screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Kwa kipindi cha miaka kama miwili hivi mchezo wa ngumi ulionekana kurudi kwa kasi na kuanza kufuatiliwa na watanzania wengi kama ilivyokuwa huko nyuma enzi za kina Rashid Matumla.
Hii ilichochewa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Mwakinyo ambaye alipata jina baada ya kumtwanga Mwingereza ambaye alikuwa Rank za juu kwenye uzito wake, bila kuwasahau Azam Sports kuamua kuupromote mchezo huu na kurusha mapambano live hivyo watanzania wengi kuweza kushuhudia.
Kwa kipindi hicho kumetokea mapambano kadhaa ambayo yalivuta hisia za watanzania wengi, kama Mwakinyo vs Tinampay, Dulla Mbabe vs Twaha Kiduku, na mengineyo, lakini ukweli ni kwamba kadri siku zinavyosonga naona ile hamasa inazidi kupotea.
Mfano ni pambano la jana la Mwakinyo dhidi ya raia wa Angola, halijapata airtime sana kiasi kwamba ni Watanzania wachache wanajua kwamba Mwakinyo jana alikuwa ulingoni, na hata ile hamasa naona imepungua, sivyo kama Mwakinyo alivyokuwa akisubiriwa kucheza pambano na Tinampay.
Binafsi ningependa vitu hivi virekebishwe kabla jahazi halijazama, nadhani vinachangia kwa kiasi kikubwa kushusha hamasa iliyoanza kuonekana;-
1. Ubora wa mabondia wanaoletwa kutoka nje
Hili limesababisha boxing kupoteza mvuto na kusababisha mashabiki wengi wa boxing huko nje kukimbilia kuangalia 'UFC', sehemu ambayo 'the best' always anapiga na 'the best', huwezi kuta bingwa anapigana na wajinga wajinga, ukiwa ranked no1 utapigana na no 2-5 au atleast top 10, na sio maboya.
Nalisema hili kwavile nimefatilia huyo jamaa aliyepigana na Mwakinyo jana amekuwa ranked no 150 huko boxRec, Mwakinyo hawezi kusonga mbele kama ataendelea kupigana na watu wa namna hii, kwa level zake ilipaswa apigane na mabondia atleast top 70, huwa namshangaa anavyosema hawezi kupigana na kina Kiduku wakati ukifatilia kwenye ranking wako juu kuliko hao mabondia anaoletewa kutoka nje.
All in all mabondia wengi wanaoletwa kutoka nje wako chini ya kiwango, waandaaji hulifanya hili makusudi kwa ajili ya kuwalindia rekodi 'wa kunyumba', ili wawatengenezee majina mazuri na kuendelea kuwatumia kupiga hela, ndio maana mabondia hawa wanaoonekana bora hapa bongo wakitoka kupigana nje wanakuwa hawana maajabu.
2. Majaji/Marefa
Marefa nao wamekuwa wakifanya makosa mengi 'kwa makusudi' ili tu kuwalinda wenyeji
3. Kushindwa kutengeneza majina makubwa mapya
Binafsi kama shabiki siko interested kuona Twaha akipigana tena na Dulla, hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa sasa kwavile mapambano yote mawili Dulla alipoteza (lile la kwanza Dulla alipewa droo kimagumashi).
Waandaaji wajiulize kwanini wanashindwa kutengeneza majina mapya, hili linasababisha kulazimisha kina Kiduku, Dulla kucheza mapambano mengi kwa mwaka kwa sababu ndio majina ambayo kidogo yanauza. Ilitakiwa kwa mwaka wasicheze mapambano zaidi ya mawili ili mashabiki wawe na hamu ya kuwaona.
4. Kisimbuzi za Azam kingeendelea kuonesha mapambano haya
NB: Mapungufu yapo mengi ila mengine yanavumilika, yataendelea kupungua kadri wanavyoandaa mapambano zaidi, kwa mtazamo wangu hayo niliyoandika juu yanachangia kiasi kikubwa kupunguza hamasa ya mchezo huu, watu tunataka kuona ushindani wa kweli na sio Magumashi

Hili ndio tatizo kubwa, na hili ni tatizo la Dunia nzima, maana hata huko mbele tunaona mabondia wengi wazuri/mabingwa wanapenda kupigana na mabondia 'nyanya' ili kuendelea kulinda rekodi zao.
