Al-mukheef
JF-Expert Member
- Feb 2, 2025
- 8,442
- 10,464
Haduri alijua kuwa Emmy alikuwa na hisia za kweli, ingawa aliona pia alikuwa na hofu fulani. Hata hivyo, alijivunia kuwa na mtu ambaye alikuwa tayari kumsaidia, na alijua kuwa mapenzi yao yalikuwa ya kipekee. Alijitahidi kuwa mkweli na mwenye adabu, akionyesha kuwa anastahili kuaminiwa. Walipokuwa wanazungumza, Haduri alijua kuwa Emmy alikuwa na mapenzi ya dhati, lakini alijua pia kwamba ilikuwa ni mapenzi ya ghafla, yenye kasi na nguvu kubwa za kipekee. Alikuwa na matumaini kwamba wangeweza kupambana pamoja, bila kujali ugumu wa maisha....na breki ya kwanza ilikuwa ni Magomeni kwa fundi ujenzi aitwaje Abdalla, huyu alikuwa ni rafiki wa kaka ake Emmy.
Abdalla alisema vibarua wamejaa ila nafasi itakapopatikana basi atapigiwa simu kujulishwa.
Wakaelekea mpaka mitaa ya Magomeni Kagera pale kuna ofisi ya kukatisha tiketi za mabasi na Emmy akamwambia Hedaru kuwa hii kazi haitakufaa....kumbe Emmy aliona wivu asije akanyang'anywa Haduri wake na abiria.
Basi walizunguka siku nzima, huku Emmy akimtia moyo Haduri kuwa kazi zipo ni kupambana tu.
Na ilipofika jioni walirudi nyumbani kuendelea na ratiba zao huku Emmy akimueleza kuwa kesho ni siku ya kuhudumu ndani ya basi, hivyo itabidi akamkodie gesti kwa maana kuonana siku moja tu si kigezo cha kumuamini kiasi cha kumuachia chumba chake abaki nacho.
Haduri alijiapiza kuwa yeye si mwizi wala kibaka kwanini hamuamini
"Wazazi wangu wamenilea vyema, na sikuwahi kuiba na wala sina hiyo tabia..., hiyo pesa ya kunilipia gesti siku mbili kwanini tusifanye ya kula? Huoni kama unachezea pesa?"
Haduri alimuuliza Emmy
"Sawa, nakuamini, ila itabidi kesho nikitoka nawe utoke ukatafute kazi, omba kazi kama mwanaume, usichague kazi...nakuombea kila la kheri ufanikiwe...nakupenda"
Emmy alimjibu Haduri huku akitabasamu na kumkumbatia.
Hakika penzi lao lilichipua ghafla mithili ya tawi jipya la mgomba.
Emmy, binti wa miaka 23 aliyechanganywa kimapenzi vilivyo na Haduri, kijana shababi wa miaka 30.
Hakika ungethubutu kuwaona kwa siku hiyo ungedhani labda penzi lao lina miaka 5 au 8...kumbe ndio kwanza wana siku 2 tu tangu waonane na kujuana.
Kweli mapenzi upofu....
....matembezi yake ya kutafuta kazi yalimpeleka mpaka kwenye ofisi moja inayoshughulika na mambo ya ulinzi, na kwa kuwa mwili wake ulikuwa umejaa jaa, waliamua kumpatia kazi ya ulinzi.Haduri alijua kuwa Emmy alikuwa na hisia za kweli, ingawa aliona pia alikuwa na hofu fulani. Hata hivyo, alijivunia kuwa na mtu ambaye alikuwa tayari kumsaidia, na alijua kuwa mapenzi yao yalikuwa ya kipekee. Alijitahidi kuwa mkweli na mwenye adabu, akionyesha kuwa anastahili kuaminiwa. Walipokuwa wanazungumza, Haduri alijua kuwa Emmy alikuwa na mapenzi ya dhati, lakini alijua pia kwamba ilikuwa ni mapenzi ya ghafla, yenye kasi na nguvu kubwa za kipekee. Alikuwa na matumaini kwamba wangeweza kupambana pamoja, bila kujali ugumu wa maisha.
Kesho yake, Haduri alijitahidi kutafuta kazi kwa juhudi, akiamini kuwa atafanikiwa. Hakuwa tayari kukata tamaa, alijua kuwa kila kitu kilikuwa kimefunguliwa kwa ajili yake. Emmy alimuahidi kumsaidia kwa njia yoyote ile, na yeye alijua kuwa penzi lao lilikuwa limechochewa na matumaini na safari ya pamoja. Walijua kuwa hali ya maisha ilikuwa ngumu, lakini walikuwa na matumaini kwamba kwa ushirikiano, wangeweza kufanikisha ndoto zao. Penzi lao lilibaki kuwa tamu, likiwa na uhakika wa maisha mapya ya pamoja.
