Mchezo wa Ngumi (Boxing) unaelekea kufa tena wasiporekebisha haya

Mchezo wa Ngumi (Boxing) unaelekea kufa tena wasiporekebisha haya

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Kwa kipindi cha miaka kama miwili hivi mchezo wa ngumi ulionekana kurudi kwa kasi na kuanza kufuatiliwa na watanzania wengi kama ilivyokuwa huko nyuma enzi za kina Rashid Matumla.

Hii ilichochewa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Mwakinyo ambaye alipata jina baada ya kumtwanga Mwingereza ambaye alikuwa Rank za juu kwenye uzito wake, bila kuwasahau Azam Sports kuamua kuupromote mchezo huu na kurusha mapambano live hivyo watanzania wengi kuweza kushuhudia.

Kwa kipindi hicho kumetokea mapambano kadhaa ambayo yalivuta hisia za watanzania wengi, kama Mwakinyo vs Tinampay, Dulla Mbabe vs Twaha Kiduku, na mengineyo, lakini ukweli ni kwamba kadri siku zinavyosonga naona ile hamasa inazidi kupotea.

Mfano ni pambano la jana la Mwakinyo dhidi ya raia wa Angola, halijapata airtime sana kiasi kwamba ni Watanzania wachache wanajua kwamba Mwakinyo jana alikuwa ulingoni, na hata ile hamasa naona imepungua, sivyo kama Mwakinyo alivyokuwa akisubiriwa kucheza pambano na Tinampay.

Binafsi ningependa vitu hivi virekebishwe kabla jahazi halijazama, nadhani vinachangia kwa kiasi kikubwa kushusha hamasa iliyoanza kuonekana;-


1. Ubora wa mabondia wanaoletwa kutoka nje

Hili ndio tatizo kubwa, na hili ni tatizo la Dunia nzima, maana hata huko mbele tunaona mabondia wengi wazuri/mabingwa wanapenda kupigana na mabondia 'nyanya' ili kuendelea kulinda rekodi zao.

Hili limesababisha boxing kupoteza mvuto na kusababisha mashabiki wengi wa boxing huko nje kukimbilia kuangalia 'UFC', sehemu ambayo 'the best' always anapiga na 'the best', huwezi kuta bingwa anapigana na wajinga wajinga, ukiwa ranked no1 utapigana na no 2-5 au atleast top 10, na sio maboya.

Nalisema hili kwavile nimefatilia huyo jamaa aliyepigana na Mwakinyo jana amekuwa ranked no 150 huko boxRec, Mwakinyo hawezi kusonga mbele kama ataendelea kupigana na watu wa namna hii, kwa level zake ilipaswa apigane na mabondia atleast top 70, huwa namshangaa anavyosema hawezi kupigana na kina Kiduku wakati ukifatilia kwenye ranking wako juu kuliko hao mabondia anaoletewa kutoka nje.

All in all mabondia wengi wanaoletwa kutoka nje wako chini ya kiwango, waandaaji hulifanya hili makusudi kwa ajili ya kuwalindia rekodi 'wa kunyumba', ili wawatengenezee majina mazuri na kuendelea kuwatumia kupiga hela, ndio maana mabondia hawa wanaoonekana bora hapa bongo wakitoka kupigana nje wanakuwa hawana maajabu.

2. Majaji/Marefa
Mara kadhaa tumewaona wakiwabeba sana wenyeji, hii hutokea sana inapofikia mechi imeisha bila KO/TKO, majaji wamekuwa wakipika point kupita kiasi ili kumfavour mwenyeji, ndio mcheza kwao hutuzwa ila kuna vitu vingine sio vya kubebana/ sio vya kulazimisha, mfano Mfaume Mfaume kuna pambano alicheza mwanzoni mwa mwaka, matokeo ya majaji yalichefua wengi, vitu kama hivi vinaua hamasa ya kufatilia huu mchezo hawajui tu, maana anayeangalia anajua tu mwisho wa siku ushindi atapewa wa nyumbani.

