Mchezo gani wa utoto ulikuwa unaupenda sana?

Mchezo gani wa utoto ulikuwa unaupenda sana?

tatizo la kukulia ushuani😀😀

Series za Mortal K ni Games nzuri sana hasa ukute mko wawili kila mtu na character wake.

Wala sijakulia ushuani,ni vile mimi na kaka zangu hatukuwa na interest na michezo ya nje sana....tumecheza sana pia tobo bao,unaijua?
 
Wala sijakulia ushuani,ni vile mimi na kaka zangu hatukuwa na interest na michezo ya nje sana....tumecheza sana pia tobo bao,unaijua?
Nimecheza sana😀 hiyo ukiguswa kidali unaenda kushika ukuta mwenzio akipita unakuwa umeokoka
 
Kula mbakishie baba na tobo dunda
tobo dunda hauna jina lingine huu mchezo?,

Nakumbuka sisi tulikuwa tunacheza gizani mtu mmoja anapanua miguu tunajificha alafu tunamtegea tunakimbia kwa kasi tunapita tobo bila kukutaja jina iwe tunapitia kwa nyuma au mbele yani ni timing na ukizembea anakutandika kibao cha mgongoni utagulia maumivu mbele ya safari
 
Karata na rede niliipenda sana.
Kula mbakishie baba, huu mchezo ulikua wa hatari ila niliupenda nao
Kula mbakishie baba wazembe walikuwa hawachezi maana watapigwa mpaka watakoma, kuna watu walikuwa wanakera ata ukijitaidi vipi lazima wakukute wakutembezee kichapo
Lakni wao hawapigiki yani ni hodari wa mbio na Kukwepa watu mpaka anafika sehemu yakugusa mti
 
mkuu naomba maelekezo wa mchezo wa kisikio poo!!
Uko hivi,mnaamua kuucheza mchezo huu pale mnapoagana ili pindi mtakapoonana atakayewahi kumwambia mwenzake KISIKIO POO! Basi atakuwa na haki ya kumpiga mwenzake sikioni kwa kidole cha shahada,hapo itaangaliwa ni siku gani,kama ni jumatatu atampiga mara 3,kama jumamosi mara moja,jumatano mara 5 n.k
Kwahiyo unatakiwa utembee kwa kujificha na kuwawahi wenzako lá sivyo wakikuwahi watakuwa wanakupiga mpaka sikio linawaka moto!
Nalog off
 
Du huu si Sijawai kucheza,na vipi ikiwa ijumaa,jumamosi na alhamisi?
 
Kuna mchezo tukiita RANGI MBILI

upo hivi mkiwa mnatembea mtaani au mnacheza ukimkuta mtu kavaa nguo zenye rangi mbili zinazofanana unawai kumwonyesha mwenzako kwa kumwambia mf. "shati nyeusi kiatu cheusi"
Mwenzako akithibitisha unakupa mashikamo haijalishi umri,
kwaiyo ni kuwa makini na rangi alafu unawai kumwambia mwezako unapewa mashikamo yako safiii kabisaaa alafu kuitikia sasa
"Marahabaaa mtoto mzuri ujambo? tunafurahia wenyewe tukisema tunajilipa mashikamo tukiyowapa wakubwa kila kukicha.
 
Kula mbakishie baba wazembe walikuwa hawachezi maana watapigwa mpaka watakoma, kuna watu walikuwa wanakera ata ukijitaidi vipi lazima wakukute wakutembezee kichapo
Lakni wao hawapigiki yani ni hodari wa mbio na Kukwepa watu mpaka anafika sehemu yakugusa mti
Huu mchezo wengi walikua wanaishia kulia
 
Huu mchezo wengi walikua wanaishia kulia
Michezo mingi ya utoto ilikuwa ni ya kupigana na kuoneana yani ubabe ubabe tu,
Nishawai kuchimbwa mkwara na mtoto mwenzangu iyo siku sikutoka kwetu nilitumwa nilikuwa muoga sana.
Nikikumbuka mikwala najua kabisa leo naenda kupigwa mtaani yani nitaamanika kwa wasichana nilikuwa mtu flani ivi makini sana,
nikimuona kwa mbali anakunja shati anajiandaa kuja kunipiga mi navua kandambili nashika mkononi mbio zake sasa mpaka home😂😂😂😂😂

NB,ilikuwa inatufunza kujiamini na kukabiliana na matatizo mbalimbali katika jamii.
 
tobo dunda hauna jina lingine huu mchezo?
Tulikua tunauita hivyo hivyo, yaani tunacheza mpira wa miguu bila kuweka magoli, tunapigana chenga ila ikitokea mtu akapigwa tobo basi anapigwa makofi hadi akashike mti ndio pona yake
 
Tulikua tunauita hivyo hivyo, yaani tunacheza mpira wa miguu bila kuweka magoli, tunapigana chenga ila ikitokea mtu akapigwa tobo basi anapigwa makofi hadi akashike mti ndio pona yake
Mmmmh kumbe, sisi ilikuwa tunagawana mfano tupo 6 basi ni timu 2 kwa idadi ya 3 kwa 3 alafu tunapiga pasi na chenga za kufa mtu uku tukipitishana tobo na tunaesabu izo tobo kwa timu husika hatukuwa tunapigana mokofi ila unadhalilishwa kwa kupitishwa tobo unaonekana mzembe,
Sisi tukiita KATA GOLI yani tunacheza bila goli huwa inatokea mpira wa wengi umeisha lakini mzuka wakucheza bado upo kwaiyo tunajikusanya wachache tunakiwasha upyaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom