Mchezo wa mieleka Una ukweli wowote?

Mchezo wa mieleka Una ukweli wowote?

Mieleka ni ya kweli na inachezwa chini ya sheria zake km ilivyo ndondi, karate, nk, ila tofauti ni pale kuumizana kuvunjana inapokuwa ruksa. Wapo walioua ulingoni, mfano rey mysterio, Brock lesnar hawa waliua ulingoni. Wapo waliovunjwa shingo mfn Daniel brayan, edge ikabidi wastaafishwe mieleka ktk umri mdogo tu... Km mieleka ingekuwa igizo tu wasingeweza kuwatoza kiingilio cha $ 120+, na watu zaidi 65,000 hugarimika kuingia uwanjani. Bifu inapotokea kwa wanamieleka inakuwa mtaji tosha kwa kampuni na haifurahii wanamieleka wapendane....Hakuna mwanamieleka masikini 90% ni matajiri. Unapokuwa mbabe kwa wenzio kila mara ndivo na pato lako inavoongezeka na bonas juu ndio maana mara pengine hushambuliana kwenye korido, vyumbani au hata hospital, au ndani ya ambulance nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mieleka ya WWE ni real na ndiyo mieleka bora zaidi hapa duniani
Wacheza mieleka hua trained kwa muda mrefu sana kabla ya kua drafted kwenye WWE, hii huwawezesha kucheza ule mchezo kwa ustadi mkubwa pasipo kutokea madhara hatarishi
Zifuatazo ni baadhi ya sheria muongozo kwa mchezo wa mieleka:
1. Hakuna kutumia kipepsi(elbow) kumpiga mwenzio. Hua wanatumia nyama iliyopo upande wa nyuma ya mkono kutoka kwenye kipepsi kwenda kwapani. Refer Shawn Michaels anavyomrukia mpinzani wake kutoka top cornered rope.
2. Hakuna kutumia knuckles unapompiga ngumi mwenzio.
3. Hakuna kumpiga kifuti au goti(knee) mwenzio. Kinachotumika ni nyama ya juu ya paja. Refer Brock Lesnar
4.Ngumi ya kata funua(upper cut) hairuhusiwi. Kunja vidole vyako vya mkononi vikate kiganja chako nusu ndipo unaweza piga upper cut. Refer Roman Reigns and Kane
5. Hakuna kumpiga kichwa mwenzio eneo la kati ya chini ya fore head mpaka kidevuni. Eneo lote la mdomo na pua hubaki safe
6. Hairuhusiwi kumpiga mwenzio na teke la kwenda juu na kumpiga mpinzani wako maeneo ya kidevuni akiwa ameinama au amechuchumaa. Hii huwalinda na ung'okaji wa meno

Zipo sheria nyingi zaidi zinazofanya huo mchezo uwe safe, na ukweli ni kua hakuna burudani tamu zaidi hapa duniani zaidi ya mieleka.
Paragraph ya mwisho, umedanganya! Hakuna tamu kama papuchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mieleka ni ya kweli na inachezwa chini ya sheria zake km ilivyo ndondi, karate, nk, ila tofauti ni pale kuumizana kuvunjana inapokuwa ruksa. Wapo walioua ulingoni, mfano rey mysterio, Brock lesnar hawa waliua ulingoni. Wapo waliovunjwa shingo mfn Daniel brayan, edge ikabidi wastaafishwe mieleka ktk umri mdogo tu... Km mieleka ingekuwa igizo tu wasingeweza kuwatoza kiingilio cha $ 120+, na watu zaidi 65,000 hugarimika kuingia uwanjani. Bifu inapotokea kwa wanamieleka inakuwa mtaji tosha kwa kampuni na haifurahii wanamieleka wapendane....Hakuna mwanamieleka masikini 90% ni matajiri. Unapokuwa mbabe kwa wenzio kila mara ndivo na pato lako inavoongezeka na bonas juu ndio maana mara pengine hushambuliana kwenye korido, vyumbani au hata hospital, au ndani ya ambulance nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutozwa kiingilio hakimaanishi kinachofanyika pale ni real, mbona kwenye ma cinemax watu wanalipa kuangalia movies tu tena kwenye screen.
kinachafanyika pale kiko planned(scripted) hasa ku determine mshindi, wanapigana kiuhalisia but ukijua mwisho wa siku ninashinda ama anashinda.. it's called reality show.
kufa kwa baadhi ni ajali kama ilivyotokea kwa Paul Walker.
 
Mchezo wa mieleka Una ukweli wowote?
Wengine wanadai ni kweli Na wengine wakidai ni mchezo unaopangwa yaani wa kuigiza tu mbele ya hadhira!!

