Mchinjita: Serikali iwalipe fidia waathirika wa Mafuriko Rufiji

Mchinjita: Serikali iwalipe fidia waathirika wa Mafuriko Rufiji

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Serikali kusababisha Mafuriko; Waziri wa Nishati awajibishwe na Wananchi wa Rufiji na Kibiti wafidiwe.

Chama cha ACT Wazalendo kinataka hatua kali za uwajibishaji dhidi ya Waziri wa Nishati Ndg. Dotto Biteko kwa kushindwa kuwawajibisha watendaji wake waliosababisha mafuriko Rufiji na Kibiti na wananchi walioathiriwa na uzembe huo walipwe fidia.

Taarifa za wananchi hao kupatwa na mafuriko zilianza tarehe 12 Machi, 2024. Mafuriko ambayo yamesababishwa na Serikali baada ya kufungulia maji kutoka bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere.

Tarehe 14 Machi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndg. Abubakar Kunenge alithibitisha kwa vyombo vya habari kuwa ni kweli Bwawa limejaa na wameyafungulia maji ambayo yameleta na yanaendelea kuleta madhara kwa wananchi kwa kuwa zoezi ni endelevu.

Athari zilizosababishwa hadi sasa ni kama vile kusombwa kwa mazao, kuongezeka kwa idadi kubwa ya viboko na mamba ambao wamejeruhi na kuua watu. Aidha, uharibifu wa Makazi na Miundombinu ya kijamii mfano shule katika maeneo ya Muhuro, King’ongo, Kipoka na Ndutwa. Na kusababisha hofu kubwa ya njaa na kukosa makazi kwa mwaka huu.

Zaidi ya kata 12 za wilaya ya Rufiji na Kibiti zimeathirika na mafuriko hayo. Vijiji 23 vilivyoathiriwa zaidi ni; Mloka, Mwaseni, Mtanza, Msona, Nyaminywili, Kipo, Kipugira, Ndundunyikanza, Ngorongo, Kilimani, Mkongo, Ruwe, Mgomba, Ikwiriri, Umwe, Nyamwage, Chumbi, Muhoro, Utunge, Nyandakatundu, Siasa Utete, Kipoko na King`ongo.

ACT Wazalendo inashangazwa kuona kwenye mradi huu mtambo wa kuzalisha umeme uliowashwa ni mmoja kati ya mitambo 9 wakati taifa linapitia wakati mgumu wa mahitaji ya umeme na huku fedha nyingi za watanzania zimetumika. Waziri anaruhusu maji yaende kuangamiza maisha ya watu na mali zao badala ya kuzalishia umeme wa kutosha kwa ajili ya maendeleo.

Kwa muda wa wiki 3 sasa Serikali inatambua kuwepo kwa janga hili lakini haijachukua hatua zozote za kuwanusuru watu hao na haijatoa pole. Badala yake inaendesha kampeni za kuwahamisha bila kuwafidia. Inasikitisha kuona Serikali inafanya kitendo cha kuwafukarisha wananchi wake lakini haiguswi wala haionyeshi kuwajibika.

Tunajiuliza uzembe huu unafanya kwa jeuri gani? Serikali haikuwa na tathmini ya mazingira na kijamii ya mradi huu? Walivyofungulia maji hawakujua kiasi kinachotoka na athari zitakazosababisha?

Vilevile, itakumbukwa kuwa Serikali ilisema kwamba ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere utasaidia kuondoa tatizo la mafuriko katika baadhi ya vijiji vilivyokuwa vikikumbwa na tatizo hilo kwa kuwa itaweza kudhibiti mtiririko wa maji. Tunashangaa kuona sasa inafungulia maji kiasi cha kusababisha mafuriko makubwa halafu haijihangaishi kudhibiti madhara yake.

Nitafanya ziara ya kutembelea katika maeneo hayo yaliyoathirika na kukutana na waathirika waliokumbwa na mafuriko hayo.

Hivyo ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuchukua hatua zifuatazo;

i. Mamlaka ya uteuzi ichukue hatua za kiuwajibishaji dhidi ya Waziri wa Nishati kwa uzembe uliotokea.

ii. Serikali ifanye tathmini ya athari iliyopatikana tangu kuanza kwa zoezi la kufungulia maji na kuwalipa fidia waathirika wote.

iii. Serikali itoe maeneo mbadala kwa wananchi kwa muda ambao shughuli zao za kiuchumi zimeathiriwa au kuonekana zinaweza kuathiriwa siku zijazo na mwendelezo wa mafuriko.

iv. Serikali itumie fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 270 kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kunufaika na maji hayo katika kuzalishia na kukuza uchumi.

v. Serikali kupitia kwa Wizara ya TAMISEMI zifanye ukarabati na matengenezo ya miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko hayo.