....alipigania ndoto zake na za mpenzi wake Emmy zisije tenganishwa na chochote kile.Haduri alishtuka kwa mshangao na furaha, lakini moyoni pia alihisi uzito mpya wa majukumu. Alimshukuru Bwana Aesh kwa kumuamini, kisha akaondoka ofisini akiwa na hisia mchanganyiko. Alijua hili lilikuwa daraja kubwa la mafanikio, lakini pia alijua maisha yake yangekuwa karibu na mtu mwingine mpya, naam ni binti wa tajiri, ambaye hata hajamfahamu bado.
Baada ya masaa machache, alirudi katika ofisi za kampuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ajira mpya. Alipowasilisha vyeti vyake rasmi vya shule, katibu wa kampuni alimwangalia kwa mshangao kisha akasema, “Samahani, lakini hapa kwenye vyeti jina halisomeki Haduri... jina lako ni Tjedi, si ndiyo?”
Haduri alitabasamu kidogo, kisha akasema, “Ndiyo, hilo ndilo jina langu halisi. ‘Haduri’ ni jina la utani tulilozoea nyumbani tangu nikiwa mdogo. Lakini kwenye nyaraka zote muhimu, mimi ni Tjedi.”
Naam, kwa mara ya kwanza, alihisi uzito wa jina lake halisi. Lilikuwa jina la kweli, lililojaa historia na heshima ya ukoo wake. Na kwa kuwa sasa alikuwa anaingia katika hatua mpya ya maisha, aliamua kulikumbatia rasmi.
Usiku huo alimueleza Emmy kuhusu mabadiliko hayo kwa sauti ya matumaini, “Sasa rasmi, mimi ni Tjedi. Jina langu halisi linatambulika kikazi na kisheria...pia nimepandishwa daraja na kuwa mlinzi binafsi wa binti wa Bwana Aesh"
Emmy alikaa kimya kwa muda mfupi kabla ya kusema kwa sauti ya chini, "Sawa nakuamini, Tjedi… ila naomba usisahau tulikotoka."
Tjedi akajibu kwa upendo, "Sitasahau kamwe, Emmy. Hata dunia ikibadilika, moyo wangu unabaki kuwa wa kwako."
Wakiwa wamekaa sebuleni penye mwanga hafifu wa taa, Emmy alimwangalia Tjedi kwa muda mrefu bila kusema neno. Halafu kwa upole, alimsogelea na kuweka kichwa chake kifuani mwa Tjedi. Moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi. Mikono ya Tjedi ilimkumbatia Emmy kwa nguvu, akihisi joto la upendo wake likimjaa mwilini. Walinyamaza kwa muda, wakisikiliza sauti za nje na pumzi zao zikichanganyika kwa kasi. Giza la usiku liliwafunika taratibu walipoingia chumbani, ambapo walijiachilia kwa hisia kali. Usiku huo haukuwa wa tamaa bali wa kuthibitisha kwamba penzi lao lilikuwa hai na lenye mizizi ya kweli.
Siku ya kuwasili kwa binti wa Bwana Aesh ilipofika, Tjedi aliandaliwa vizuri akiwa amevalia suti nyeusi, miwani meusi na kipokea sauti cha sikioni. Gari la kifahari lilipofika, mlango ukafunguliwa taratibu na hapo ndipo Tjedi alipomuona kwa mara ya kwanza… binti huyo, Zara.
Alikuwa na tabasamu la kirafiki, lakini macho yake yalionekana yenye siri nzito, na hapo ndipo safari mpya ya Tjedi ilipoanza, safari ya kulinda si tu usalama wa Zara, bali pia uaminifu wake kwa Emmy na ndoto zao.