Marefa nao wamekuwa wakifanya makosa mengi 'kwa makusudi' ili tu kuwalinda wenyeji

3. Kushindwa kutengeneza majina makubwa mapya
Sijashangaa kuona Twaha Kiduku na Dulla Mbabe wanapigana mara ya 3, kupigana mara nyingi sio kitu cha ajabu kwenye ndondi kwani hata huko mbele tunaona Wilder na Fury wanapigana kwa mara ya 3, lakini utofauti ni kwamba kule wanachopigania ni World Title, sasa hawa kina Dulla wanapigania nini hasa?[emoji16][emoji16], Mi nadhani waandaaji wanalazimisha hili kutokana na kushindwa kutengeneza majina mengine makubwa.

Binafsi kama shabiki siko interested kuona Twaha akipigana tena na Dulla, hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa sasa kwavile mapambano yote mawili Dulla alipoteza (lile la kwanza Dulla alipewa droo kimagumashi).

Waandaaji wajiulize kwanini wanashindwa kutengeneza majina mapya, hili linasababisha kulazimisha kina Kiduku, Dulla kucheza mapambano mengi kwa mwaka kwa sababu ndio majina ambayo kidogo yanauza. Ilitakiwa kwa mwaka wasicheze mapambano zaidi ya mawili ili mashabiki wawe na hamu ya kuwaona.

4. Kisimbuzi za Azam kingeendelea kuonesha mapambano haya
Kwa sasa watanzania wengi wanamiliki kisimbuzi cha Azam, sijajua kwa nini pambano la jana la Mwakinyo limekuwa hosted na DSTV, hili limesababisha wengi kushindwa kuangalia live pambano hilo tofauti na mapambano yake mengine ambayo yalikuwa hosted na AZAM.

NB: Mapungufu yapo mengi ila mengine yanavumilika, yataendelea kupungua kadri wanavyoandaa mapambano zaidi, kwa mtazamo wangu hayo niliyoandika juu yanachangia kiasi kikubwa kupunguza hamasa ya mchezo huu, watu tunataka kuona ushindani wa kweli na sio Magumashi
 
Umeongea ukweli kabisa mdau...hili walifanyie kazi.
Katika jambo lililonitibua ni upendeleo wa wazi..huu ni upumbavu wa hali ya juu imeleta aibu kubwa.
Jambo lingine ni kwamba inasemekana kwamba mpinzani wa Mwakinyo alipewa short notice hivyo kuwa na maandalizi duni...kama hili ni kweli itakuwa ni kitu kibaya sana.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Hayo mapambano ya vitasa plus wangeyaondoa tu maana namna watu wanavyopigana utadhani waliokotwa tu mtaani bila training yoyote wakapelekwa ulingoni yani kwa kifupi ni mapambano yasiyo na ladha kabisa ..
Omba wewe pambano utest tujue hao wanaokotwa au wanauza game
 
Umeongea ukweli kabisa mdau...hili walifanyie kazi.
Katika jambo lililonitibua ni upendeleo wa wazi..huu ni upumbavu wa hali ya juu imeleta aibu kubwa.
Jambo lingine ni kwamba inasemekana kwamba mpinzani wa Mwakinyo alipewa short notice hivyo kuwa na maandalizi duni...kama hili ni kweli itakuwa ni kitu kibaya sana.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Short notice inakubalika endapo mpinzani aliyepangwa awali amepata dharura itayomfanya asiweze cheza pambano husika. Mfano Andy Ruiz alipewa short notice kupigana na Anthony Joshua baada ya mpinzani wa awali Jarrel Miller kushindwa kupass vipimo, na Andy Ruiz akaitumia hiyo nafasi vizuri na kufanikiwa kuwa mmexico wa kwanza kutwaa taji la dunia la uzito wa juu. Ila kumpa short notice mpinzani pasipo dharura yoyote si sawa
 
Yaani Dstv wasioneshe Kwa sababu?

Yaani Azam ndo waoneshe Peke yao?

Seriously?
 
Yaani Dstv wasioneshe Kwa sababu?

Yaani Azam ndo waoneshe Peke yao?

