Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wkt mchezo wa magari tanzania ngazi ya kitaifa unaingia raundi ya sita inayotarajia kufanyika jijini arusha ili kumpata bingwa wataifa wa mchezo huo nakaribisha maswali yoyote yanayohusiana na mchezo huo na jinsi unavyoendeshwa karibuni.
je ukitaka kushiriki katika ngazi za awali unafanyaje??
Cha kwanza kbsa unatakiwa kuwa na lesen ya kawaida ya udereva thn jiunge na club zilizopo ktk mikoa tofauti kwamfano arusha kuna amsc,dar kuna mmsc na dmsc,tanga kuna tmsc,kilimanjaro kuna kmsc ambapo kupitia club utajifunza sheria na taratibu za kutimiza ndoto zako karibu
Embu tukumbushe baadhi ya madereva wa magari waliowai kutingisha kwenye hii tasnia ya mashindano
.
Embu tukumbushe baadhi ya madereva wa magari waliowai kutingisha kwenye hii tasnia ya mashindano
.
Ni mambo gani yanaangaliwa wakat wa mashindano ilikumpata mshindi?
Madereva waliowai kutingisha kuna kina tosky hans wa arusha,collins higgins wa morogoro,gerald miller,kirit pandya,jayant shah,mzee lesirwa,lukumayi,humprey soka,hussein jettex,omar bakhressa,ahmed huwel,balbou,khalid bakhressa( r.i.p),navraj hans,randeep birdi,amarjit dhillon,pano,baba dee,twalib etc
Mshindi akishinda anapewa zawadi gani?je dereva akipata ajali akaumia na gari lake kuharibika nani anawajibika kumtibu dereva pia na kutengeneza gari lake?
Kutokana na kutokuwa na udhamin mkubwa kwny mchezo huu washind hupewa vikombe labda ikatokea mdhamin bas huwa wanapata hela,na ikitokea dereva akaumia wkt wa mchezo insurance ndo huwa ina mgharamia matibabu yake kwasababu huwez kuwa na leseni ya kuendesha haya magar bla kukata insurance na pindi itakapokea gar lmeharibika kama dereva ni self sponsered bas hulitengeneza gar lake mwnyw lkn kana ana udhamin bas kampuni husika ndo hutengeneza ilo gari
Asante mkuu kwa ufafanuzi mzuri.je kwanzia umri gani wanaruhusiwa kushiriki na ni watanzania tu au n watu wote wanaruhusiwa?
Umri ni kuanzia miaka 18 imbayo inakuruhu kumiliki leseni lkn tunawaimiza madereva kuanza kuwajenga watoto wao mapema ili kupata madereva wenye ushindani bdae kuhusu ushiriki watu wote wanaruhusiwa kama haya mashindano yanayokuja kufanyika arusha tunategemea madereva kutoka kenya,uganda na zambia