Asante sana kwa pongezi mkuu Etugrul Bey kwa kutambua kwanza uwepo wetu na pia kutambua tunachofanya.Kumbe watu wanapata shida ya bure ya kuandika riwaya wenyewe kumbe ni swala la korabo tu mzigo unakamilika
Big up sana Madame B binafsi naona una kipaji cha kuandika story,kama ulikuwa hujijui basi jua hilo,the same kwa Al-mukheef
Nimependa hamjaleta sana zile process za chumbani,maana hakuna haja ya details sana,jinsia mbili zikilala pamoja inajulikana nini kinafanyika
Well mpaka hapa tunapoendelea kusoma ni patamu sana
Kongole kwenu
Asante sana tupo pamoja,nikupe siri tu mwanzo nilitaka kuunga na mimi lkn nikaona hapana kama nyie wawili mmenoga sana hapo hahahaAsante sana kwa pongezi mkuu Etugrul Bey kwa kutambua kwanza uwepo wetu na pia kutambua tunachofanya.
Unajua yote yanawezekana mkiwa mnaenda kwa utaratibu na mtiririko endelevu.
Shukrani sana pia kwa kuendelea kutusoma mpaka wakati huu.
Karibu sana.
Shukrani🫡
Sawa mpwa, tumekuelewa.Na kwa kuongezea kama ushauri now imekuwa story flan serious sana,sio kamchezo tena,kwahiyo tulizeni vichwa mtupe mambo matamu
Na watao unga tafadhali kama huwezi kwenda na mtiririko ambao unavutia sasa,basi usitie neno tusome tu na kufaidi
Ni hayo tu!
Hapana,unaweza kuunga.Asante sana tupo pamoja,nikupe siri tu mwanzo nilitaka kuunga na mimi lkn nikaona hapana kama nyie wawili mmenoga sana hapo hahaha
Asante ila mlipofikia napendelea kusoma zaidi,ntabakia msomaji tuHapana,unaweza kuunga.
Kule mwanzo tulikuwa 4, na bado stori ilieleweka.
Ni kusoma tu na kisha kufanya muendelezo
Karibu sana
Yaani nami nimeshangaa kumbe watu wana vipawa vya kuandika namna hii...hongereni aisee!Kumbe watu wanapata shida ya bure ya kuandika riwaya wenyewe kumbe ni swala la korabo tu mzigo unakamilika
Big up sana Madame B binafsi naona una kipaji cha kuandika story,kama ulikuwa hujijui basi jua hilo,the same kwa Al-mukheef
Nimependa hamjaleta sana zile process za chumbani,maana hakuna haja ya details sana,jinsia mbili zikilala pamoja inajulikana nini kinafanyika
Well mpaka hapa tunapoendelea kusoma ni patamu sana
Kongole kwenu
Am sorry wewe sasa unataka kutukimbiza ndugu yanguHaduri alianza kuutalii mwili soft wa Emmy kwa mkono wake wa kulia huku mkono wake wa kushoto akitomasa chuchu sita za Emmy,Emmy aliwehuka kimahaba akihema kwa nguvu akambusu Haduri wakaendelea kubadilishana ndimi zao kwa muda kidogo….. Emmy kwa Sauti ya upole akamwambia Haduri ‘niko tayari mpenzi…’
Haduri akajivuta kidogo na kutoa mashine akaanza kuipeleka kwenye uke laini wa Emmy ……
Asante sana.Asante ila mlipofikia napendelea kusoma zaidi,ntabakia msomaji tu
Ila huyo mwamba Tjedi ameunga story vizur pia,ila kachomekea jina lake kiaina ndani ya story
Akitokea character mwingine jipendelee na wewe bhana
Jua kwamba mimi ni shabiki wenu katika huu uzi
Asante
Asante sana.Yaani nami nimeshangaa kumbe watu wana vipawa vya kuandika namna hii...hongereni aisee!
hujanikwaza mkuu ni FASIHIAm sorry wewe sasa unataka kutukimbiza ndugu yangu
Sio wote tunapenda hizo details,samahani lakini kama nimekukwaza
Hapana mkuu ila najichaji kwanza maana duh! kazi sio ndogoAsante sana.
Naona mkuu Al-mukheef kabanwa na majukumu kidogo
Zara alijua kuwa ilikuwa ni wakati wa kumfuata Tjedi na kumtangaza hisia zake. Alijua kuwa kama angechelewa, Emmy angemshinda kwa urahisi, lakini alijua pia kuwa Tjedi alikuwa mlinzi wake, sio tu kwa usalama bali pia kwa moyo wake. Usiku wa sikukuu ya Xmass, baada ya sherehe, alipomwambia, “Haduri, sina hakika kama kazi yako tu ndiyo inayokufanya unifuate,” alijua kuwa alikuwa ameanzisha vita isiyo na mshindi. Tjedi alijua kuwa hakutaka kuchagua kati ya mapenzi ya binti wa tajiri na mpenzi wake Emmy, lakini alijua pia kuwa kila hatua aliyoichukua ingeweza kumfanya kuwa sehemu ya hadithi isiyosahaulika....alipigania ndoto zake na za mpenzi wake Emmy zisije tenganishwa na chochote kile.