Hili limesababisha boxing kupoteza mvuto na kusababisha mashabiki wengi wa boxing huko nje kukimbilia kuangalia 'UFC', sehemu ambayo 'the best' always anapiga na 'the best', huwezi kuta bingwa anapigana na wajinga wajinga, ukiwa ranked no1 utapigana na no 2-5 au atleast top 10, na sio maboya.
Nalisema hili kwavile nimefatilia huyo jamaa aliyepigana na Mwakinyo jana amekuwa ranked no 150 huko boxRec, Mwakinyo hawezi kusonga mbele kama ataendelea kupigana na watu wa namna hii, kwa level zake ilipaswa apigane na mabondia atleast top 70, huwa namshangaa anavyosema hawezi kupigana na kina Kiduku wakati ukifatilia kwenye ranking wako juu kuliko hao mabondia anaoletewa kutoka nje.
All in all mabondia wengi wanaoletwa kutoka nje wako chini ya kiwango, waandaaji hulifanya hili makusudi kwa ajili ya kuwalindia rekodi 'wa kunyumba', ili wawatengenezee majina mazuri na kuendelea kuwatumia kupiga hela, ndio maana mabondia hawa wanaoonekana bora hapa bongo wakitoka kupigana nje wanakuwa hawana maajabu.
2. Majaji/Marefa
Mara kadhaa tumewaona wakiwabeba sana wenyeji, hii hutokea sana inapofikia mechi imeisha bila KO/TKO, majaji wamekuwa wakipika point kupita kiasi ili kumfavour mwenyeji, ndio mcheza kwao hutuzwa ila kuna vitu vingine sio vya kubebana/ sio vya kulazimisha, mfano Mfaume Mfaume kuna pambano alicheza mwanzoni mwa mwaka, matokeo ya majaji yalichefua wengi, vitu kama hivi vinaua hamasa ya kufatilia huu mchezo hawajui tu, maana anayeangalia anajua tu mwisho wa siku ushindi atapewa wa nyumbani.
Marefa nao wamekuwa wakifanya makosa mengi 'kwa makusudi' ili tu kuwalinda wenyeji
3. Kushindwa kutengeneza majina makubwa mapya
Sijashangaa kuona Twaha Kiduku na Dulla Mbabe wanapigana mara ya 3, kupigana mara nyingi sio kitu cha ajabu kwenye ndondi kwani hata huko mbele tunaona Wilder na Fury wanapigana kwa mara ya 3, lakini utofauti ni kwamba kule wanachopigania ni World Title, sasa hawa kina Dulla wanapigania nini hasa?[emoji16][emoji16], Mi nadhani waandaaji wanalazimisha hili kutokana na kushindwa kutengeneza majina mengine makubwa.
Binafsi kama shabiki siko interested kuona Twaha akipigana tena na Dulla, hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa sasa kwavile mapambano yote mawili Dulla alipoteza (lile la kwanza Dulla alipewa droo kimagumashi).
Waandaaji wajiulize kwanini wanashindwa kutengeneza majina mapya, hili linasababisha kulazimisha kina Kiduku, Dulla kucheza mapambano mengi kwa mwaka kwa sababu ndio majina ambayo kidogo yanauza. Ilitakiwa kwa mwaka wasicheze mapambano zaidi ya mawili ili mashabiki wawe na hamu ya kuwaona.
4. Kisimbuzi za Azam kingeendelea kuonesha mapambano haya
Kwa sasa watanzania wengi wanamiliki kisimbuzi cha Azam, sijajua kwa nini pambano la jana la Mwakinyo limekuwa hosted na DSTV, hili limesababisha wengi kushindwa kuangalia live pambano hilo tofauti na mapambano yake mengine ambayo yalikuwa hosted na AZAM.