Mchina kazubaa wapi kwanini hatengenezi magari ya umeme?

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kulingana na hali ya bei za mafuta kuendelea kupanda siku hadi siku, naiona fursa kubwa kwa soko la magari yanayotumia nishati mbadala kama vile umeme nk.

Mimi binafsi ntakua mteja wa kwanza kwanza kabisa pindi magari hayo yakianza kupatikana maana nimeshachoka na hizi bei pasua kichwa za mafuta na maringo ya wenye sheli.

Nawashauri wakombozi wetu Wachina waingie chimbo haraka sana wazalishe magari madogo mazuri yanayotumia umeme na watapiga hela ndefu maana yatanunuliwa kama njugu!
 
Anasubiri apewe technology na wazungu.. wamarekani Kwa sasa hawatoi technology yao ovyo.. mchina Hana anachojua Zaid ya kukopy
Unawabeza wachina eti wanasubiri mpaka wapewe teknolojia? Katika dunia ya sasa amboapo wanaweza kununua gari moja tu na kulisasambua na kulisoma kila kitu ndo wasubiri kupewa teknolojia? Hawajaamua tu kwa sababu ambazo wanaona wao. Pia bado soko la afrika halijaonesha kuchangamkia magari ya umeme
 
mchawi kwenye EV ni Lithium , ambayo demand yake ni kubwa kuliko supply
Hiyo lithium haina mbadala? Sisi tunachotaka ni gari la umeme hata kama litatumia betri za kawaida mradi litembee. Na liwe linachajiwa kwa chaja za kawaida kama za simu mtu ukiwa nyumbani, ofisini, bar nk unapachika kwenye chaji!
 
Kulingana na hali ya bei za mafuta kuendelea kupanda siku hadi siku, naiona fursa kubwa kwa soko la magari yanayotumia nishati mbadala kama vile umeme nk.

Mimi binafsi ntakua mteja wa kwanza kwanza kabisa pindi magari hayo yakianza kupatikana maana nimeshachoka na hizi bei pasua kichwa za mafuta na maringo ya wenye sheli.

Nawashauri wakombozi wetu Wachina waingie chimbo haraka sana wazalishe magari madogo mazuri yanayotumia umeme na watapiga hela ndefu maana yatanunuliwa kama njugu!
Ziko mapaka bajaji za solar zimejaa, shida kubwa nchi yetu hawaweki sera kuondoa ushuru au kupunguza kwa kiasi kikubwa gari za umeme au bajaji za solar ilikuhamasisha watu kuagiza kwa wingi. Fursa zipo.
 
Kulingana na hali ya bei za mafuta kuendelea kupanda siku hadi siku, naiona fursa kubwa kwa soko la magari yanayotumia nishati mbadala kama vile umeme nk.

Mimi binafsi ntakua mteja wa kwanza kwanza kabisa pindi magari hayo yakianza kupatikana maana nimeshachoka na hizi bei pasua kichwa za mafuta na maringo ya wenye sheli.

Nawashauri wakombozi wetu Wachina waingie chimbo haraka sana wazalishe magari madogo mazuri yanayotumia umeme na watapiga hela ndefu maana yatanunuliwa kama njugu!
Mbona mchina anatengeneza magari ya umeme toka kitambo....

Kuna mtangazaji wa Redio ya Clouds FM anaitwa Kennedy the Remedy, alienda China akawa anatuonesha maisha ya China, wana gari za umeme tena za kisasa, lakini kwa Mujibu wa Kennedy the Remedy, gari zao zinauzwa moja kwa moja Ulaya, China haina soko la moja kwa moja la Magari Afrika, na kama unataka gari lao basi itabidi uende Ulaya ukanunue kisha ulete Afrika. Na kipindi anaongea alikuwa kwenye gari moja la kichina ambalo ni la umeme na lina mfumo wa AI (Artificial Intelligence), ambapo pia linaweza kujiendesha... Lakini linatumia lugha ya Kichina na kuna sauti ya Robot ambae ni msaidizi wako wakati wa kuwasha na kuendesha gari lakini unazungumzia nae kwa kichina tu, vile vile kuna mchina akasema kama unataka lenye mfumo wa lugha ya kiingereza yapo, lakini upelekwa moja kwa moja kwenye soko la ulaya.
 
Chuma moja wapo ni hii hapa Hongqi E-HS9
hongqi-e-hs9-my22-cn-1001x565-(1).jpg

Unawabeza wachina eti wanasubiri mpaka wapewe teknolojia? Katika dunia ya sasa amboapo wanaweza kununua gari moja tu na kulisasambua na kulisoma kila kitu ndo wasubiri kupewa teknolojia? Hawajaamua tu kwa sababu ambazo wanaona wao. Pia bado soko la afrika halijaonesha kuchangamkia magari ya umeme
Kwakweli nadhani imefika wakati sasa wa kuhama kutoka kwenye magari yanayotumia hizi fossil fuels maana sioni future yoyote kila siku ni kupigwa tuu.
 
Kulingana na hali ya bei za mafuta kuendelea kupanda siku hadi siku, naiona fursa kubwa kwa soko la magari yanayotumia nishati mbadala kama vile umeme nk.

Mimi binafsi ntakua mteja wa kwanza kwanza kabisa pindi magari hayo yakianza kupatikana maana nimeshachoka na hizi bei pasua kichwa za mafuta na maringo ya wenye sheli.

Nawashauri wakombozi wetu Wachina waingie chimbo haraka sana wazalishe magari madogo mazuri yanayotumia umeme na watapiga hela ndefu maana yatanunuliwa kama njugu!
Wabongo munapenda kupayuka na misifaa kede kede na ujinga kwa wingii .Unataka gari ya umeme unaijua bei yake .Unataka gari ya Umeme unao umeme wa uhakika je una energy ya kutoshaaaa ,kabla ya kutaka haya pigania umeme na maji ya uhakika pamoja na bara bara hayo mengine yote yatafuata baadae .Munataka maendeleo kwa mdomo tu hakuna kitu hicho .Usione vyaelea vimeundwa.Duniani hakuna ujinga wa umeme kukatwa na kuzimwa including maji pamoja na barabara huo ujinga wa umekatika umeme na kuzimwa ni Tanzania tu .
 
Back
Top Bottom