DPN
Member
- Sep 28, 2020
- 97
- 180
Sidhani kama unajua kilichowapata M23 kule DRC enzi za JK akiwa Presdaa; ungelijua hilo ungekuja na kauli tofauti na uliyoitoa hapo juu.Ka nchi kenye ukubwa wa kariakoo kutoka mashariki mwa Africa leo kameenda kuzima jaribio la kigaidi lililoitesa Mozambique na SADC nzima?
Afu tunataka kusema Tanzania tunaweza kuwahimili Rwanda kijeshi... Mnatania nyie.
M23 walikuwa na full backup ya haohao unaowapigia chapuo; walisumbua kiasi cha kutaka kuiondosha serikali iliyokuwa madarakani DRC wakati ule!!
Juliet Whiskey Tango Zulu ndio waliowafurusha hao vijana wa "Tall" kutoka DRC; mpaka "Tall" akanuna!!
Leo hii kwa kuwa vijana wa "Tall" wameondosha "kikundi" cha freelance wapiganaji, wasiokuwa na mkakati wowote wa kijeshi, majambazi, wezi na waporaji unawapa credit vijana wa "Tall"?
Hapakuwa na vita huko Msumbiji; palikuwa na ujambazi tu. Kilichofanyika ni jambazi kukabili jambazi mwenzie tu.
Hakuna vita ya kuua raia, kuiba mali za raia na kubaka; vita ni combat kati ya askari na askari; na ni kitendo halali pale nchi inapokuwa imevamiwa kijeshi " fully" sio kwa insurgents au majambazi kama wa Msumbiji. Umeelewa?