Zara, binti pekee wa Bw. Aesh, alikuwa ni mtoto na binti pekee wa bwana huyo tajiri.
Mke wa Bw. Aesh alifariki akiwa anajifungua Zara kule jijini London, Uingereza.
Na kabla ya kuzaliwa alimuahidi mkewe kuwa nae bega kwa bega katika malezi ya binti yao huyo, ila kumbe Mungu alipanga yake.
Mkewe hakuamka siku ile ya operation, alifia juu ya kitanda cha hospital huku akimuachia mumewe binti mzuri Zara, jina alilotoa mkewe endapo akijifungua salama.
Bw. Aesh alipanga kumlinda bintiye kwa gharama yoyote ile, iwe jua au mvua.
Alimpenda sana binti yake kuliko kitu chochote duniani.
Aliamua kumsomesha shule za gharama ili aje kuwa msomi na tajiri kama yeye baba yake.
Alimuasa kutojihusisha na mapenzi kwa namna yoyote ile, na aliapa kushughulika na yeyote yule atakayemuendea kinyume binti yake.
Mpaka anafikia umri wa miaka 25, Zara bado alikuwa bikra...ndiyo, alikuwa bikra kwani hakuwa na muda wa kulala na mwanaune yeyote yule, mawazo yake yalikuwa juu ya masomo na mafanikio.
Lakini sasa, ameshakuwa binti mkubwa, ameshamaliza chuo na sasa anarejea nyumbani Tanzania ili kuendesha na kuiendeleza miradi ya baba yake iliyopo Tanzania.
Baba yake alimnunulia nyumba kubwa na ya kifahari mitaa ya Mbweni, alimuwekea wafanyakazi wawili na mbwa mmoja.
Pia alimtafutia mlinzi binafsi ambae ndie Bw. Tjedi (Haduri)
Siku ya kwanza Tjedi kukutana na Zara, moyo wake ukakiri kuwa kakutana na mwanamke mzuri kuliko wote duniani,
Aliona kabisa penzi lake na Emmy lipo kwenye mtihani.
Zara, alipomuona Tjedi kwa mara ya kwanza alihisi kama kamuona mwanaume pekee aliyeandaliwa kwake.
Alivutiwa na umbo la mlinzi wake, pia sura yake ya u-serious nayo ilimmaliza kabisa Zara.
Zara kwa mara ya kwanza alihisi kuzama penzini na mlinzi wake Tjedi.
Ila kutokana na tabaka walilokuwa nalo, hakuruhusu hisia zile zionekane waziwazi mbele ya Tjedi.
Maisha mapya yalianza ya kumlinda binti wa tajiri, sio binti tu bali kulinda penzi lake na Emmy kwani aliona kabisa akifanya mzaha basi anaweza akamkosa Emmy mazima, jambo ambalo hakutaka litokee kabisa.
Kila alipoenda Zara, Tjedi alikuwa nyuma yake....iwe sinema, muziki, shopping, kwenye matembezi, kwenye hafla mbalimbali na hata Zara alipotaka kwenda kuonana na marafiki zake, Tjedi alimsindikiza.
Zara alimuamini mno mlinzi wake.
Na aliahidi kumuongezea mshahara kama asante kwa kumlinda vyema.
Ilipofika December, sikukuu ya Xmass, Zara aliandaa party pale nyumbani kwake na kualika marafiki wachache, Tjedi (Haduri) nae akaona si mbaya amualike kipenzi chake Emmy kwenye sherehe zile za boss wake Zara....
Bila kujua kuwa Zara ana ajenda ingine ya siri,....ndio, aliandaa party ile makusudi ili aweze kuwa karibu na Tjedi usiku ule........
Kwa mwendo wa kuchumpa, ilibidi Tjedi awakimbize Zara na Emmy haraka kwenye chumba cha siri kilichopo chini ya jengo lao maeneo ya jikoni, kwani ujio wa gari lile lenye vioo vyeusi ulionekana dhahiri si ujio mwema.....ingeweza kumfanya kuwa sehemu ya hadithi isiyosahaulika. Naam, usiku ulikuwa umetulia kwenye nyumba ya Zara. Wageni wengi walikuwa wameshaondoka, taa zilizokuwa zikimetameta awali sasa zilikuwa zimeanza kufifia taratibu, na sauti ya muziki ilikuwa ya chini kuashiria sherehe imefika tamati.
