Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo wizara inamtabua mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.

Mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo thamani yake ni shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya Tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo,” amesema Prof. Msanjila.

Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.

1592987909310.png


====​
Serikali imenunua mawe hayo kutoka kwa mchimbaji huyo na yatawekwa katika makumbusho ya taifa
 
Back
Top Bottom