Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mei 14, 2025, Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, amekutana na viongozi wa Ngome ya Wanawake wa kata 20 za Manispaa ya Lindi mkoani Lindi katika kikao kilicholenga kuhamasisha ulinzi wa kura na kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye mchakato wa uchaguzi.
Katika kikao hicho, Ngome ya Wanawake ya Jimbo la Lindi ilitangaza azma yao ya kuanza kazi ya kuzitafuta na kuzihesabu kura kabla ya siku ya kupiga kura, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kuwa kura zote zinahesabiwa na kulindwa ipasavyo. Wamesisitiza kuwa kipindi cha kampeni kiwe uwanja wa mazoezi ya kulinda kura, siyo tu wa kushawishi wapiga kura.
Mchinjita amewaeleza wanawake hao kuwa Operesheni Linda Demokrasia ya chama hicho inalenga kuhakikisha kuwa kila kura inapata heshima na thamani yake. Amesisitiza umuhimu wa wanawake kuchukua nafasi zao kama walinzi wa demokrasia kwa kushiriki kikamilifu katika kulinda matokeo ya uchaguzi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Tunahitaji kila mmoja wenu kuwa askari wa demokrasia. Kura si karatasi tu—ni sauti, ni matumaini, ni hatima ya wananchi. Tunapozilinda kura, tunalinda maisha yetu na mustakabali wa taifa letu," amesema Mchinjita huku akihamasisha mshikamano na ujasiri kwa wanawake hao.