Utekelezaji wa mradi huu unaendelea kuwa mwiba kwa wananchi wa Rufiji na Kibiti badala ya kuwa fursa ya kimaendeleo. Mpaka sasa wananchi hawa hawajaona thamani ya mradi huo mkubwa, hata fedha za wajibu wa mradi kwa jamii (CSR) Shilingi bilioni 270.67 ambazo kwa mujibu wa ripoti ya CAG zilikuwa hazijatolewa na mkandarasi. Tuna wasiwasi fedha hizo zimetumika kwenye mambo mengine au ipo hatari ya kuzipoteza ikiwa mradi utakamilika bila ya hatua muafaka kuchukuliwa.

Imetolewa na;
Ndg. Isihaki Rashid Mchinjita
Waziri Mkuu Kivuli.
April 04, 2024
 
Sawa, wazo zuri

Hao wanastahili kufidiwa maana maeneo yao yamesaxcrifaiwa (duuh, whaat😜!!) kwa maslahi mapana ya mradi wa umeme wa nchi nzima.

Hivyo inaleta mantiki kufidiwa na watu kwa maana ya serikali
 
imani yangu kubwa kwa chama cha mapinduzi sina shaka kwa maafa yaliyo wakumba watanzania wenzetu rufiji serikali ni sikifu na inamipango sahihi nyakati zote
 
kila siku nitasisitiza watu weusi hatukuumbwa na akili. imagine hiyo ndio serikali inayoongoza watu wanafanya mambo ya kijinga hali ikoje kwa wananchi wenyewe?
 
Kama wamehamisha wamasai maelfu kwa kuwajengea nyumba na cash juu,wanashindwa nini kuhamisha hao waliopo kwenye hilo bonde kwa maslahi ya nchi nzima?
 
imani yangu kubwa kwa chama cha mapinduzi sina shaka kwa maafa yaliyo wakumba watanzania wenzetu rufiji serikali ni sikifu na inamipango sahihi nyakati zote
hadi hapo imeshafeli. suala la athari za kimazingira lilipigiwa kelele toka mwanzoni mwa mradi. haya madhara yanayotokea yalikua yanafahamika. ni dharau na kukosa akili kwa watawala wenu hapo ukimani.
 
Hapa mnajidai wakali ukifika wakati mnawasifu na kuwapa kura zenu kisha mnaanza kulalama tena!
 
Kama wamehamisha wamasai maelfu kwa kuwajengea nyumba na cash juu,wanashindwa nini kuhamisha hao waliopo kwenye hilo bonde kwa maslahi ya nchi nzima?
Itakuwa hajapatikana mwarabu kuja kuwekeza kwenye hilo bonde.
 
I Second.
Nafikiri kuna jambo lenye kuweza kuleta tija, hata hapo baadae hususani wakati maji yameongezeka.

Mfano mzuri walioutoa ACT ni Kilimo, yaani kilimo cha Umwagiliaji.

Mimi Syllo napendekeza Mabwawa kadhaa yajengwe pembezoni/karibu na vijiji ili yawe yanaweza kuchukua ongezeko lolote la maji.
iii. Serikali itoe maeneo mbadala kwa wananchi kwa muda ambao shughuli zao za kiuchumi zimeathiriwa au kuonekana zinaweza kuathiriwa siku zijazo na mwendelezo wa mafuriko.

iv. Serikali itumie fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 270 kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kunufaika na maji hayo katika kuzalishia na kukuza uchumi.


Na wasiishie hapo tu, mabwawa hayo yatumike pia Kuzalisha samaki-Samaki wakukaushwa baadae, yaani wakavu kwani mazingira ya kusini yanafaa.
 
ACT- Wazalendo wataka serikali ilipe fidia kwa wananchi walioathiriwa na maji yaliyofunguliwa bwawa la Julius Nyerere


View: https://m.youtube.com/watch?v=HGdAFy8xCDU

Viongozi hao wa ACT - Wazalendo walifika Rùfiji mkoa wa Pwani kukagua athari zilizoletwa na maamuzi ya serikali kulinusuru bwawa la umeme na hatua hiyo imesababisha mashamba, mifugo, nyumba na mali za wananchi kuharibika....

Viongozi hao walitumia maboti na mitumbwi kukagua athari ya hatua ya serikali kufungulia maji, na kushangaa vipi wananchi wasifidiwe kwa hatua hiyo iliyosababisha maafa ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Rufiji

Kama mkulima alitegemea kuvuna tani 5 za mpunga, serikali itoe fidia stahiki ya jasho la mkulima .....
 
1712526573639.png
 
Back
Top Bottom