Emmy alifika akiwa amevalia gauni la rangi ya samawati lililomfanya kuonekana mrembo na kuvutia zaidi. Alitembea kwa hatua za utulivu kwenye bustani ya mbele ya nyumba, ambapo watu wachache walikuwa bado wakizungumza kwa sauti za chini. Tjedi alipomwona, moyo wake ulidunda. Alihisi kama mwili wake umeganda kwa sekunde moja, akamkaribia na kumkumbatia.
"Umekuwa mzuri sana leo," Tjedi alimwambia Emmy kwa sauti ya chini, uku mikono yake ikimshika kiuno.
Emmy alitabasamu kwa aibu, "Asante, nimekuja kukushuhudia unavyofanya kazi yako. Pia, nilitaka kumjua boss wako."
Kwa upande wake, Zara akiwa amevalia gauni jekundu lililong’aa kwa mwanga wa taa hafifu, alikuwa amesimama kwenye balcony ya ghorofani, mkononi akiwa na glasi ya Champaign aina ya Dom Perignon. Macho yake yalikuwa yameelekezwa kwa Tjedi na Emmy.
Kwa mara ya kwanza, Zara alihisi hasira ya wivu. "Kwa nini anampenda huyo mwanamke wa kawaida sana wakati mimi nipo hapa?" alijiuliza moyoni. Alikunywa kinywaji chake kwa haraka, kisha akashuka chini na kumfuata Tjedi.
“Tjedi, mgeni wako umemtambulisha? Mbona amependeza kama First Lady!” alitamka kwa tabasamu la bandia.
Tjedi akacheka, “Huyu ni First Lady wa moyo wangu.”
"Tjedi," Zara alimwita kwa sauti tamu lakini iliyobeba msisitizo. "Ningependa uje huku unisaidie kitu kidogo."
Tjedi alimtazama Emmy kwa macho ya kuomba ruhusa, kisha akamfuata Zara ndani ya nyumba.
"Unanifanyia nini?" Zara alimwuliza ghafla, sura yake ikibadilika. "Toka siku ya kwanza nimekuona moyo wangu ulivutiwa nawe, na sipo tayari kukupoteza kwa huyo mwanamke."
"Mimi ni mlinzi wako, Zara. Lakini Emmy ni mwanamke wa maisha yangu," Tjedi alisema kwa msisitizo.
"Sitaki kusikia jina lake!" Zara alimkatiza, kisha akamkaribia na kumkumbatia kwa nguvu. "Nataka uwe wangu."
Wakati huo huo, Emmy, aliyekuwa na wasiwasi juu ya kuchelewa kwa Tjedi, aliamua kumfuata. Alipofika mlangoni, aliona jinsi Zara alivyomkumbatia Thedi, moyo wake ulipasuka.
"Tjedi!" Emmy alipiga kelele, machozi yakimwagika. "Kweli umenidanganya? Hiki ndio 'kitu kidogo'?"
"Emmy, si-" Tjedi alijaribu kujitetea, lakini Emmy alishika njia na kuondoka kwa haraka. Zara akatabasamu kwa ushindi wa muda.
Ghafla, simu ya Tjedi ililia. Ni Bwana Aesh. "Tjedi, nimesikia habari mbaya. Kuna watu wanaomfuatilia mwanangu. Wanataka kumdhuru. Tafadhali kuwa makini, ongeza ulinzi!"
Sekunde chache baadaye, gari lenye vioo vyeusi lilifika na kusimama mbele ya geti. Watu waliovaa nguo nyeusi na sura kufunikwa walishuka wakiwa na bunduki mikononi.
....Zara, Tjedi na Emmy walizidi kusonga mbele gizani, huku wakisindikizwa na sauti za vyura waliokuwa wanashindana kukoroma ndani ya kibwawa kidogo kilichokuwa pembeni ya kinjia walichopita.Mambo yalizidi kuwa magumu mule ndani....Naam... hali ilikuwa ya taharuki. Katika kile chumba cha jikoni, Tjedi aliendelea kutega sikio, jicho lake likiwa limekodoa kwenye mlango mdogo wa kuingilia jikoni.
--London, Miaka 25 Nyuma---
Gari la Bwana Aesh lilikuwa likisafiri kwa kasi barabarani za jiji la London, likielekea hospitali. Bi. Nadira alikuwa katika maumivu makali ya kujifungua pia akiwa ameshikwa na wasiwasi.