Seriously?
Kwanini DSTV pekeyao waonyeshe UEFA/ EPL hapa Tanzania? Ukijibu hilo na mimi nitakujibu
 
Kwa kipindi cha miaka kama miwili hivi mchezo wa ngumi ulionekana kurudi kwa kasi na kuanza kufuatiliwa na watanzania wengi kama ilivyokuwa huko nyuma enzi za kina Rashid Matumla, hii ilichochewa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Mwakinyo ambaye alipata jina baada ya kumtwanga Mwingereza ambaye alikuwa Rank za juu kwenye uzito wake, bila kuwasahau Azam Sports kuamua kuupromote mchezo huu na kurusha mapambano live hivyo watanzania wengi kuweza kushuhudia. Kwa kipindi hicho kumetokea mapambano kadhaa ambayo yalivuta hisia za watanzania wengi, kama Mwakinyo vs Tinampay, Dulla Mbabe vs Twaha Kiduku, na mengineyo, lakini ukweli ni kwamba kadri siku zinavyosonga naona ile hamasa inazidi kupotea. Mfano ni pambano la jana la Mwakinyo dhidi ya MuAngola, halijapata airtime sana kiasi kwamba ni watanzania wachache wanajua kwamba Mwakinyo jana alikuwa ulingoni, na hata ile hamasa naona imepungua, sivyo kama Mwakinyo alivyokuwa akisubiriwa kucheza pambano na Tinampay. Binafsi ningependa vitu hivi virekebishwe kabla jahazi halijazama, nadhani vinachangia kwa kiasi kikubwa kushusha hamasa iliyoanza kuonekana;-


1. Ubora mabondia wanaoletwa kutoka nje
---Hili ndio tatizo kubwa, na hili ni tatizo la dunia nzima, maana hata huko mbele tunaona mabondia wengi wazuri/mabingwa wanapenda kupigana na mabondia 'nyanya' ili kuendelea kulinda rekodi zao, hili limesababisha boxing kupoteza mvuto na kusababisha mashabiki wengi wa boxing huko nje kukimbilia kuangalia 'UFC', sehemu ambayo 'the best' always anapiga na 'the best', huwezi kuta bingwa anapigana na wajinga wajinga, ukiwa ranked no1 utapigana na no 2-5 au atleast top 10, na sio maboya. Nalisema hili kwavile nimefatilia huyo jamaa aliyepigana na Mwakinyo jana amekuwa ranked no 150 huko boxRec, Mwakinyo hawezi kusonga mbele kama ataendelea kupigana na watu wa namna hii, kwa level zake ilipaswa apigane na mabondia atleast top 70, huwa namshangaa anavyosema hawezi kupigana na kina Kiduku wakati ukifatilia kwenye ranking wako juu kuliko hao mabondia anaoletewa kutoka nje. All in all mabondia wengi wanaoletwa kutoka nje wako chini ya kiwango, waandaaji hulifanya hili makusudi kwa ajili ya kuwalindia rekodi 'wa kunyumba', ili wawatengenezee majina mazuri na kuendelea kuwatumia kupiga hela, ndio maana mabondia hawa wanaoonekana bora hapa bongo wakitoka kupigana nje wanakuwa hawana maajabu.

2. Majaji/Marefa
---Mara kadhaa tumewaona wakiwabeba sana wenyeji, hii hutokea sana inapofikia mechi imeisha bila KO/TKO, majaji wamekuwa na wakipika point kupita kiasi ili kumfavour mwenyeji, ndio mcheza kwao hutuzwa ila kuna vitu vingine sio vya kubebana/ sio vya kulazimisha, mfano Mfaume Mfaume kuna pambano alicheza mwanzoni mwa mwaka, matokeo ya majaji yalichefua wengi, vitu kama hivi vinaua hamasa ya kufatilia huu mchezo hawajui tu, maana anayeangalia anajua tu mwisho wa siku ushindi atapewa wa nyumbani. Marefa nao wamekuwa wakifanya makosa mengi 'kwa makusudi' ili tu kuwalinda wenyeji

