Mchezo wa Draft ndio mchezo unaoshika nafasi ya pili kwa kupendwa nchini Tanzania, Serikali ikae na wadau kuanzisha na kuendeleza mchezo huu

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Ukiondoa mpira mguu, mchezo wa draft ndio mchezo ambazo unachezwa katika wilaya zote nchini, hakuna wilaya hapa nchini utaenda utakosa wachezaji wa mchezo huu, nenda wilaya yoyote draft lipo na wachezaji wapo, Dar es salaam ndio balaa, kule manzese, mbagala, kinondoni ndio kuna mafundi wakubwa draft.

Yupo mkongwe anaitwa Mangwelele serikali imtafute huyu pamoja na Shaban Katoto, ili wakae wanao wawakusanyie wadau wa mchezo huu ili draft uwe ni mchezo uliorasimishwa kama mpira wa miguu, kwa kuisaidia serikali iende pale Kitunda kwenye baa moja inaitwa Java yule mmiliki wa Java baa huwa anaita mafundi wote wa draft TAnzania anadhamini na watu wanajaa kama wako uwanja wa Taifa, ndugu yangu Gerson Msigwa mama yetu Dkt.Samia atakuwa amepata heshima kubwa kwa vijana hawa nchini kote.

Cha msingi waiteni wadau mkae nao muwasikilize ili muswada upelekwe bungeni kuanzisha chama cha draft nchini, chama hiki kitafanya kazi ya kupita wilaya zote kutengeneza uongozi na baadae kuanzisha ligi ya wilaya kisha ligi ya mkoa na baadae ligi ya TAifa.

Msigwa utakuwa umemsaidia sana Rais katika kuendeleza burudani na michezo, narudia hata wabunge akina mrisho Gambo ni wachezaji wazuri wa draft, Antony Mavunde naye pia, yaani wilaya zote ukienda vijiweni draft linapigwa.

Hebu fikiria kwa mfano sasa hivi tu mkasema muwaagize wakuu wa mikoa na wilaya muwape fedha shs milioni 5 tu kila wilaya waanzishe ligi ya draft utakuwa umemtangaza sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna dogo huyo hafungiki kwenye draft sasa hivi, anaitwa Dogo Sisco yuko pale Manzese Watu Huru, kuna Noel Namaloe, Dogo Janja, Amani Siri Mchunguzi, Dogo Shuku, Issa Mamba, Dogo Ally, Nduli Ndulima, CR7, Gaidi, Dogo Shuku, Omary Kiwembe nk.

Serikali isipuuze, fanyeni utafiti kwa kuwauliza wakuu wa mikoa kama katika wilaya zao kuna mchezo wa draft au hakuna mtakuja kunipa majibu.Mchezo huu mimi mwenyewe naucheza na siwezi kulala hadi niucheze.

Mchezo huu una sytle mbalimbali kuna staili inaitwa Mabano, Tege, Kavimba, Taa treni, Meja, Nuguza nk.

Chonde chonde serikali uangalieni huu mchezo wa draft mlete heshima kwa serikali.
 
Huu mchezo ni wa kutumia akili
 

Attachments

  • ed588717745b4326882608db4be3c883.mp4
    1.8 MB
Ianzishe tena?
 
Hapa mwenyewe nucheza balaaa siku haipiti bila kucheza
 
kabla sijachangia, kwanza sheria za draft Tanzania zibadilishwe, King zipunguziwe nguvu kama Ulaya , yani king inapaswa kuwa na nguvu kidogo zaidi ya kete ya kawaida hivyo itaruhusiwa kwenda one step diagonal tu, na sio king inavuka vyumba 2,3,4,5,6 hii si sawa.

Pia je huyu jamaa anaeitwa MANGWELELE ni kweli bingwa wa Draft katika nchi hii
 
kwa Sheria za Draft la Tanzania zibadilishwe kidogo, iwe kama america, kingi isiweze kwenda step zaidi ya moja direction zote, hao sio kwamba hawafungiki ni sheria mbovu za draft la kitanzania
 
pasati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…