nilikuwa siujui vizuri😅😅😅
 
Need For Speed Most Wanted
Kuna game fulani hivi nimesahau jina lake liko unachagua ukaokoe watu kwenye train ama meli(nalitafuta hadi sasa ni zuri kinyama)
Na lingine la kuua maaskari nimesahau jina lake

troublemaker unakumbuka?
 
Need For Speed Most Wanted
Kuna game fulani hivi nimesahau jina lake liko unachagua ukaokoe watu kwenye train ama meli(nalitafuta hadi sasa ni zuri kinyama)
Na lingine la kuua maaskari nimesahau jina lake

troublemaker unakumbuka?
Mimi need4speed na mortal kombat peke yake ndiyo michezo niliyocheza na mpaka leo nacheza. Hiyo mingine sikuwahi.


Mdako na rede kulwa hukucheza?
 
Mimi need4speed na mortal kombat peke yake ndiyo michezo niliyocheza na mpaka leo nacheza. Hiyo mingine sikuwahi.


Mdako na rede kulwa hukucheza?
Mortal kombat sijawahi kuielewa

Hapana sijacheza mdako na rede
 
Karata na rede niliipenda sana.
Kula mbakishie baba, huu mchezo ulikua wa hatari ila niliupenda nao
 
Mortal kombat sijawahi kuielewa

Hapana sijacheza mdako na rede
tatizo la kukulia ushuani😀😀

Series za Mortal K ni Games nzuri sana hasa ukute mko wawili kila mtu na character wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…