Mchina aingilia Miundombinu ya TCRA na kusababisha hasara Tsh. Milioni 221

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Raia wa China Li Naiyong amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita likiwemo kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh221 milioni.

Naiyong amesomewa mashtaka yake leo, Februari 15, 2023 na Wakili wa Serikali, Yusuph Aboud mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Akimsomea mashtaka yake, Aboud amedai kuwa kati ya Agosti 13 hadi Oktoba 22, 2022, katika Hoteli ya Hongkong iliyopo Kariakoo, Wilaya ya Ilala, aliingiza vifaa mbalimbali vya mawasiliano vya kielekroniki bila kuwa na leseni.

Wakili Abood amedai pia katika tarehe hizo mshitakiwa huyo alisimika na kusimamia mitambo ya mawasiliano ya kielekroniki bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Vilevile mshtakiwa huyo kwa nia ovu, alitumia mawasiliano kwa kutumia vifaa hivyo vilivyounganishwa katika njia ya mawasiliano kwa lengo la kupokea na kutoa mawasiliano, bila ya kuwa na leseni.

Shtaka la tano, mshitakiwa huyo anadaiwa kuendesha mitambo hiyo ya mawasiliano kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano kimataifa, pamoja na kufanya matumizi mabaya ya vifaa hivyo kwa nia ya kukwepa makato, kwa kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila leseni.

Shtaka la sita, katika tarehe hiyo kwa vitendo vyake hivyo, aliisababishia serikali na TCRA hasara ya Tsh. Milioni 221,163,600.

Upande wa mashtaka wamedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haukamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mazengo alitoa masharti ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo ambayo yamemtaka mshtakiwa kuwasilisha fedha taslimu Sh 110,581,800 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia mshtakiwa huyo ametakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja awe ni mtumishi wa Serikali.

Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo kurudishwa rumande hadi Machi Mosi, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa.
 
Kwani jamaa alileta mitambo ya kufanya nini hasa maana taarifa naona mawasiliank mawasiliano mawasiliano......hebu tupe nasi kisa hasa cha kwamba jamaa alikuwa anafanya nini tujue
SemperFI
 
Pale bandarini au airport nani aliruhusu hyo mitambo iingie?

Kama waliruhusu ilikuwa na kibali Cha kufanya nini?

Mbona saiz Kuna plastic na madawa ambayo hayana ubora nani anayaruhusu hata?

Fikiria na ogopa sana hii usije ukasikia hapo mwisho wa kesi hukumu itakuwa "kwakuwa mtuhumia aneisababishia serikali hasara ya Zaid ya 225m hvyo mahakama inamtia hatian mtuhumiwa hvyo afungwe jela miez sits au fain ya 6m.

Hapo hapo mtanzania aliekamatwa kwa kuiba baiskeli jela miaka 6 na fain ya million 2
 
Tundu Lissu ana lipi la kusema kuhusu hili?

CHADEMA wana lipi lakusema kuhusu hili?

kitaeleweka.
 
Raia wa China aingilia miundombinu TCRA, kusababisha hasara Sh221 mil​

Dar es Salaam. Raia wa China Li Naiyong amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita likiwemo kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh221 milioni

Naiyong amesomewa mashtaka yake leo, Februari 15, 2023 na Wakili wa Serikali, Yusuph Aboud mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Akimsomea mashtaka yake, Aboud amedai kuwa kati ya Agosti 13 hadi Oktoba 22, 2022, katika Hoteli ya Hongkong iliyopo Kariakoo, Wilaya ya Ilala, aliingiza vifaa mbalimbali vya mawasiliano vya kielekroniki bila kuwa na leseni.

Wakili Abood amedai pia katika tarehe hizo mshitakiwa huyo alisimika na kusimamia mitambo ya mawasiliano ya kielekroniki bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Vilevile mshtakiwa huyo kwa nia ovu, alitumia mawasiliano kwa kutumia vifaa hivyo vilivyounganishwa katika njia ya mawasiliano kwa lengo la kupokea na kutoa mawasiliano, bila ya kuwa na leseni.

Shtaka la tano, mshitakiwa huyo anadaiwa kuendesha mitambo hiyo ya mawasiliano kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano kimataifa, pamoja na kufanya matumizi mabaya ya vifaa hivyo kwa nia ya kukwepa makato, kwa kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila leseni.

Shtaka la sita, katika tarehe hiyo kwa vitendo vyake hivyo, aliisababishia serikali na TCRA hasara ya Sh221, 163, 600.

Upande wa mashtaka wamedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haukamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mazengo alitoa masharti ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo ambayo yamemtaka mshtakiwa kuwasilisha fedha taslimu Sh 110,581,800 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia mshtakiwa huyo ametakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja awe ni mtumishi wa Serikali.

Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo kurudishwa rumande hadi Machi Mosi, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Wachina wengi tuu humu bongo wanaishi bila vibali kazi na wanaendelea na maisha yao kila siku ya kufanya biashara na kazi ndogo ndogo
 
Wako sehemu nyingi tu wengine katika jiji la DSM wana viwanda bubu uhamiaji wakifika wanachukua tu rushwa na kuondoka zao.
 
Maisha yanataka nini china maisha safi lakini hawatulii nchini kwao kila siku wanapanga mbinu mpya za kupiga pesa.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
Maisha yanatakiwa yaende kwa mtindo huu sasa. Hao wachina wanatumia fursa zilizopo mbele yao. Siyo sisi wabongo ambao miaka nenda tumelala usingizi wa pono.
 
Kumbe huko TCRA Wako Vizuri sana kwenye ongezeko la mapato Nchini
Fikiria kwa miezi takribani miwili tu, mtu mmoja amesababisha upetevu wa mapato ya takribani shilingi 2.2Bilioni.
Wanachi wanahitaji huduma bora hivyo, Ashuhulikiwe kwa mujibu wa sheria!
 
Maisha yanatakiwa yaende kwa mtindo huu sasa. Hao wachina wanatumia fursa zilizopo mbele yao. Siyo sisi wabongo ambao miaka nenda tumelala usingizi wa pono.
Unatete wezi mkuu hilo tukio angefanya muafrika kule china basi wala usingesikia kesi wangemalizana nae kimya kimya kwa njia wanayojua wao.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Unatete wezi mkuu hilo tukio angefanya muafrika kule china basi wala usingesikia kesi wangemalizana nae kimya kimya kwa njia wanayojua wao.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
Mimi simtetei huyo Mchina. Ila nilitamani kuona tukio kama hilo likifanywa na mzawa. Maana hata viongozi wetu nao wanaiba! Shida iko wapi na sisi tukiiba?
 
Back
Top Bottom