Wapi ni wapi[emoji21][emoji21][emoji21][emoji21][emoji21]!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengi hawawezi kuukubali ukweli kwa sababu ya mapenzi yao kwenye hii burudani(entertainment),cha kwanza lazima ujue hii ni burudani tu na so mchezo(sport).Kingine ambacho huwa hakiwekwi wazi kwa sababu za kibiashara ni kuwa huwa kuna rehearsals na ndio maana watu(mainly watoto) huonywa kujaribu kwakuwa wao huamini moja kwa moja wakidhani kuna uhalisia kama kwenye boxing.Kuna mambo mengi kwa mtu yoyote mwenye fikra lazima awastukie kuwa sanaa ndio inayoendelea na wala si mpambano halisi. Nakushauri tu hata kama unamapenzi kiasi gani na hiyo burudani,jaribu kutumia 'jicho' la tatu wakati unaangia wanavyofanya.Haitakuchukua hata dkk2 utaweza kutenganisha pumba na mchele.
 
MMA tu ndo halisi.wale jamaa wa WWE wanaitwa 'performers' so wanatufanyia maigizo tu pale.
Script na bifu zinatemgenezwa ili kuweka mvuto ila pale ukumbini baadhi ya mechi ni kweli, mfano money in the bank!
 
Na mimi anataka kufahamu kama ni kweli au wanaigiza.Japo nafahamu kuna waigizaji maalum wa porno
Kama vyombo vinaingiliana bado kuna maigizo tena?

Igizo ni ku'act' upresidaa kwenye movie wakati wewe ni mchimba chumvi wa Uvinza.

Kama sikosei Eminem aliwahi kutaka kuingia huko kwenye tasnia ya mieleka lakini daktari wake akamzuia kwamba kwa weight yake hawezi. Nadhani sehemu kubwa ni uhalisia isipokuwa kama ni kweli wanaandaa script na kuzifanyia mazoezi ni kwa lengo la kuleta mvuto wa pambano. Kumbuka bila hivyo ingekuwa kuna mapambano hayachukui hata dakika 3 hasira zingemaliza pambano

Ok kwahiyo inapangwa fulani ashinde? Maana mtu analegezwa kama mlenda halafu mwishoni anashinda yeye na vipi hairuhusiwi kuzuia ngumi? Maana unakuta mtu anapigwa za uso bila kuzuia
 
try it at home, halafu uje na feedback hapahpa
 
Hauna uhalisia hata kidogo maana wangekuwa wamekufa wengi sana, hata bifu zao huwa ni feki

Small minded people won't understand
Wanapigana kwa kupokezana! Jamaa kaishiwa nguvu, ghafla anaibuka kuwa mshindi!
 
Kwani ninyi hamkuwahi kuiangalia ile mieleka ya akina
Power Bernado
Power Mwanza
Power Vuru Mroma
Power Chaka, nk.
Walivyokuwa wanacheza mieleka wakati ule ?
Katika WWE kuna baadhi ya matukio ya kutangaza pambano huwa wanaigiza ili kuchochea pambano.
Lakina unapoona Mkanda umewekwa ujue ni pambano halisi.
Mfano Mchezaji Jeff harry alikuwa anakataa kucheza na mdogo wake Joe harry, mdhamini alimpa pesa Joe ili amchokoza Jeff ili apandwe na hasira hadi akubali kucheza naye, hapo sasa utaona maigizo ya kuwafanya mashabiki waje kwa wingi kuuona mchezo wao.
Wazungu hawawezi kutoa pesa yao kuangalia maigizo ya mieleka.
Kama ni maigizo basi ungeona kila mtu anaicheza huo mchezo, na hata vimbaumbau wangewapiga wenye nguvu kama The Undeteka.
Kuna wachezaji wengi tu walijeruhiwa na wengine kufia uringoni.
Wakati ule wa akina Power Bernado walikuwa wanacheza kama leo unavyoona katika WWE. viti maalum vilitumika kupigania uringoni.
Mzee wangu alikuwa anapenda sana kuangalia mieleka na alikuwa anaenda na mimi karibu kila pambano la mieleka.
WWE ni mchezo halisi, na uliwahi kuchezwa hata hapa TZ.
Kwasasa mchezo huu hauchezwi hapa kwetu kwakuwa chama cha mieleka kimeshindwa kutimiza kanuni za mchezo, na kughalamia maandalizi, vifaa, matibabu, ukumbi na uringo wa mchezo huo.
Umemsahau Power Mangwana mkuu!

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom