Mchina jela miezi mitano kwa kuua tembo 511, Mtanzania jela miaka 60 kwa kukutwa na meno ya tembo na kiboko

Tanzania ukiiba kidogo (vibaka) utapigwa mawe ufe, na ukibahatika kwenda mahakamani utapewa mvua ya miaka.
Ukiiba mabilioni unatenga fungu la kuwalambisha unaachiwa huru!!!! Halafu eti tuna majaji na wanasheria wasomi!!!! Hawaoni hizi double standards?
 
Haki utaipata ukifa kama unaamini life after death
 
Sheria zinasemaje ?

Mara nyingine kuna technicalities nyingi ambazo zinatengeneza loopholes za wenye rupia kuweza kupenyeza kwenye udhia...

Huenda kukutwa na nyara ni kosa kubwa kuliko kuua nyara...
 
Kuua tembo 511 kama ni kweli, ni uhalifu wa kutisha. Ni kama mauaji ya kimbari (genocide). Wachina ni hatari!
 
Nchi hii Ina Tembo kiasi gani hadi uue 500 plus na bado wakabaki? Tuanzie hapo kwanza.
 
Nchi hii Ina Tembo kiasi gani hadi uue 500 plus na bado wakabaki? Tuanzie hapo kwanza.
 
Haki utaipata ukifa kama unaamini life after death
Pesa inanunua haki!! Ukiona una hatia inamaanisha hauna hela ya kutosha, Kama ipo ndio Yale ya Jumanne (aka J4).Tutafute pesa ndugu zangu
 
Sheria zinasemaje ?

Mara nyingine kuna technicalities nyingi ambazo zinatengeneza loopholes za kwenye rupia kuweza kupenyeza kwenye udhia...

Huenda kukutwa na nyara ni kusa kubwa kuliko kuua nyara...
Is this a joke? Au ni Fact!
 
Nchi hii Ina Tembo kiasi gani hadi uue 500 plus na bado wakabaki? Tuanzie hapo kwanza.
Na aliua kwa muda gani and how could they prove kwamba ni 511 na sio 505 ? Hii habari ukiangalia kwa jicho la upembuzi yakinifu linaleta ukakasi hii figure huenda ina typo
 
Kawaida tunapenda kujikomba kwa hizi nchi kubwa kwa hofu ya kunyimwa misaada. Unakuta wageni wanafanya issue very serious kama kubaka au kumkejeli kuu lkn utasikia kapewa masaa 24 aondoke. Mkiamua kuwafunga basi watafanya kila njia kuwatisha, kuahidi kufuta deni nk. Kwao raia mmoja aliyekufa au kufungwa nje ya nchi inaweza kumkosesha mtu uraisi kwenye uchaguzi. Sisi wapo chungu telw walionyongwa au kufungwa nchi mbali mbali na hatufanyi jitihada yoyote kuwatoa. Ndo kama hivi mtu wetu kapigwa mvua while mgeni anapeta.
 
Kalamu umeninukuu vibaya tu wadau wa sheria sio kwamba nimewaita wenyewe la hasha! ndio maana bandiko lipo public!
Lakini hii ni double starndad ya kiwango cha Dunia
 
 
Kalamu umeninukuu vibaya tu wadau wa sheria sio kwamba nimewaita wenyewe la hasha! ndio maana bandiko lipo public!
Lakini hii ni double starndad ya kiwango cha Dunia
Uko sahihi 'mkuu Nanyaro Ephata', najua jukwaa lipo wazi kwa kila mtu mada inapoletwa hapa, hata siye tunaotumia inayoitwa 'common sense' tunajimwaga tu.

Lakini pia, ingependeza sana kama wapo wenye ufahamu wa kitaalam katika eneo husika, kama hili la sheria wangekuwa wanajitokeza kututoa tongotongo zaidi, na kupanua 'common sense' tunayoitumia sisi wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…