"Tunafika hivi karibuni, mpenzi kuwa na imani" alimtuliza Bwana Aesh huku dereva wake akiendelea kusonga mbele kwa kasi ya ajabu
Ghafla watu wawili wakiwa kwenye pikipiki wakawapita kwa kasi na kuachia risasi tatu ambazo zilipenya kwenye kioo cha gari, moja kati ya hizo ikimgonga Bi. Nadira kifuani!
"NADIRA! HAPANA!" Bwana Aesh alipiga kelele kwa mshangao na huzuni. Damu ilimwagika kwa kasi ndani ya gari.
Dereva alizungusha usukani kupiga msele na kubadili mwelekeo na kuanza kukimbizaa gari kwa kasi zaidi kuelekea hospitali ya karibu.
"Endelea kuwa nami mpenzi! Usiniache" Bwana Aesh alimwambia mke wake huku akiwa ameziba jeraha la risasi kwa mkono wakati damu ikiendelea kuvuja kwa kasi
Walipofika hospitalini, wakunga walimchukua Bi. Nadira kwa haraka na kumpeleka kwenye chumba cha dharura.
"Mtoto anahitaji kutolewa sasa hivi, vinginevyo wote wawili watakufa!" daktari alisema kwa msisitizo.
Bwana Aesh alikuwa amesimama nje ya chumba hicho akiomba Mungu amwokoe mke wake na mtoto wake.
Baada ya Masaa kadhaa daktari alitoka huku uso wake ukionekana na huzuni.
"Samahani, Bwana Aesh... tumefanya kila tunachoweza, Bi. Nadira amepoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi. Lakini mtoto wako ni mzima, na ni msichana."
Bwana Aesh alimuangalia mtoto wake mchanga, akamwita 'Zara', jina alilopendekeza mke wake kabla hajafa.
Wote wanaliohusika na tukio hili watalipa!" alipaza sauti huku akikandamiza meno yake kwa hasira kali. Alijua kuwa ana maadui wengi wa biashara lakini hakujua ni nani alikuwa nyuma ya shambulizi illo na alijitoa moyo kwamba anafahamu tu.
-----
Mbweni, dar es salaam
Ghafla, mlango wa jikoni ulianza kufunguliwa taratibu. Tjedi alinyanyuka kimya kama kivuli na kushika kisu kilichokuwa mezani. Emmy na Zara walijificha nyuma ya kabati kubwa la chuma lililokuwa pembeni, wakitetemeka kwa hofu.
Mlango ulipofunguka kidogo, kivuli cha mguu kilionekana. Kabla jambazi hajaingiza mwili wote ndani, Tjedi alimrukia kwa kasi na kumchoma kisu kwenye koromeo
Pah! Pah!
Yule jambazi aliachia risasi mbili zilizomkosa kosa Tjedi na kupiga ukutani huku damu zikitoka kwa kasi kwenye koromeo lake akajikuta akiishiwa nguvu, na kudondosha bunduki huku mwili wake ukianguka kwa kishindo kwenye sakafu
"Wapo huku chini!" Mmoja wa majambazi alipiga kelele baada ya kusikia milio ya risasi.
"Haraka, inabidi tuondoke hapa", Tjedi alisema kwa sauti ya haraka lakini tulivu. "Kuna mlango wa dharura unaotokea kwenye njia ya chini ya ardhi. Njooni!"
Wakiwa na hofu na mioyo ikidunda kwa kasi, Zara na Emmy walimfuata Tjedi kwa haraka kupitia korido ya siri iliyo nyuma ya friji kubwa la jikoni. Njia hiyo Ilijengwa na bwana Aesh kwaajili ya dharura kama hizi, lakini haijawahi kutumika, hadi leo.
Walitembea kwa haraka kwenye njia hiyo hadi walipofika kwenye mlango mwingine wa chuma. Tjedi alitoa funguo kwenye shingo yake, akauufungua. Mlango ulifunguka kuelekea kwenye msitu mdogo nyuma ya nyumba.
"Hatuwezi kutumia gari. Tutasonga kwa miguu hadi tutakapoona usalama. Tutampigia Bwana Aesh baadaye, Zara" Tjedi alisema.
Zara aliangalia nyuma, machozi yakimtoka. “Wameua mtu nyumbani kwetu... Kwa ajili yangu.”
Tjedi alimwekea mkono begani. “Tutalipa kisasi Lakini kwanza ni lazima tuishi”