Mtemi Eno
Member
- Jul 10, 2023
- 37
- 148
Kuna mchezo mpya siku hizi kina mama hasa wenye nyumba za kupanga huwa wanawafundisha mabinti kujenga ukaribu na wapangaji wa kiume ili kuingia vyumbani mwao kuangalia tv, kuomba kuwafanyia usafi, kuomba kuingiziwa nyimbo au muvi, n.k. (mbinu kibao) sambamba na kuwafunza mitego ya kuwazuzua kimapenzi. vijana walengwa huwa ni wale wa chini ya miaka 30, wengi bado hawajakomaa vizuri kiutu uzima.
Mabinti hawa wanaotumika kama chambo wengi huwa shule zishawashinda ama watoro waliotukuka, Binti anaweza kuwa na miaka 16 lakini ni mtundu si kidogo, upole wake ni script tu, ashafundishwa akwambie ana miaka 19 akutoe uwoga ila siku ya fumanizi watasema ana miaka 14 na umemlaghai aache kwenda shuleni.
Mpango mzima unakuwa hivi, Kama umekuwa na msimamo hutegeki kimapenzi basi hutumia mbinu zingine kuingia chumbani, mfano binti anakuja kuomba maji ya kumezea panado kichwa kinamuuma, akinywa maji anaomba apumzike nusu saa anaomba apumzike, hapo ndipo mama mwenye nyumba anastua matapeli wenzie wawili watatu waje, wengine wanaleta kabisa mtendaji wa mtaa ama polisi ambao washanogewa na pesa za huu mchezo mchafu.
Wakiingia ndani humo wanarekodi video kwa simu, hupewi hata nafasi ya kujieleza kila mtu anasema umelala na binti mwenye umri chini ya miaka 18, utajitetea kwamba mlikuwa mnacheki tv au alikuwa kapumzika anaumwa lakini haitasaidia, utajitetea alikwambia ana miaka 19 utaoneshwa cheti (hata cha mchongo) kazaliwa 2007 kiufupi hapa upo ndani ya 18 zao!.
Hapo kuchomoka hakuna kiwango maalum, watakukadiria kulingana na hali yako ya uchumi na ufundi wako wa maneno, ila wengi huwa wanachapwa laki 5 hadi 8. Hapo watamalizana kimya kimya, inakuwa siri na ndio maana ni ngumu kukuta habari hizi hadi uwe na ukaribu na wahanga.
kijana hawezi kubaki hio nyumba atahama tu hata kama kabakiza kodi ya miezi minne, muendelezo wa upigaji huu unaendelea kwa wapangaji wapya.
Kwa watu wasio na shida na hela bali kisasi ama kukomoana hutumia mbinu hii kuwatupia vijana jela, kwa wengine binti akiwa mzigo nyumbani hii ndio njia ya ndoa ya mkeka.