Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Kwani kuna watu wanajua Kicheko wa mchiriku ndio huyo wa E-fm?,doooh!.
 
Nyimbo hii wenye Chaukucha(watoto wadogo waliokomaa vichwa),lakini wengi wanaitambulisha vibaya kwamba ni ya Jagwa.
 
Hisani walileta mapinduzi makubwa sana kwenye mchiriku

Na laiti Mkapa asingeupiga marufuku basi sasa hivi mchiriku ungekua zaidi ya bongo flavour
Hisani ndio waasisi wa mnanda,wameutoa kutoka kwenye Chakacha.
 
Wakati Mwembe Yanga biashara ya machungwa inatamba,mameza kama yote.
 
I hope someone angetengeneza documentary ya historia ya muziki wa mchiriku
Mimi niko mbioni kufanya hivyo,kwani nina historia iliyoshiba ya mziki huu na nawajua watu wengi waliokua ni wadau wakubwa ambao wanaweza kunirekebisha nikoseapo.Halafu naupenda mziki huu.
 
Mimi ninayo ila nashindwa kuapload humu, nitumie namba ya WhatsApp nitakutumia. Halafu kuna WhatsApp group la Mchiriku lipo ukitaka utaunganishwa, huko utapata kila unachotaka kuhusu Mchiriku.
Naomba uniunge what's up group la mchiriku, 0713963812
 
Yap,hongera kwa kuwaweka sawa .Marumbambano na zogo kubwa(Kondakta)wenyewe ni Chaukucha,kundi lililoimarishwa na maprofesheno waliojitoa Jagwa baada ya kurumbana.Humu zimepigwa dumbaki kali sana na za kuchezeka.
 
Wimbo wa ajali ya kibada nani aliimbiwa?

Ni kweli wasanii wa mnanda waligongwa na gari walikuwa waporaji?
Washkaji karibuni maskani
Lakini msione kimyaa
Said dabani hamumuoni
Amefariki dunia kwa ajali ya gari
Ambayo imetokea buguruni
Said dabani kaacha majonzi
Hata kwa mzazi mwenzie
Pili mama Ali amebaki analia
Said dabani kaacha majonzi
Kwa kisia babu na fikiri fika enock wa mbeya na magomba wanalia
Saidi Dabani kaacha majonzi
Kwa bwana tondo na bwana Ema uvuruge na omar wanalia
Na siri ya mungu kubwa siri haeleweki sifahamu safari hii nani atatangulia kama mimi bwana ommy au wewe bwana tondo .
 

Naskia kuna wanamuziki wa mnanda vibaka ambao walikuwa wanalala barabarani magari yakisimama wanayapora siku hiyo huko Kibada Kigamboni dereva alisimamishwa lakini hakusimama akawagonga wote wakafa,jamaa akawaimbia huo wimbo wa Ajali ya Kibada

 
Bangusilo tutimke, masela tutimke... Moody boy tutimkeee.. Kitambo. Ila sasa hivi Jagwa wanapiga mpaka kwenye stage za Ulaya. Mambo yamebadilika aha.
Mkuu huu wimbo unaitwaje?naupenda sana ila sijajua jina lake
 
Unaitwa Beach Boy na umeimbwa na Marehemu Omary Omary akiwa na bendi ya Atomic na sio Jagwa.
Ahsante mkuu,ila nimeutafuta mtandaoni sijaupata,Kama unao nauomba,mimi jagwa ndio bendi yangu pendwa so nikajua wameimba wao
 
Mimi bhana naomba kujua hawa waliokuwa wanatajwa kwenye nyimbo za jagwa walikuwa na cheo gani kwenye bend,
1.Kamongo Manja(Manjalino)
2.Jolijo
3.Saidi Misape
4.Bonge mzito
4.Baba Dullah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…