3. Kushindwa kutengeneza majina makubwa mapya
----Sijashangaa kuona Twaha Kiduku na Dulla Mbabe wanapigana mara ya 3, kupigana mara nyingi sio kitu cha ajabu kwenye ndondi kwani hata huko mbele tunaona Wilder na Fury wanapigana kwa mara ya 3, lakini utofauti ni kwamba kule wanachopigania ni World Title, sasa hawa kina Dulla wanapigania nini hasa?[emoji16][emoji16], Mi nadhani waandaaji wanalazimisha hili kutokana na kushindwa kutengeneza majina mengine makubwa. Binafsi kama shabiki siko interested kuona Twaha akipigana tena na Dulla, hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo kwa sasa kwavile mapambano yote mawili Dulla alipoteza (lile la kwanza Dulla alipewa droo kimagumashi). Waandaaji wajiulize kwanini wanashindwa kutengeneza majina mapya, hili linasababisha kulazimisha kina Kiduku, Dulla kucheza mapambano mengi kwa mwaka kwa sababu ndio majina ambayo kidogo yanauza. Ilitakiwa kwa mwaka wasicheze mapambano zaidi ya mawili ili mashabiki wawe na hamu ya kuwaona.

4. Kisimbuzi cha AZAM kingeendelea kuhost haya mapambano[/B]
---kwa sasa watanzania wengi wanamiliki kisimbuzi cha Azam, sijajua kwa nini pambano la jana la Mwakinyo limekuwa hosted na DSTV, hili limesababisha wengi kushindwa kuangalia live pambano hilo tofauti na mapambano yake mengine ambayo yalikuwa hosted na AZAM.

NB: Mapungufu yapo mengi ila mengine yanavumilika, yataendelea kupungua kadri wanavyoandaa mapambano zaidi, kwa mtazamo wangu hayo niliyoandika juu yanachangia kiasi kikubwa kupunguza hamasa ya mchezo huu, watu tunataka kuona ushindani wa kweli na sio Magumashi
Umeongea vizuri sana
Ungesisitizia pia kwa nini mabondia wanapingwa sasa hivi nje ya nchi kuliko pale awali walikuwa wanashinda sasa hivi mabondia wamekwenda nje ya nchi zaidi ya mara 25 lakini hamna hushindi
 
Short notice inakubalika endapo mpinzani aliyepangwa awali amepata dharura itayomfanya asiweze cheza pambano husika. Mfano Andy Ruiz alipewa short notice kupigana na Anthony Joshua baada ya mpinzani wa awali Jarrel Miller kushindwa kupass vipimo, na Andy Ruiz akaitumia hiyo nafasi vizuri na kufanikiwa kuwa mmexico wa kwanza kutwaa taji la dunia la uzito wa juu. Ila kumpa short notice mpinzani pasipo dharura yoyote si sawa
Uko sahihi, Brendon Denis aliyepangwa awali alipata majeraha yaliyomsababisha ashindwe kushiriki.
......
Tena bondia mwenyewe alikuwa hajapigana mwaka mzima alikuwa inactive. Alafu 10 days notice hataleta upinzani mzuri.
 
Only 14 African countries will be sending boxers to Tokyo for olympic games. Algeria leads with 8 boxers, Morocco is 2nd with 7 boxers while Kenya & DRC rank 3rd having 4 boxers each, Uganda, Zambia,Ghana& Cameroon have 3 boxers each are 4th in terms of number of boxers qualified for Tokyo Olympic games.... Opine please screpa
Screenshot_20210608-112649.jpg
 
Mwakinyo ana majivuno sana ilifika pahala mpaka akawa anawatusi mashabiki kwenye account take Instagram. Ninaona sasa kuna mtu amepewa kazi ya kuiendesha account take ya Instagram.
 
Kuna ' Vaccum' Ulimwenguni Karibia Michezo Yote...... ! Watu Kama Cassius Clay. Mike ' Iron Tyson ni ngumu Kuwapata Sasa Sembuse Bongo!!!
 
Back
Top Bottom