Mchina yeyote asiyezungumza Kiswahili na Kingereza kufurushwa Kenya

Mchina yeyote asiyezungumza Kiswahili na Kingereza kufurushwa Kenya

Mfumo wa SGR ni mpya kwetu, hivyo lazima wao wahusike pakubwa kwenye uendeshaji wake huku tukirithi kimikakati hatua kwa hatua.
Wao kulazimishwa kuongea lugha zetu ni mojawapo wa kuhakikisha tunarithi mfumo, maana leo analetwa muhandisi Mchina asiyejua Kiswahili wala Kingereza, wanaongea wao kwa wao, wewe unasubiri utafsiriwe alichokisema, lini utakuja kujifunza anachokifanya.
Kama umewahi kufanya kazi yoyote ya kitaalam kwenye nchi ya watu, huwa lazima uonyeshe mikakati ya kupokeza ujuzi wako kwa wazawa na itakuchukua muda gani.
hii inatia uchungu na aibu sana katika uendeshaji wa shughuli zinazofadhiliwa na hawa mabwana hukupa wataalamu wao wenye kujua lugha moja tu,inakuwa ngumu sana katika mawasiliano na usambazaji wa taaluma.
 
Back
Top Bottom