Mchezo wa Biko wanashinda wenye namba za tigo tu na Wengi wanatoka Dar es Salaam

Mchezo wa Biko wanashinda wenye namba za tigo tu na Wengi wanatoka Dar es Salaam

jambo Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Posts
377
Reaction score
281
Nimefuatilia washindi karibu wote ni kampuni ya tigo tu.je kwanini voda na makampuni wengine hawashindi?
===================================================

Kinachonishangaza kwenye BIKO ni hivi vifuatavyo

Kwanza Washindi walio wengi wanatokea Dar haswa Mbagala na Tabata.

Pili Namba zinatembea mda mchache sana. Katika kuchezesha.

Tatu Kila namba inayoshinda ikipigwa simu inapatikana muda huo huo hakuna cha network kusumbua wala nini. Haijawahi kukosekana hewani hata siku moja. Wahusika huwa hawakai mbali na simu

Nne Nakumbuka Vodacom walikuwa wanafanyaga zao kipindi cha nyuma wakipiga haipatikani inatafutwa ya pili hadi ya tatu mbona hawa hakunaga hivyo? Au hii ni bahati nasibu ya vipi?

Ps. Kuna mchezo mchafu unachezwa nyuma ya pazia kama Tatu Mzuka tu mana hawa nao ukiweka namba kubwa wanakwambia iliyoshinda ni ndogo ukiweka ndogo wanakwambia iliyoshinda ni kubwa huu nautafsiri kama ni uhuni huu.
 
Kuna staff mmoja namba 0754****87,anakula sana rushwa
 
Nimedadavua na kusubiri kuona hats mabadiliko kwa kadiri Sikh zinavyosonga na mchezo huu wa ,Nguvu ya Buku'nikaishia kugundua kuwa matokeo bado ni Yale Yale.
Katika mitandao ya mawasiliano kwa simu za mkononi zinazohusika katika mchezo huo ni mbili tu huwa Wateja wake wanashinda kati ya mitatu.
Swali, je hao wa mtandao mwingine wao hawachezagi?
 
Asee hizi kamari za kishamba waachieni wakulima huko vijijini wacheze ..hizi ni kama promotion za mitandao.atleast uishie kubet soccer
 
Leo itakuwa wengi tumeangalia huu mchezo maana leo mara ya kwanza kuona wakiwa wanachezesha.
 
Back
Top Bottom