Mchinjita: Kasi ya ongezeko deni la taifa chini ya Rais Samia haijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate uhuru

Mchinjita: Kasi ya ongezeko deni la taifa chini ya Rais Samia haijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate uhuru

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
"Hadi kufikia Aprili 2025 deni la Serikali limefikia shilingi trilioni 107.70 ikilinganishwa na shilingi trilioni 91.7Machi mwaka 2024. Hili ni ongezeko la shilingi trilioni 16. sawa na 17.23% kutoka mwaka wa Fedha uliopita. Ambapo Deni la Nje ni Trilioni 72.94 na Deni la Ndani ni Trilioni 34.76

Kasi ya ukuaji wa Deni la Serikali ya awamu wa Sita chini ya Rais Samia kwa miaka minne imekuwa kubwa sana. Ongezeko hili halijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate uhuru. Amekopa kiasi cha shilingi trilioni 52.73 Tangu alipoingia madarakani.​

Mwenendo huu wa Deni la Serikali unatishia maendeleo ya watu, uwezo wa nchi kujihudumia na kusababisha ukuaji wa uchumi unaoendeshwa na deni (debt driven growth).​

Waziri ameliambia Bunge kuwa eti Deni la Serikali ni Himilivu lakini takwimu zinamkataa, Ilipotufikisha serikali fisadi ya CCM ni kwamba Uwiano wa Deni kwa Pato la Taifa ni 40.3 kwa asilimia 55, hii ni kuonesha kuwa Kama taifa tunakaribia mstari Mwekundu wa hatari ya kukopesheka. Madhara makubwa ya ukopaji huu holela ni kuongeza gharama za kulipa deni kama tunavyoona kwenye bajeti ya mwaka huu." Isihaka Mchinjita akizungumza kuhusu Uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026

​
 
Hadi kufikia Aprili 2025 deni la Serikali limefikia shilingi trilioni 107.70 ikilinganishwa na shilingi trilioni 91.7Machi mwaka 2024. Hili ni ongezeko la shilingi trilioni 16. sawa na 17.23% kutoka mwaka wa Fedha uliopita. Ambapo Deni la Nje ni Trilioni 72.94 na Deni la Ndani ni Trilioni 34.76
🥺🥺🥺🥺
 
Back
Top Bottom